Kuna wanawake ukiwaomba namba ya simu wanamajibu mabaya sana

Hivi kwa sasa kuna mtu anapata shida kabisa kupata namba ya mwanamke? Kati ya kitu rahisi miaka hii kukipata basi ni namba ya mwanamke ila sasa unaweza kuiblock mwenyewe! Mimi sasa hivi nimeacha kabisa mambo ya kuomba namba!
 
Utafikiri unaomba pesa ,akijibu pumba namtukana pia
 
Ndio mana huwa mnapigwa na vitu vizito unawezaje kumtamani mtu kisa dp au umesahau kama tunatumia utambulisho fake humu?
 
Rudia hoja yako kwanza maana naona hata hoja yako uliyoandika huijui maana unajipinga mwenyewe tu hapa

Jifunze kutumka ubongo
 
Hivi kwa sasa kuna mtu anapata shida kabisa kupata namba ya mwanamke? Kati ya kitu rahisi miaka hii kukipata basi ni namba ya mwanamke ila sasa unaweza kuiblock mwenyewe! Mimi sasa hivi nimeacha kabisa mambo ya kuomba namba!
Unreacha mambo ya kuomba namba unafanyaje
 
Ila namba zinaombwa wapi? Unadhani utapata nafasi ya kukutana Kila mahala?

Wewe ndio mshamba na aibu zako ,hata hivyo mbinu ziko nyingi Kwa watu kama.wewe mwenye aibu unanitajia nakariri kichwani.
Anadhani kuna sehemu special kumetengwa watu wanaenda kuombana namba, hakuna sehemu yoyote utayoomba namba ikawa Comfortable labda iwe penzi la kuunganishiwa.
 
Ndio mana huwa mnapigwa na vitu vizito unawezaje kumtamani mtu kisa dp au umesahau kama tunatumia utambulisho fake humu?
Hapa tunaanza kwa kupenda avatar kwanza
 
Wewe huwa unatumia njia gani kumpata mtoto wa kike?
 
Bullies…. Tunakuwaga bullied here and there basi tu tunakomaa tutafanyeje?

Mimi kuna kaka chuo alinitaka/aliniomba namba mara ya kwanza tu nilivyofika… mi nikapotezea, alooooh hamna sehemu nimeishi kwa shida kama chuoni, kuna siku aliniambia nitakujaga kukugonga na gari, ukiniona pita hivi 😂😂😂😂 mpaka nikawa nashauriwa nikashitaki, asa mi mkubwa mzima nishitaki shitaki vitu kama hivyo naona jau..
 
kisha nikashusha kioo cha gari na kumuuliza yule dada unaenda wapi? Twende nikusogeze. Akasema poa nikamdrop home then nikampa business card.
YEye ndiye alonitafuta.

ujumbe: tutafute hela, namba haiombwi Anatoa mwenyewe.

(Alisikika mzinzi mmoja)
Na unaweza usitafutwe vile vile… maisha yana levels na hakuna kitu kizuri kama kuijua level yako na kuilenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…