Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Daaah mkuu hii pia inanikuta sasa hapa job napojitolea. yani ni hatri sababu Mimi ni mkimya ,mpole, nina kipawa cha kukutambua kwa kukuangalia USO au macho kama unaniwazia mabaya then nitakwambia. Pia napokuwa na changamoto ya ofisi fulan huwa siogopi kuonana na kiongozi husika na kama na namba yake nitampigia hivyo nimejikuta na namba nyingine za viongozi hasa mawaziri kwahyo hii inanipaga shida ingawa naipenda sana hii kazi sababu binafisi najijua Mimi ni mpelelezi na mdadisi sana na nikiwa nimekiamulia kitu siku haiishi nimekipatia ufumbuzi . mkuu nimekuelewa sana sababu hali hii inanikuta now, inafika hatua unaomba kazi unanyimwa ukihofiwa kwamba huenda ukawa kwenye system. Same time natamani sasa ningekuwa kweli
Mkuu mbona umeni quote kitu sijaongelea kiongozi au ndio stress kiongozi?
 
Nini dhumuni la mleta mada? Kutisha, au kumwongezea akili au uwezo mtajwa?

Nimeshindwa kuelewa dhumuni la uzi.
 
Kawaida kila nchi ina maafisa usalama luluki.

Umuhimu wao ni clearance ya security level.

Kuna wapasha habari wa source moja na kunawapokea habari wa source tofauti.

Kuna habari zinakuwa shared na watu wachache sana.

Na watu muhimu ni analysts kwenye usalama wa taifa au watu wenye uwezo wa kwenda kutafuta umbea huku wakiweka maisha yao rehani.

Vinginevyo labda Tanzania, otherwise nchi kama uingereza senior civil servants wote ni usalama wa taifa.

Ni uelewa wetu mdogo tu wa national security.Sasa Kitila ana akili gani ya kusaidia nchi ata kama usalama wa taifa zaidi ya kupeleka umbea.

Intelligence ni mchezo wa watu wenye akili nothing else, yaani wewe mtu kama Mavunde au Katambi wanafaida gani kwenye usalama.

Usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili, Key players ni analysts na watu wanaohatarisha maisha yao kuleta habari.

Wengineo wambea tu.

Usalama wa taifa sio shughuli ya mzaha, kama huyo mama yenu alivyoifanya kulinda madaraka yake.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Kuwa maofisa wa TISS, kwa bongo hii, hakuna maana, hainatofauti na kuwa chawa kama mwijsku, baba levo, Gerald, Doto magari,,,zembwela, Kitenge, ni kupayuka tu, story ni ccm, na ni kama mama, yanga na Simba,
Nchi imeoooza hii, kila kenge mtasni ni TISS, hata vibaka wa uvccm,na wao ni TISS!
 
Kwa vile nimezaliwa familia ya Tiss baba na mama, then it is expected na mimi kuwemo, kwetu tumezaliwa 8, hivyo hatuwezi wote 8 tuwe huko!. Ndugu zangu 5 wako serikalini sisi 5 sekta binafsi. Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?
P
Mkuu Pascal, nadhani si mbaya ukiwa miongoni mwao la muhimu ni kuficha identity yako na kufanya kazi yenye maslahi kwa taifa.
 
Wakuu wa wilaya

Wakuu wa mikoa

Mabalozi

Viongozi wa vyama vya upinzani...

...na wengineo mara nyingi huwa ni TISS. Zamani walikuwa wanaandaliwa vizuri hawatambuliki ila hawa wa sasa mkiwa baa tu mkazinguana anatoa pistol na kuanza kuropoka...

Hata humu JF nawafahamu kwa asilimia 100 mabinti watatu na bro mmoja (siyo Pasikali)...😁🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
Wa humu nao huwa wanatoa 🔫?
 
Mkuu Mundu, Kamundu , kwa lengo la kusaidiana tuu, kukusaidia wewe na wengine wasiojua, kumtaja kwa majina mtu yoyote wa TISS na kumu expose kuwa ni TISS, huyo mtu akiwa ni TISS kweli, then kumtaja kwa jina ni kosa la jinai!.

I can just imagine, kama sisi tuliajaliwa jicho la tatu, ma Tiss tunawajua kwa kuwaona tuu sura, je tungewataja ma Tiss wote tunaowajua, tungebaki salama?
Huwezi kutoboa boti mnayasafiria. Ikizama mnakufa wote!, au kulikata tawi la mti uliolalia!.

