Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Mmenikumbusha mbali kuna wageni wawili walikuja nyumbani sasa tuna utaratibu wa kupakua chakula cha wote mezani wacha wale ugali wote wa watu sita tena usiku ikabidi tuanze kupika mwingine tena
 
Au mna badilisha utaratibu, mama anampakulia kila mtu jikoni, ukiwakaribisha chakula kiko kwenye sahani tayari.
Hiii ndiyo nzuri weka chakula kwenye sahani weka mezani Ila matunda weka kwenye sinia weka mezani chukua sahani yako jipimie matunda kwa kadri uwezavyo shushia na glass ya maji. Hii safi big up kwa wazo zuri mjini huku maisha magumu.
 
Aisee nimecheka sana...lakini huo ndio ukweli! Mimi nilipata mgeni last two weeks lakini alikuwa wakipekeee...alikuwa anakuja na Taulo tena akiwa kifua wazi Mezani! Muda wote alikuwa akizunguka na Taulo na bila Vest ndani hata pale ambapo walikuja wageni zake kumtembelea! Hakika nilikuwa na wakati mgumu sana! Lakini finally nilitumia diplomasia kumuondoa!
[emoji23][emoji23][emoji23] watu wana maujasiri
 
Ukinikaribisha chakula Mara
Nikaribishe tena huenda sijaskia vizuri
 
Usimuonee aibu mtu ambaye haoni aibu.mpe ukweli hapo hapo akizira kula ni juu yake maana hana AIBU
 
Mara nyingi inasababishwa na umaskini wa muhusika, hizi tabia wanazo sana watu wanaotokea uswahilini, mfano unakuta sikuku hizi za kidini yaani mtu atazunguka hata sehemu 10, zote anataka kula, mpaka unamuonea huruma anavyopata tabu
 
Hii tabia Kwa kweli mie nimkali sana hasa uharubifu wa vyakula, mgeni mwingine anachukua samaki wengi na wali ama ugali..na anabakisha kwa sahani wali na ugali kwa kweli hapana!

Watoto wangu wote wanajua kuacha chakula kwa sahani ni dhambi kwahyo wanajipakulia kinachowatosha hadi miaka 3.5 anafanya hvyo. Nashukuru Mungu hawataniaibisha huko kwa majirani.

Kuna mtt wa jirani yangu jaman darasa la 6 ila chakula anayokula ni zaidi mtu mzima mwenye familia, mama yake anasema hataki aende hata kwa ndugu.
Sky Eclat Kupakua chakula bila kujali wanao baki ni ujinga wa kukosa malezi Bora kutoka kwa wazazi, muhimu kwamba kitu kinapo kuwa kidogo mnagawana kidogo kidogo ili kila mtu apate.

Ila Tabia nyingine ambayo siipendi ni kubakiza chakula kwenye sahani, Kuna watu kubakiza chakula kwenye sahani wanaona fashion, wanachukia kingi cha nini Kama hawawezi kumaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii tabia Kwa kweli mie nimkali sana hasa uharubifu wa vyakula, mgeni mwingine anachukua samaki wengi na wali ama ugali..na anabakisha kwa sahani wali na ugali kwa kweli hapana!

Watoto wangu wote wanajua kuacha chakula kwa sahani ni dhambi kwahyo wanajipakulia kinachowatosha hadi miaka 3.5 anafanya hvyo. Nashukuru Mungu hawataniaibisha huko kwa majirani.

Kuna mtt wa jirani yangu jaman darasa la 6 ila chakula anayokula ni zaidi mtu mzima mwenye familia, mama yake anasema hataki aende hata kwa ndugu.
Hii tabia ya kubakiza chakula inaniuma Sana Yani, mwisho wa siku kinaishia kumwaga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee nimecheka sana...lakini huo ndio ukweli! Mimi nilipata mgeni last two weeks lakini alikuwa wakipekeee...alikuwa anakuja na Taulo tena akiwa kifua wazi Mezani! Muda wote alikuwa akizunguka na Taulo na bila Vest ndani hata pale ambapo walikuja wageni zake kumtembelea! Hakika nilikuwa na wakati mgumu sana! Lakini finally nilitumia diplomasia kumuondoa!
[emoji16][emoji16] aisee na ukute li kifua lake lina vinywele nywele vile vya mbalimbal kama inzi, watoto wanabaki kushangaa tu
 
Kweli, juzi sikukuu niliamua nichemshe nyama bila kukatakata kwa lengo itaenda mezani yote halafu kaka mkubwa atakatakata,

Heeee mmoja yuko mi napenda nyama si kachota pande hilooo kaweka pembeni anajilia,

Huwezi ficha tabia lazima ionekane tu.
 
Hapa kuna mawili. Ikiwa umealikwa chakula kwamba leo chakula njoo nyumbani ni jukumu la mwenyeji kujiandaa chakula cha kutosha maana amekualika, ila ikitokea kwa bahati umefika sehemu na ukakaribishwa chakula maana imebidi wa kwambia karibu lakini hawakujiandaa basi nakushauri sio vizuri kukaribia unaweza kutoa sababu tu hata kama una njaa huo ndio ustaarabu na kama imetokea umekubali basi chukuwa kidogo sana kuonesha heshima nadhani hii ndio njia sahihi. Maana unaweza kuwa umekaribishwa lakini sio kwa kupenda watu wanasema huyu naye hajaona wakati wa kuja ila wakati wa chakula mioyo sio misafi kuepuka kataa kukaribia hata kama una njaa hapo heshima yako juu na huyo aliyekuwa anakukaribisha huku roho nyeusi itamsuta. Ila tabia za kula mezani na wenzako halafu kutwa umeshikilia simu nachukia sana au kuongea na simu. Mimi nikitoka na family sharti moja simu pembeni inakera sana badala ya kuongea mko busy kuongea na watu wa mbali. Watoto ni jukumu la wazazi kuwafundisha tabia za kula na watu.
 
Watu wa Dar acheni uchoyo kwanini msipike chakula kingi?..ndo mana mnakufa kwa stress mana moyoni mmejaza kila aina za uchoyo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Wenyewe chakula tunapima kama ni kipimo kipo akija mgeni mnaongeza chake na nyama ni vipande viwili ikizidi vitatu na samaki kipande kimoja ndio maisha tuliyoyazoea yeye aje apange yake kama ni Mimi yeye achukua vipande vitatu siongezi hadi aone kabisa wawili wamekosa ili kesho asirudie makosa
 
Back
Top Bottom