Kununua ardhi halafu huna pesa ya kujenga ni ujinga, Bora hiyo hela ufanyie biashara

Oya mpe muda narudia mpe muda utakuja kumuelewa baadae ramani haijakaa sawa tu ila mpe muda atajenga
 
Sio kila mtu ni mfanyabiashara Mkuu.

Asilimia 90% ya sisi watanzania sio wafanyabiashara
Jamaa Yuko sahihi.
Nikuambie tuu nusu ya nyumba unazoziona mjini na Tanzania zimejengwa kwa mfumo anaoutumia jamaa.

Na nusu ya wazee na watu wazima wasio na nyumba walikuwa na mawazo kama yako.
 
ukinunua ardhi pale mbweni leo Milioni 100 ikakaa tu pale, kitu tofauti na mwenye milioni 100 leo akaingiza sokoni kwa muda wa miaka 5
 
ukinunua ardhi pale mbweni leo Milioni 100 ikakaa tu pale, kitu tofauti na mwenye milioni 100 leo akaingiza sokoni kwa muda wa miaka 5
Wapo walionunua chini ya hapo na wanauza hizo bei baada ya miaka mitano..
Ardhi imewatoa sana watu wenye mitaji mikubwa Arusha yapo maeneo wanauza kwa usd 200,000 kwa heka moja na walichukua ile ardhi kwa shilingi tena hela ya kawaida tu..
 
Good point, umenyooka kabisa mkuu
 
Huyo kadanganywa na hawa wazee wanaojuta kutokununua ardhi enzi za zamani, Pesa unayotegemea ipande kwa miake yote hio unaweza kuipata hata kwenye Biashara na zaidi ukapata mahitaji ya kila siku huku unatengeneza profit kuliko kuiweka yote ardhini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…