Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Mkuu mbona umeni quote kitu sijaongelea kiongozi au ndio stress kiongozi?
 
Nini dhumuni la mleta mada? Kutisha, au kumwongezea akili au uwezo mtajwa?

Nimeshindwa kuelewa dhumuni la uzi.
 
Kawaida kila nchi ina maafisa usalama luluki.

Umuhimu wao ni clearance ya security level.

Kuna wapasha habari wa source moja na kunawapokea habari wa source tofauti.

Kuna habari zinakuwa shared na watu wachache sana.

Na watu muhimu ni analysts kwenye usalama wa taifa au watu wenye uwezo wa kwenda kutafuta umbea huku wakiweka maisha yao rehani.

Vinginevyo labda Tanzania, otherwise nchi kama uingereza senior civil servants wote ni usalama wa taifa.

Ni uelewa wetu mdogo tu wa national security.Sasa Kitila ana akili gani ya kusaidia nchi ata kama usalama wa taifa zaidi ya kupeleka umbea.

Intelligence ni mchezo wa watu wenye akili nothing else, yaani wewe mtu kama Mavunde au Katambi wanafaida gani kwenye usalama.

Usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili, Key players ni analysts na watu wanaohatarisha maisha yao kuleta habari.

Wengineo wambea tu.

Usalama wa taifa sio shughuli ya mzaha, kama huyo mama yenu alivyoifanya kulinda madaraka yake.
 
Tanzania ailewi maana ya usalama wa taifa.

That’s not a joke
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa πŸ’― ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Kuwa maofisa wa TISS, kwa bongo hii, hakuna maana, hainatofauti na kuwa chawa kama mwijsku, baba levo, Gerald, Doto magari,,,zembwela, Kitenge, ni kupayuka tu, story ni ccm, na ni kama mama, yanga na Simba,
Nchi imeoooza hii, kila kenge mtasni ni TISS, hata vibaka wa uvccm,na wao ni TISS!
 
Kwa vile nimezaliwa familia ya Tiss baba na mama, then it is expected na mimi kuwemo, kwetu tumezaliwa 8, hivyo hatuwezi wote 8 tuwe huko!. Ndugu zangu 5 wako serikalini sisi 5 sekta binafsi. Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?
P
Mkuu Pascal, nadhani si mbaya ukiwa miongoni mwao la muhimu ni kuficha identity yako na kufanya kazi yenye maslahi kwa taifa.
 
Wa humu nao huwa wanatoa πŸ”«?
 
Pascal kati ya vitu ambavyo nadhani bado tunapaswa kuvitazama upya kwenye taasisi ni kufanya maamuzi ya ku-recrute watu kutoka kwenye majeshi yetu kwa asilimia kubwa sana.
Kule nyuma kulikuwa na system pamoja na kupitia jeshini vijana waliandaliwa kuanzia walipokuwa shule na vyuo.Hii ilitoa watu cream, loyal, very confidential,talented, focused and cheer will.
Haikuwa rahisi hata kidogo kumfahamu mtu ambaye yuko kwenye system labda wanaotumika kwa nafasi zao kama DG,RSO,DSO na hata informers haikuwa rahisi kuwajua kwasababu ni information feeders.

Kwenye kazi za awali za kukusanya data, kutafsiri data na kushauri kwa mamlaka husika kabla ya kilichoongezeka kwenye sheria mpya haikuwa rahisi kumsikia mtu wa Tiss anajitaja kuwa ni mtu wa Tiss.
Kuna mahali kwenye miiko tumepungua tujisahihishe kama taifa na taasisi.

Pongezi kwa kazi njema na ushirikiano kwa mamlaka nyingine kama kwenye military operations, administration nk.

Mmefanya kazi kubwa sana awamu fulani katika nyanja za uchumi na kijamii.
Nafasi yenu ni kubwa kwenye kui-influence nchi positively kwenye maeneo mengi.
Mungu awasaidie.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa πŸ’― ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Ila si niliwahi kusikia kwamba Hawa jamaa Huwa hawajulikani kirahisi sasa ilikuwaje kwa huyu mwamba
 
Sisi tutawataja wale ambao hawafanyi kazi kwa manufaa ya umma. Hakuna mtu ambaye anafanya kazi kwa manufaa ya uma halafu aende kutetea wizi wa kura! Huyu lazima alipuliwe.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa πŸ’― ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.


Huyu mwandishi mkongwe naye ni usalama wa taifa lakini alianza kuchuja baada ya kuwa Chawa wa Lowassa

MUHIDIN MICHUZI

 
Ongezea pia viongozi wa dini mapadre na mashekhe
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa πŸ’― ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Ilitakiwa kila mtanzania aishi kama Israel na north Korea. Akifika darasa la tatu anaanza rasmi mafunzo ya mtaala wa kijeshi na uzalendo kwa kuilinda nchi yake. Sijawahi kusikia muisrael msaliti kwa nchi yake. Usalama wa Israel unawahusu waebrania wote. Ipende nchi, itumikie na kuilinda.
 
Zamani nilikuwa nikisikia mtu ni usalama wa taifa nilikuwa namuona wa maana kweli. Lakini baada ya kujua ukweli kuwa nao ni walamba miguu ya viongozi, naona hata kinyaa nikisikia mtu akitaja hao usalama wa taifa.
Usalama wa Taifa kwa mfumo wetu umekaa kichawa chawa inategemea sana na Rais aliyopo madarakani kama ni wa amsha amsha mfumo unakua active sana ndo Rais akipatikana aliepoa kama uji nao uwa unapoa kumbuka kipindi cha JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…