Hiii ndiyo nzuri weka chakula kwenye sahani weka mezani Ila matunda weka kwenye sinia weka mezani chukua sahani yako jipimie matunda kwa kadri uwezavyo shushia na glass ya maji. Hii safi big up kwa wazo zuri mjini huku maisha magumu.Au mna badilisha utaratibu, mama anampakulia kila mtu jikoni, ukiwakaribisha chakula kiko kwenye sahani tayari.
[emoji23][emoji23][emoji23] watu wana maujasiriAisee nimecheka sana...lakini huo ndio ukweli! Mimi nilipata mgeni last two weeks lakini alikuwa wakipekeee...alikuwa anakuja na Taulo tena akiwa kifua wazi Mezani! Muda wote alikuwa akizunguka na Taulo na bila Vest ndani hata pale ambapo walikuja wageni zake kumtembelea! Hakika nilikuwa na wakati mgumu sana! Lakini finally nilitumia diplomasia kumuondoa!
Sky Eclat Kupakua chakula bila kujali wanao baki ni ujinga wa kukosa malezi Bora kutoka kwa wazazi, muhimu kwamba kitu kinapo kuwa kidogo mnagawana kidogo kidogo ili kila mtu apate.
Ila Tabia nyingine ambayo siipendi ni kubakiza chakula kwenye sahani, Kuna watu kubakiza chakula kwenye sahani wanaona fashion, wanachukia kingi cha nini Kama hawawezi kumaliza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii tabia ya kubakiza chakula inaniuma Sana Yani, mwisho wa siku kinaishia kumwaga tu.Hii tabia Kwa kweli mie nimkali sana hasa uharubifu wa vyakula, mgeni mwingine anachukua samaki wengi na wali ama ugali..na anabakisha kwa sahani wali na ugali kwa kweli hapana!
Watoto wangu wote wanajua kuacha chakula kwa sahani ni dhambi kwahyo wanajipakulia kinachowatosha hadi miaka 3.5 anafanya hvyo. Nashukuru Mungu hawataniaibisha huko kwa majirani.
Kuna mtt wa jirani yangu jaman darasa la 6 ila chakula anayokula ni zaidi mtu mzima mwenye familia, mama yake anasema hataki aende hata kwa ndugu.
[emoji16][emoji16] aisee na ukute li kifua lake lina vinywele nywele vile vya mbalimbal kama inzi, watoto wanabaki kushangaa tuAisee nimecheka sana...lakini huo ndio ukweli! Mimi nilipata mgeni last two weeks lakini alikuwa wakipekeee...alikuwa anakuja na Taulo tena akiwa kifua wazi Mezani! Muda wote alikuwa akizunguka na Taulo na bila Vest ndani hata pale ambapo walikuja wageni zake kumtembelea! Hakika nilikuwa na wakati mgumu sana! Lakini finally nilitumia diplomasia kumuondoa!
Kulima mpaka kuvuna sio rahisiii mkuuuYaan hawa jamaa wamekariri life sababu wao wanalima na kuvuna wanahis na huku hivyohivyo ni rahis tu
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Mkuu hii tabia ipo sana, ukishasikia Hilo neno shukuru Mungu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kaka hapo kwenye shemeji umenipatia nilishapata kumuona kima mmoja mwenye tabia hizo
Hapana mkuu kutokana na hali halisi siku hizi hatutumii hilo neno, ni karibu chakula tugawane hivyo hivyo mapungufu tusameheane basi, hapo sasa wageni wanajiongeza wenyewe.Ulivomkaribisha si ulimwambia ajiskie yupo nyumbani?
Wenyewe chakula tunapima kama ni kipimo kipo akija mgeni mnaongeza chake na nyama ni vipande viwili ikizidi vitatu na samaki kipande kimoja ndio maisha tuliyoyazoea yeye aje apange yake kama ni Mimi yeye achukua vipande vitatu siongezi hadi aone kabisa wawili wamekosa ili kesho asirudie makosaWatu wa Dar acheni uchoyo kwanini msipike chakula kingi?..ndo mana mnakufa kwa stress mana moyoni mmejaza kila aina za uchoyo.
#MaendeleoHayanaChama
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Sure ni tabia mbaya...au ukute jitu linatafuna mdomo wazi Kama hondohondo ...Ukiwa peke yako hamna tatizo, fikiria unakula na baba mkwe wewe uko Instagram. Mwisho watu wote wanamaliza Kula unabaki wewe.
Kwa hiyo nyumbani anakula hawafikirii wengine? Ni ubinafsi tu ndio uliomjaa.Ulivomkaribisha si ulimwambia ajiskie yupo nyumbani?