Kuna yeyote aliyeoa single mother na wakafanikiwa kuishi vizuri tu kwenye ndoa?

Kuna yeyote aliyeoa single mother na wakafanikiwa kuishi vizuri tu kwenye ndoa?

Nimekaribia kuingia kwenye huu mtego aisee, nimepata single mother mzuri kinoma, ananisikiliza kila kitu , ni muislamu yupo tayari kubadili dini na kua mkristo, Yuko smart kichwani yaani naona kabisa huyu naenda kufanya nae maisha, yaani mtoto ni mweupeee waarabu flani wa kasulu huko.

Lakini Kila niliemshirikisha ananiambia nikimbie mbio nyingi nisirudi nyuma, Wala nisijaribu kumuonea huruma, lakini nimefanya research watu wanaongoza kuachana ni hao hao ambao hawakuoa single mother,

Unaweza pata mwanamke bikra na bado mkaachana tu, una uhakika gani huyu mwanamke uliyenaye hajawai kuchoropoa mimba au kutumia P2/ majira kwenye maisha yake?

Kuna wengine wanaingia kwenye usingle mother kwa sababu ya mistake ndogo ndogo 😁😁..

NB, jamaa aliemzalisha anafamilia yake, alitumia advantage ya dogo kwa umaskini wake kumrubuni kupata kazi.

Nioe au nikimbie mbio nyingi sana.
Kama aliyemdhalisha Yuko hai hakuna rangi utakuja aacha kuiona .
 
1. Unampenda kwa mapenzi ya dhati na siyo mihemko tu?

2. Unajua unachokitafuta kwa mke wako mtarajiwa?

3. Huyo singo maza ana angalau robo tatu ya sifa unazozitafuta?

4. Umepata muda wa kukaa naye na kumfahamu vizuri? Na yeye pia amepata muda wa kukufahamu vizuri?

5. Mmekaa pamoja na kuwa na mazungumzo magumu (hard talk) kuhusu ishu ya uhusiano wake na baby daddy wake utakavyokuwa wakati umemuoa? Umemuweka wazi kuhusu kitakachotokea iwapo utapata uthibitisho kwamba amepasha kiporo na huyo mzazi mwenzie? Ana maoni na mtazamo gani kuhusu jambo hili ambalo ni kama single mothers wote wanatuhumiwa?

6. Kama huyo mtoto wake mtakaa naye, mmeongea kuhusu malezi yake; na ushiriki wa baby daddy utakavyokuwa?

Haya maswali yanatosha kwa kuanzia na kama majibu yako hapa ni chanya na unaamini kuwa umepata mke mwema basi oa tu usiogope. Kuna single mothers wengi ambao wanajitambua na wanajua makosa waliyofanya; na wameshaapa kutoyarudia tena. Na hawa huwa ni wake bora sana na wasiotetereka. Kuna mifano mingi naifahamu.

Sikiliza moyo wako. Msikilize Mungu wako. Halafu fanya maamuzi sahihi. You may end up with the best woman of your dreams kuliko hata waliooa mabikra!
 
Single maza ni mwanamke mjinga sana:

●KWANZA, alikubali kutiwa mimba na mwanaume ambaye sio mume wake

●PILI, ujinga mwingine wa single maza ni kumchagua irresponsible man (mwanaume ambaye hayuko tayari kutimiza majukumu yake) amtie mimba

Mwanamke mjinga kama huyu kweli uumfanye mke?

You will learn the hard way
 
Unafikiri kuzaa au kutokuzaa kabla ya ndoa ina guarantee lifetime ya ndoa yako? Wengi wameoa single mothers na wameishi, wengine wameoa mabinti wenye hawana watoto ila ndoa chali baada ya mwaka tu...sisemi single maza hawana shida wala ndoa hazivunjiki, hapana!
Issue sio kuishi issue mnaishi vipi hapo ndio ugumu wa kuoa single mother ulipo
 
Singo maza hapana sio wa kuoa mkuu, we jichanganye unaanza kumtetea kwasbb ya hisia za ngono......na jingine sio rahisi muislamu kubadili Dini ni swala la mda tu.tena kama baba mtoto alikua muislamu mwenzie hapo utalia kabisa utasikia wewe unaolewa je na kafiri, rudi nikupe chochote unacho taka kwa ajiri ya Allah ila uachane na kifiri, huyo ili uwepuke moto wa jihanamu na laana.
Hapo kinachofanyika ni hiki,huyo singo madha ndio anahitaji ndoa na sio wewe,yaani siri ya kuhitaji kitu ipo hivi,kkama mvuvi anavyohitaji samaki,basi mvuvi anapaswa kujua samaki nahitaji nini,na jibu ni kwamba samaki anahitaji chambo,hivyo unapaswa uweke chambo kwenye ndoano ili samaki aje kirahisi.Na ndio huyo singo madha anachofanya yeye anahitaji ndoa,ameshajuwa ndoa inahitaji utiifu usikivu akili upole hivyo amekuektia vyote hivyo ili uingie kwenye mtego ili upate wazo la kumuoa,akishaipata ndoa tuu,utaziona rangi zake halisi.
 
Kuna mwamba mmoja alikua anaongea hivi yani nilichekaaa "eti mwanaume atakaejifanya kuoa mwanamke niliezaa nae, nakua naenda kumuona mwanangu asubuhi, mchana na usiku" 🤣🤣🤣🤣🤣
Jamaa hajielewi, sasa siangemuoa..,kama ni mm ndio niliyemuoa huyu single mother na nishajua nia ya jamaa mbona ataisoma.
 
Back
Top Bottom