Kuna wanawake ukiwaomba namba ya simu wanamajibu mabaya sana

Kuna wanawake ukiwaomba namba ya simu wanamajibu mabaya sana

Hivi kwa sasa kuna mtu anapata shida kabisa kupata namba ya mwanamke? Kati ya kitu rahisi miaka hii kukipata basi ni namba ya mwanamke ila sasa unaweza kuiblock mwenyewe! Mimi sasa hivi nimeacha kabisa mambo ya kuomba namba!
 
Ulivyosema kakuita mweusi mawazo yameenda mbali naona kama kakuonea maana hapa kwa I'd yako ni mweupe sana kijeiefu tukija pm yani tunarusha mistari tukitegemea ukikubali tutakutana na mtu mweupe kama huyo.

Japokua tunaweza kuokota dodo tukakutana na Black beauty
Ndio mana huwa mnapigwa na vitu vizito unawezaje kumtamani mtu kisa dp au umesahau kama tunatumia utambulisho fake humu?
 
Sema hujui kuanzisha mahusiano. Kwahiyo ukikaa naye Mwendokasi ndio unarukia kuomba namba atagawia wangappi? Fikiri mara mbili. Eti binti anapita zake wewe unamwambia naomba namba zako. Akikupa ni malaya huo.

Kama hujui nenda kwa bibi @Faizafox akufundishwe namna ya kutongoza
Rudia hoja yako kwanza maana naona hata hoja yako uliyoandika huijui maana unajipinga mwenyewe tu hapa

Jifunze kutumka ubongo
 
Hivi kwa sasa kuna mtu anapata shida kabisa kupata namba ya mwanamke? Kati ya kitu rahisi miaka hii kukipata basi ni namba ya mwanamke ila sasa unaweza kuiblock mwenyewe! Mimi sasa hivi nimeacha kabisa mambo ya kuomba namba!
Unreacha mambo ya kuomba namba unafanyaje
 
Ila namba zinaombwa wapi? Unadhani utapata nafasi ya kukutana Kila mahala?

Wewe ndio mshamba na aibu zako ,hata hivyo mbinu ziko nyingi Kwa watu kama.wewe mwenye aibu unanitajia nakariri kichwani.
Anadhani kuna sehemu special kumetengwa watu wanaenda kuombana namba, hakuna sehemu yoyote utayoomba namba ikawa Comfortable labda iwe penzi la kuunganishiwa.
 
Ndio mana huwa mnapigwa na vitu vizito unawezaje kumtamani mtu kisa dp au umesahau kama tunatumia utambulisho fake humu?
Hapa tunaanza kwa kupenda avatar kwanza
 
Sema hujui kuanzisha mahusiano. Kwahiyo ukikaa naye Mwendokasi ndio unarukia kuomba namba atagawia wangappi? Fikiri mara mbili. Eti binti anapita zake wewe unamwambia naomba namba zako. Akikupa ni malaya huo.

Kama hujui nenda kwa bibi @Faizafox akufundishwe namna ya kutongoza
Wewe huwa unatumia njia gani kumpata mtoto wa kike?
 
kuna jamaa yangu anatabia kama hiyo bas anaenda kwa upole jamaa: dada habari, dada:safi jamaa: kama nakufananisha hv we si ulikuwa unakaa kuleeeee dada:wapi? Jamaa:hapaa kwa kina nani hivi lucy unampata? dada kabla hajajibu jamaa tuache hayo unajua we ni mrembo yaan dah sijui nisemeje ooh hebu nisaidie kwanza namba yako ,, dada:mi nimeolewa namba yangu ya nini? Hadi hapo jamaa uvumilivu unamshindwa jamaa:hivi we mdada mbona unajiona sana cheki ulivyo miguu kama suria kudadek nilikuwa nakujaribu tu utanipeleka wap mtu kama wewe,, kwa aibu dada wa watu huyoo hapo jamaa ndio anazidi siku nyingn ukiniona upite mbali.. Nina hasira sana na ww dada umetangaza vita, na sio kwamba anatania, akimkuta tena kejel tena mara ya tatu ndio anaomba tena kwa woga wa dada anampa na akisha pewa hamtafuti
Bullies…. Tunakuwaga bullied here and there basi tu tunakomaa tutafanyeje?

Mimi kuna kaka chuo alinitaka/aliniomba namba mara ya kwanza tu nilivyofika… mi nikapotezea, alooooh hamna sehemu nimeishi kwa shida kama chuoni, kuna siku aliniambia nitakujaga kukugonga na gari, ukiniona pita hivi 😂😂😂😂 mpaka nikawa nashauriwa nikashitaki, asa mi mkubwa mzima nishitaki shitaki vitu kama hivyo naona jau..
 
kisha nikashusha kioo cha gari na kumuuliza yule dada unaenda wapi? Twende nikusogeze. Akasema poa nikamdrop home then nikampa business card.
YEye ndiye alonitafuta.

ujumbe: tutafute hela, namba haiombwi Anatoa mwenyewe.

(Alisikika mzinzi mmoja)
Na unaweza usitafutwe vile vile… maisha yana levels na hakuna kitu kizuri kama kuijua level yako na kuilenga.
 
Back
Top Bottom