Kishua inatakiwa upewe introduction kutoka kwa mtu anayewajua wote wawili.
Yani hutakiwi kumvamia mtu tu humjui.
Kwa mfano. Mwanamme una rafiki yako mwanamme kama wewe, ana girlfriend wake, yule girlfriend wa rafiki yako anakujua vizuri, anakujua uko single, na yeye ana rafiki yake anayemjua yuko single, halafu anaona kuna tabia fulani mnafanana mtafaa kuwa pamoja, basi huyo girlfriend wa rafiki yako anatoa mutual introduction mnajuana na huyo rafiki yake, halafu mnajiongeza wenyewe.
Yani hapo mna mtu ambaye anawajua wote katoa pande, huyo mtu si rahisi kutoa pande sehemu yenye lawama.
Ndiyo washua walivyofanya hivyo, yani kumvamia mtu barabarani ilikuwa kituko.
Siku hizi watoto wanepindua meza.