Kuna watu wanapigania mfumo kristo kwa kigezo cha utanganyika tuwakatae

Mimi sikatai hayo yote, yani ni kusema hawakuwa wanapigania Zanzibar ila walikuwa wanapigania dini ndio maana Vita yao ilikuwa dhidi ya makanisa

Hivyo hivyo kwa hawa wanaojificha kwenye kichaka cha utanganyika na kuchoma Mali za waislamu na miundombinu ya Serikali hawa ni magaidi kama wale tu

..Oil Com kachomewa kwasababu inasemekana inamilikiwa na Kikwete, na sio kwasababu ni Muislamu. Hata mabasi ya Ester yamechomwa kwasababu yanadaiwa kumilikiwa na Mwigulu na sio kwasababu ni Mkristo.
 
Hebu nambie TRA, BOT na mahakama kuu ziko wapi? Kati ya bara (Tanganyika) na Zanzibar

..TRA iko Tanganyika na Zanzibar.

..lakini kuna Zanzibar Revenue Board.

..Na sisi tunastahili Tanganyika Revenue Board.

..Pia kuna Jaji Mkuu wa Zanzibar, hakuna Jaji Mkuu wa Tanganyika.

..Kwanini Wazanzibari wanateuliwa ktk nafasi zisizo za muungano?
 
..Oil Com kachomewa kwasababu inasemekana inamilikiwa na Kikwete, na sio kwasababu ni Muislamu. Hata mabasi ya Ester yamechomwa kwasababu yanadaiwa kumilikiwa na Mwigulu na sio kwasababu ni Mkristo.
Kwahiyo ridhwani Kikwete ndio mwenye hati ya muungano?

Ajenda zenu tushazijua pembe za ng'ombe hazifichiki

Wachomaji wa makanisa na miundombinu nyingine wote ni magaidi
 
..TRA iko Tanganyika na Zanzibar.

..lakini kuna Zanzibar Revenue Board.

..Na sisi tunastahili Tanganyika Revenue Board.

..Pia kuna Jaji Mkuu wa Zanzibar, hakuna Jaji Mkuu wa Tanganyika.

..Kwanini Wazanzibari wanateuliwa ktk nafasi zisizo za muungano?
Nyerere alitaka kuifanya Zanzibar kuwa mkoa alishindwa ndio maana ukaona muundo wa muungano haueleweki wewe umeona wapi nchi Ina rais bila jeshi?
 
Mimi sikatai hayo yote, yani ni kusema hawakuwa wanapigania Zanzibar ila walikuwa wanapigania dini ndio maana Vita yao ilikuwa dhidi ya makanisa

Hivyo hivyo kwa hawa wanaojificha kwenye kichaka cha utanganyika na kuchoma Mali za waislamu na miundombinu ya Serikali hawa ni magaidi kama wale tu
Kuna ushahidi wa kusema kilichotokea 29/10 ni jambo la wakatoliki tu?
Waliuwawa wakatoliki pekee?
Waliochomewa mali zao ni wasio wakatoliki tu? Hakuna wakatoliki au wakristo walioibiwa au kuchomewa mali zao?
Bill Nas aliye ibiwa na kuchomewa duka lake ni muislam?
Hakuna waislam walioandamana ile 29/10?
Hakuna waislam waliouwawa zile siku 3?
 
Nyerere alitaka kuifanya Zanzibar kuwa mkoa alishindwa ndio maana ukaona muundo wa muungano haueleweki wewe umeona wapi nchi Ina rais bila jeshi?

..Watanganyika tunastahili kitambulisho cha Mtanganyika, Tanganyika Revenue Board, Jaji Mkuu wa Tanganyika, na kutoingiliwa mambo yetu ya ndani na Wazanzibari.
 
Kuna ushahidi wa kusema kilichotokea 29/10 ni jambo la wakatoliki tu?
Waliuwawa wakatoliki pekee?
Waliochomewa mali zao ni wasio wakatoliki tu? Hakuna wakatoliki au wakristo walioibiwa au kuchomewa mali zao?
Bill Nas aliye ibiwa na kuchomewa duka lake ni muislam?

..hakuna ushahidi wowote ule.

..Muislamu Oil Com kachomewa vituo vyake.

..Mkristo Ester kachomewa mabasi yake.

..sasa Udini uko wapi?
 
HII CHUKI NA HILI JAMBO LINACHOCHEWA NA HAWA JAMAA WENYE ELIMU NDOGO YA THEOLOJIA WANAJIITA TEC N.K

WANASAHAU WAISLAMU WALIPAMBANIA UHURU WA HII NCHI SANA
Yani TEC wana elimu ndogo? Kwa kauli hii sishangai pia na hii ndio akili zenu
1000623418.jpg
 
Kwahiyo ridhwani Kikwete ndio mwenye hati ya muungano?

Ajenda zenu tushazijua pembe za ng'ombe hazifichiki

Wachomaji wa makanisa na miundombinu nyingine wote ni magaidi

..wewe ulidai mali za Waislamu zimechomwa. Mimi nikakwambia mali hizo zilichomwa kwasababu ya siasa sio dini. Na nimekupa na mfano wa mabasi ya Ester ambayo nayo yalichomwa kwasababu ya siasa sio dini.

..sasa usiulize kama Ridhiwani Kikwete ana hati za muungano, huku ukimuacha Mwigulu Nchemba ambaye amekumbwa na mkasa kama wa Ridhiwani.

