Heaven Sent
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 32,682
- 98,253
Couldn't have said it better. ThanksKuna kisa kimoja kinawahusu wanaume 40 wenye matatizo mazito ambao walienda kuombewa na kiongozi wa dini. Kiongozi wa dini akafanya dua/maombi akatokea malaika. Basi huyo malaika akawaambia wale watu kila mmoja aandike matatizo yake yote Yale anayo amini ndio matatizo makubwa kuliko yote. Ayaandike kwenye karatasi kisha aifunge ile karatasi halafu juu yake aandike namba ya siri. Baada ya hilo zoezi kufanyika malaika akawaambia haya sasa kila mmoja aweke karatasi yake kwenye ndoo . Wote wakaweka karatasi zao kwenye ndoo. Baada ya dakika ishirini akawaambia haya sasa chukueni hayo makaratasi yenu lakini hakikisha unachukua karatasi ambalo sio lako yani ambalo hujaliandikia password.
Zoezi likafanyika. Baada ya zoezi kufanyika yule malaika akawaambia kila mmoja asome kwa makini kilicho andikwa kwenye karatasi aliyo iokota ( maana yake ni kwamba asome matatizo ya mtu mwingine) Zoezi likafanyika.
Baada ya zoezi kufanyika yule malaika akawaambia sasa ninawapa dakika tano mfanye maamuzi kila mmoja wenu. Kwamba ubadilishane matatizo na huyo mtu ambae unasoma matatizo yake kwenye karatasi yake uliyo iokota kwamba matatizo yake yawe yako na yako yawe yake. Unaambiwa ukumbi mzima zilitokea ngumi kila mmoja anataka arejeshewe karatasi yake ili abaki na matatizo yake kuliko kubeba matatizo ya mwingine. Kila mmoja alijiona kumbe ana afadhali kubwa sana kwenye maisha.
Amini kwamba matatizo uliyo nayo ni afadhali kuliko matatizo ya mtu mwingine.
Matatizo mengi huwaga yapo kwenye mindset n.a. sio kwenye uhalisia. So don't bother to fix the problem but just fix the way you think and the problem will fix itself.
Wewe ni mkristo kuwa kama ilivyo shauriwa kwenye bible kwamba you should be a prisoner of hope..
Binafsi nimefikia kwenye realization kwamba things are not happening to us but they are happening for us
Ushauri wa ziada; watu wenye hekima na busara wanasema hakuna njia nzuri ya kukabiliana na matatizo kama to reduce ur problems in to songs. Whenever you face a problem just reduce it into a song and ur mind will release out the problem.
Wazulu walitumia technic hii during apartheid and it worked for them.
You can try it out.
May the peace of the Lord be upon you