Kunena kwa lugha ni nini? Na nini hutokea pale mtu anaponena kwa lugha?

Siamini katika kunena kwa lugha, maana huwezi kuzungumza kitu ambacho huwezi kutafsiri, mitume wakati wanaenda kusambaza injili walipewa karama ya kuzungumza lugha ya wakazi wa eneo husika na sio lugha ambayo kwa sasa si wewe wala mkazi wa eneo husika anaejua

Hivi ni lugha gani ambayo ina maneno yasozidi hata 10 as a matter of fact, nahisi matano tu mengi ni mwendo wa RABASHABAKA. . .

Ikiwa yapo maneno mengine mtanifuta nipo paaale mniite jina lolote maadam limpendezalo Mungu

Nashukuru imani yangu haina hayo masuala, wala kuabudu masanamu, wala kuambiwa baadae ntapewa 70 ilhali huyu mmoja ananitosha, wala kusujudia miungu watu kwa gia ya maji na mafuta

Mi ni Dua kwa Mungu mmoja kupitia kwa mkombozi wetu Masihi, kushika siku saba ya Juma, kusambaza upendo na kupiga vita chuki na kuyashika yote niliyoamriwa.
 
Kunena kwa lugha ni lugha ya kiroho ambayo huja automatic na hakuna awezaye kuimiliki...

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilihisi Mshana Jr atakuwa mbobezi kwenye hili kumbe, hakuna anayejua yote! Kasome biblia yako vzr kunena kwa lugha inaanzia kushuka kwa roho siku ya pentekoste na inaonyesha bayana ya kuwa waliokuwa wananena walinena kwa lugha za kibinadamu ambazo wao walikuwa hawazijui kabla, mfano msukuma aaze kuongea kiitaliano ambacho hakuwa kujifunza mwanzo huku akitaja ukuu wa Mungu! Na. Mfaransa aanze kuongea kiangaza, kisha muangaza ashangae mbona anaongea maneno ya ukuu wa Mungu kwa lugha yake??? Swali zile robo shaka shaka ni lugha gan? Kule ni kupuyanga tuh hakuna roho wa hivyo
Ref :matendo ya mitume 2:1-13
 
Umenena vyema !👏🏾
 
Matapeli wana lugha zisizotafsirika kwenye kamusi yoyote ile ... Wakimaliza kunena lugha zao utasikia shika sadaka yako.. Na wanakondoo wanajipuputisha walivyo navyo wakirudi nyumbani ni kwenda kununua mafuta ya mia mbili na kupika ugali dagaa wa free (mchana hadi jioni) huku wamenyanyua mikono ya nabii kwa 50k ..
 
Unaweza ukawa na elimu,pesa na bado ukawa kichaa,We unavyowaona walokole wako sawa.
Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.
2 Kor 5:13 SUV
 
Ndio wote ni vichaa unakuta mtu kapaza sauti anaongea lugha hata ukimuuliza ume maanisha nini hajui,Huo ni ukichaa bin wendawazimu.
Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.
2 Kor 5:13 SUV
 
Sawa mkuu
 
Kunena kwa lugha ni tendo la kiroho lisilo na tafsiri yoyoye iwayo yote katika ulimwengu! Ni tendo la ndani mno na haliji kwa siku moja wala kwa kupanga
Kadiri unavyokuwa na usafi wa kiroho.. Uchaji wa kiimani na usadifu wa maombi kuna viwango vya kiroho na kiimani unajiona kabisa unapanda..

Na pindi unapoingia kwenye maombi kuna hali fulani hivi hukuvaa na kujikuta unahama kutoka ulimwengu huu na kuingia ulimwengu mwingine mwepesi na mng'avu sana.. Hapo ndio kuna maneno hukutoka bila utashi wako na bila kujua unaongea nini.. Lakini unakuwa na hakika MOJA tu si maneno ya kujitungia wala ya kidunia ni maneno yenye lugha yenye uhai na una i feel kabisa..

Nilishaishi katika wokovu kwahiyo ninalifahamu hili kwa hakika[emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna lolote ni usanii tu..rakashobayatattaaaaa yayyyy
 
Umrsahau mito inayotiririka Konyagi,Amarura ,Safari,Balimi, Kimpimu na Wanzuki!
 

Kunena kwa Lugha au Glossolalia let me talk on 3 persepectives...

Kisayansi/Afya..

Kunena kwa lugha au Glossolalia kisayansi inakuwa associated na Magonjwa ya Afya ya Akili kama Schizophrenia ,Bipolar na mania...

Kwa sababu Mtu yoyote anayejiona kama anaongea na mtu Mwingine ambaye hamuoni na anaona kama anamuona huku akimwambia vitu visivyoeleweka yeye akiamini Vinaeleweka hiyo 2⁰ Mania au bipolar na huenda ikawa schizophrenia kabisa kwa Visual na mind halucination..

Na haipingiki ukija kwangu unanena kwa lugha nakuchoma Haloperidol za kutosha ili urudi sawa...

Kibiblia na kidini
Haipingiki kwamba Kunena kwa lugha ni karama ya roho ila yenye utaratibu wake katika kuifanya Uataratibu huo umewekwa kwenye 1 wakorintho 14..

Paulo anasema kuwa ziko sauti Nyingi duniani na zote zina maana... 1 Wakorintho 14:10


Na utaratibu aliuweka mzuri kwamba ukitaka kunena kwa lugha basi Wanene wachache na wengine watafasiri kinenwacho.. 1 Wakorintho 14:27-28


Wanachokifanya walokole Ndo kitu Paulo Amekiita kama Wazimu kwenye 1Wakorintho 14 :23-25
na anasisitiza Bora kutoa Hotuba ila sio Kuzungumza lugha isiyoeleweka...
Ieleweke kwamba neno Lililotumika hapo kama wajinga ni


Sasa najua unaweza ukaja ukasema neno kuhusu Wajinga wanapoingia...
Sasa hii ni tafsiri kwa lugha ya Kingereza...



Na pia unaweza ukaona katika Lugha ya Kigreek fungu hilo ni...

"Εἰ οὖν συνέλθῃ ἡ ἐκκλησία ὅλη ἐπὶ τὸ αὐτὸ καὶ πάντες γλώσσαις λαλήσουσιν, εἰσέλθωσιν δὲ ἰδιῶται ἢ ἄπιστοι, οὐκ ἐροῦσιν ὅτι μαίνεσθε; εἰ δὲ πάντες προφητεύουσιν, εἰσέλθῃ δέ τις ἄπιστος ἢ ἰδιώτης, ἐλέγχεται ὑπὸ πάντων, ἀνακρίνεται ὑπὸ πάντων, τὰ κρυπτὰ τῆς καρδίας αὐτοῦ φανερά γίνεται, καὶ οὕτως πεσὼν ἐπὶ τὸ πρόσωπον αὐτοῦ προσκυνήσει τὸν Θεὸν, ἐξαγγέλλων ὅτι ὄντως ὁ Θεὸς ἐν ὑμῖν ἐστιν"

sasa neno " ἰδιώτης" ambalo Kiswahili wametafsiri kama Mjinga lina maana ya Mtu asiyejua,layman ama Mtu kutoka Sehemu nyingine au outsid...

My take kuhusu Kunena kwa lugha kwenye biblia naconclude kama Paulo alivyoconclude tu kwenye hilo 1 Wakorintho 14:36



Na PERSPECTIVE YA MWISHO NI WALE WAFATA MKUMBO..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…