Ndugu yangu umeandika ujinga mkubwa sana. Inaonekana kichwani mwako kumejaa fikra za udini.
Tangu enzi za uongozi wa Mwinyi, watu wanaiaka Setijali ta Tanganyika. Mpaka ikafika Bunge kupitisha azimio kwa kauli moja kuwa Serikali ya Tanganyika irudishwe. Serikali ikaridhia. Mwalimu Nyerere kwa kutumia kofia ya chama ndiye aliingilia kati na kufanikiwa kubatilisha uamuzi wa Bunge, na kumlaumu Mwinyi kwa nini Serikali imeridhia.
Wakati wa Kikwete, kupitia Tume ya Warioba, watanganyika na wazanzibari, wote walitaka iundwe Serikali ya Tanganyika.
Sasa kama una akili timamu, jiulize kama hao wote waliotaka Serikali ya Tanganyika kama walikuwa wakristo. Na hao wazanzibari waliotaka kuwepo serikali ya Tanganyika, ina maana ni wakristo?
Kwa kweli ukiona mtu anaelekeza mambo kwenye udini, huyo ni mpum.bavu. Watanzania hatuna mambo ya udini, tumeoleana, tuna mahusiano ya karibu, na undugu bila ya kujali dini. Mnaleta hoja za kijinga kuongelea mambo ya udini.
Mwalimu alisema kuwa waliofilisika akili na kisiasa, huwa wanapenda kunificha kwenye udini na ukabila. Wengine tuna akili timamu, huo udini utawaokota wajinga wenzako, siyo wenye akili.