Kwa taarifa yako ma TISS ni wengi kuliko unavyodhania hata Sultani naye ni Tiss, hata Mkuu nanilii pia ni Tiss
Ila sio kila Tiss ni Tiss

Kuna Tiss wa aina 3.
  1. Staff hawa ni waajiriwa, wafanyakazi wa Tiss, ni watumishi wa mishahara, hawa staff wako wa aina mbili, kuna open staff, hawa wanajulikana kama DGIS na maofisa wote wa TISS wanaojulikana kama RSO, ma DSO etc, hawa kuwataja hakuna tatizo, ila kuna ma SS, secret service, hawa hawatakiwi kujulikana, na ikitokea ukawajua, huruhusiwi kuwataja!.
  2. Viongozi wote, wateuliwa wote na watendaji wote, hawa ni ma Tiss kwa mujibu wa positions zao, wakiwemo mabenki yote yana mtu wa kitengo cha FIU hawa ni ma TISS, taarifa ya FIU lazima ipite kwa bank manager hivyo mameneja wote wa financial institutions zote ni ma Tiss.
  3. Informers, hawa ni watu wa kawaida wanakuwa recruited kuripoti Tiss na kulipwa posho tuu, huku wakiendelea na shughuli zao.
NB. Mimi nina damu ya TISS kwenye veins zangu kwa wazazi wangu wote wawili, na tumezaliwa 8, haiwezekani sisi wote nane tukawamo!. Kunidhania mimi ni mmoja wao rukhsa na angalia hapa ninavyoisifia ofisi yangu TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hapa namtishia bosi wangu Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Na kunapotokea matishio ya kiusalama, badala ya kuripoti ofisini, mimi naripoti jf Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Boss wa TISS ni CinC, mwenyewe amepania ile mbaya 2025-2030, mtumishi wa idara anaweza kweli kuandika hivi ?. Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

Boss wako anajipanga kwa mserereko wa 2025, kijana wake anaweza kupandisha kitu kama HII?.

P.
Pascal kati ya vitu ambavyo nadhani bado tunapaswa kuvitazama upya kwenye taasisi ni kufanya maamuzi ya ku-recrute watu kutoka kwenye majeshi yetu kwa asilimia kubwa sana.
Kule nyuma kulikuwa na system pamoja na kupitia jeshini vijana waliandaliwa kuanzia walipokuwa shule na vyuo.Hii ilitoa watu cream, loyal, very confidential,talented, focused and cheer will.
Haikuwa rahisi hata kidogo kumfahamu mtu ambaye yuko kwenye system labda wanaotumika kwa nafasi zao kama DG,RSO,DSO na hata informers haikuwa rahisi kuwajua kwasababu ni information feeders.

Kwenye kazi za awali za kukusanya data, kutafsiri data na kushauri kwa mamlaka husika kabla ya kilichoongezeka kwenye sheria mpya haikuwa rahisi kumsikia mtu wa Tiss anajitaja kuwa ni mtu wa Tiss.
Kuna mahali kwenye miiko tumepungua tujisahihishe kama taifa na taasisi.

Pongezi kwa kazi njema na ushirikiano kwa mamlaka nyingine kama kwenye military operations, administration nk.

Mmefanya kazi kubwa sana awamu fulani katika nyanja za uchumi na kijamii.
Nafasi yenu ni kubwa kwenye kui-influence nchi positively kwenye maeneo mengi.
Mungu awasaidie.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Ila si niliwahi kusikia kwamba Hawa jamaa Huwa hawajulikani kirahisi sasa ilikuwaje kwa huyu mwamba
 
Sisi tutawataja wale ambao hawafanyi kazi kwa manufaa ya umma. Hakuna mtu ambaye anafanya kazi kwa manufaa ya uma halafu aende kutetea wizi wa kura! Huyu lazima alipuliwe.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.


Huyu mwandishi mkongwe naye ni usalama wa taifa lakini alianza kuchuja baada ya kuwa Chawa wa Lowassa

MUHIDIN MICHUZI

1736277509406.png
 
Wakuu wa wilaya

Wakuu wa mikoa

Mabalozi

Viongozi wa vyama vya upinzani...

...na wengineo mara nyingi huwa ni TISS. Zamani walikuwa wanaandaliwa vizuri hawatambuliki ila hawa wa sasa mkiwa baa tu mkazinguana anatoa pistol na kuanza kuropoka...

Hata humu JF nawafahamu kwa asilimia 100 mabinti watatu na bro mmoja (siyo Pasikali)...😁🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
Ongezea pia viongozi wa dini mapadre na mashekhe
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Ilitakiwa kila mtanzania aishi kama Israel na north Korea. Akifika darasa la tatu anaanza rasmi mafunzo ya mtaala wa kijeshi na uzalendo kwa kuilinda nchi yake. Sijawahi kusikia muisrael msaliti kwa nchi yake. Usalama wa Israel unawahusu waebrania wote. Ipende nchi, itumikie na kuilinda.
 
Zamani nilikuwa nikisikia mtu ni usalama wa taifa nilikuwa namuona wa maana kweli. Lakini baada ya kujua ukweli kuwa nao ni walamba miguu ya viongozi, naona hata kinyaa nikisikia mtu akitaja hao usalama wa taifa.
Usalama wa Taifa kwa mfumo wetu umekaa kichawa chawa inategemea sana na Rais aliyopo madarakani kama ni wa amsha amsha mfumo unakua active sana ndo Rais akipatikana aliepoa kama uji nao uwa unapoa kumbuka kipindi cha JPM
 
Back
Top Bottom