..Wewe una ajenda ya kuwagawa Watanganyika kidini, lakini nakwambia jambo hilo sio sahihi. Sisi Watanganyika tumechangamano mno kidini mpaka ngazi ya familia. Ukileta mambo ya udini huku Tanganyika tutajua wewe sio mwenzetu, au unafanya kazi ya watu wasio Watanganyika.
 
Wachomaji wa miundombinu wote ni magaidi no matter what! Tumekataa kucheza ngoma isiyotuhusu

Hata kipindi cha uamsho walisema ni siasa

Hata kinachotokea Palestine wanasema ni siasa akili kumkichwa

Siku zote madhara hayana target, hata wale waliovamia Galisa Kenya waliua hadi waislamu wenzao
 
..Ugaidi wakati mwingine huwa ni matokeo na kuzibwa kwa njia halali za kudai haki.

..hata wakina Samora Machel, Robert Mugabe, Sam Nujoma, Nelson Mandela, kuna kipindi waliharibu miundombinu kama sehemu ya jitihada za kudai haki.

..Watanzania tulipaswa kujifunza kwanini wapigania uhuru tuliokuwa tukiwaunga mkono walikuwa wakiharibu miundombinu. Katika kujifunza kwetu tungeweza kuzuia matukio ya wanaodai haki hapa kwetu kuharibu miundombinu.
 
Nimejaribu kukuelewesha na kukufungua macho bado hunielewi

Kunya anye kuku akinya bata kaharisha

Uamsho--magaidi
TEC----Wapigania tanganyika

Matendo yaleyale mbinu tofauti
 
..sijawahi kusema Uamsho ni magaidi.

..waliosema Uamsho ni magaidi na kuwafunga kwa miaka 9 ni Ccm.

..Uamsho walikuwa wakiwaelimisha Wazanzibari kuhusu mapungufu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Basi ukae ukijua ajenda za uamsho na TEC ni sawa utofauti upo kwenye mbinu

Sasa kama uliwaunga mkono uamsho na agenda zao za mahakama ya kadhi na kuondoa mfumo kristo

Ni unafiki kuwaunga mkono TEC maana hizo ni dini kinzani
 
..Uamsho walikuwa Zanzibar hawakuwahi kufika Tanganyika kutoa elimu.

..yuko Sheikh Ponda Mtanganyika aliwahi kushiriki ktk mihadhara ya Uamsho Zanzibar.

..kwani mahakama ya Kadhi haiko Zanzibar? Rais wa Zanzibar si ndiye anayemteua Kadhi Mkuu?

..Yeyote anayeleta hoja ya Uislamu dhidi ya Ukristo ni mgeni hapa Tanganyika, au anatumika na watu wa nje.
 
Sheik Hasan ilunga nae alikuwa wa Zanzibar?

Hizo fikra za kulipwa mnazo nyinyi waeneza propaganda
 
Mleta mada ni mpumbavu. Tumeshawaambia nyie wapumbavu wa Samia. Hiyo ajenda ya udini hatuinunui.
 
Ukitaka niwataje wapambania uhuru asilimia 90 ni Waislam na ndio waliokuwa wakazi wa Dar es salaam kabla hamjaja makafiri

Ninyi pamoja na huyo Baba yenu wa Taifa tumekufunzeni kuanzia kujisitiri kwa kuvaa suruali

Wasomi wa kiislam walikuwepo wengi tu akina Fundikira na kina Mwapachu ila walimwachia nyerere hiyo nafasi
Taja Waswazi wenzako wa mkoa wa Pwani, eti mlifundisha watu kuvaa suruali wakati mlikuwa mnashinda na kanzu za kuchanikachanika. Shule zote za mission na za seminary primary school(ambayo ilikuwa inaenda mpaka standard 4 na middle school ambayo ilianzia standard 5 mpaka 8) walikuwa na somo la kuainzia kuvaa smart mpaka namna ya kufunga tai sasa eti mvaa kanzu na kushindwa peku(enzi hizo) afundishe waliopitia shule hizo namna ya kuvaa, pathetic.
Unakimbilia kutaja wasomi waliokuwa chawa wa Nyerere pale Makerere University, hapo ndiyo umejisibisha kabisa.
 
Usitujumuishe waislamu wote. Waislam tunaamini katika umoja. Hata tukiunganishwa na Kenya na Uganda poa tu, ila sio kutuenfanisha na Zanzibar. Zanzibar na Sisi ni dugu moya.
Uongo huu,
Asilimia kubwa ya Wazanzibari hawautaki muungano tangu siku nyingi. Na hiyo ndio sababu hata rais wao wa zamani Aboud Jumbe alitumbuliwa kinyemela. Je, hao Wazenji sio waislamu?
 
Sheik Hasan ilunga nae alikuwa wa Zanzibar?

Hizo fikra za kulipwa mnazo nyinyi waeneza propaganda

..Ustaadh Ilunga Kapunga badala ya kutetea Waislamu alijikita kushambulia Wakristo.

..badala ya kuichagiza serikali iwainue Waislamu kama raia wake, Ustaadh Kapungu alijielekeza kushambulia Wakristo wakati wote.

..mtu mzima kama yule, na Mtanganyika, alipaswa kutuunganisha badala ya kutugawa.
 
Back
Top Bottom