Kungekuwa na sumu ya kujidunga kisha unakufa usingizini wengi tungeshatoweka duniani

Kuna kipindi nilitaka kujitupa kwenye maji nife mitaa ya seaview, hapo nakaa kwenye apartment kali uko seaview

Ukinicheck unaweza kusema jamaa kayapatia, ila nikukupa matatizo yangu unapasuka kichwa hapo hapo kwa kuwaza

Ila mungu mkubwa nilishinda mtihani wa kutaka kujitupa kwenye maji .kwenye korongo baharini
 
Hapo pa kwanini ulizaliwa pawe fundisho kwetu tunaohamasisha kuzaa watoto wengi....baadae tunaishia kuwatesa kama ivi
 
Mtu ana bando na kuscroll jf anawaza kujiua 😁😁😁😁.
Kila nikiona mirinda nyeusi hayo mawazo huwa yanapotea ghafla.
 
Shida sio kutafuta pesa.BALI HIZO NJIA ZA KUTAFUTA PESA[emoji1787][emoji1787][emoji1787].
yaani tunapeana tu moyo tafuta pesa.
Ila kiukweli njia z kutafuta pesa ni ngumu.huna kazi,Huna mtaji ,Huna kibarua,Huna connection. Hizo hela unatafuta vipi?
Hiyo ni changamoto nyingine, ni muhimu sana kwa kijana kuishi kwa kuangalia fursa. Ukiwa mtu wa kuangalia fursa utazungukwa na kuwa karibu na watu watakaokusaidia kuzipata fursa.

Pia ni muhimu zaidi vijana kukubali kufanya kazi yoyote halali ili kujipatia kipato. Ajira hakuna lakini kazi zipo, ni muhimu sana kwa kijana 'kujichanganya' na watu sahihi.
 
KTioa

Mimi ni kijana ambae sichagui kazi pamoja na kwamba nimesoma na sina ajira kwasasa.Nishawahi hadi kusaidia mafundi ujenzi kwa kubeba tofali na kufanya kazi ambazo kwa vijana wa sasa wanaomaliza vyuo huwezi kuwashauri wafanye, yote ni kwasababu nina majukum hivyo sipaswi kuchagua kazi ilimradi tu iwe halali.
 
Book: Feeling Is the Secret
Author: Neville Goddard

Hakika ukisoma hichi kitabu na ukayatekeleza yale yalioandika hakika utaweka historia mpya katika maisha yako... Maarifa ndio kila kitu katika hii dunia
 
Dah! [emoji848]
 
Hata hao matajiri wana stress za madeni,kodi, mikopo nk. Mtu anatembelea V8 lakini anakunywa dawa za pressure,sukari na usingizi everyday ili aweze kuendelea kubaki hai. Kikombe unacho kinywea muombe Mungu tu kisiwe kichungu au chamoto kupitiliza .
 
Daah!! Pole sana Mkuu! Sina cha kuongea hapo! Mungu asikie hitaji la Moyo wako
 
Aliyesema life begins at 40 alitudanganya[emoji1][emoji1][emoji1]
Hajadanganya, vile tu haujamwelewa! Life begins at forty haina maana ya kuwa uanze kutafuta maisha ukiwa na miaka 40, hiyo miaka ni kuanza kuishi kwa kulingana na ulichokiwekeza au kukitafuta kwa miaka 39 nyuma!
 
Tukuchangie pesa Kwa namba ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…