Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Kwenye kupenda huwa hatutumii akili bali tunatumia roho.Nimekaribia kuingia kwenye huu mtego aisee, nimepata single mother mzuri kinoma, ananisikiliza kila kitu , ni muislamu yupo tayari kubadili dini na kua mkristo, Yuko smart kichwani yaani naona kabisa huyu naenda kufanya nae maisha, yaani mtoto ni mweupeee waarabu flani wa kasulu huko.
Lakini Kila niliemshirikisha ananiambia nikimbie mbio nyingi nisirudi nyuma, Wala nisijaribu kumuonea huruma, lakini nimefanya research watu wanaongoza kuachana ni hao hao ambao hawakuoa single mother,
Unaweza pata mwanamke bikra na bado mkaachana tu, una uhakika gani huyu mwanamke uliyenaye hajawai kuchoropoa mimba au kutumia P2/ majira kwenye maisha yake?
Kuna wengine wanaingia kwenye usingle mother kwa sababu ya mistake ndogo ndogo 😁😁..
NB, jamaa aliemzalisha anafamilia yake, alitumia advantage ya dogo kwa umaskini wake kumrubuni kupata kazi.
Nioe au nikimbie mbio nyingi sana.
Roho inaishinda akili kwa maamuzi ikiwa imependa.
Hata tukwambie ukweli kuwa huyo hakufai utatusikiliza?
Ni bahati mbaya sana vijana wetu wa sasa mnabebwa na mitandao na ukisasa, sisi hatuwawezi!
Wewe huyo mchumba wako katika kuonesha nia yake ya kuolewa ulitarajia akuoneshe makucha yake halisi?
Hakuna mwanamke aliyetulia akazalia nyumbani.
Na mwanamke huwa anabembeleza ndoa na kujionesha utulivu na upole ili kulinda haki zake, yaani ukiisha muoa tu, anajiachia kwa tabia zake halisi hilo ulielewe.
Na muungano wa kiroho kwa ajili ya mtoto kati yake na mzazi mwenza huwa haufi na hilo jambo akishatulizana kwenye ndoa, wewe litakunyima sana usingizi.
Sijataka kumwagika sana kwenye uchambuzi wangu, itoshe kusema tu kuwa, kama haujawahi kuoa katika maisha yako, si vizuri kuyaanza maisha yako ya kwanza kwa ndoa na mwanamke aliyekwisha kuzaa na mwanamme mwingine.