Kuoa Kumbe Siku Hizi ni Upumbavu Kabisa

Mti wenye matunda ndio unapigwa mawe, ndoa ni kitu chema sana kwa hakika, adui wa ndoa ndiyo walewale adui wa mema mengine yote ya duniani hii hata na mbingu pia, kimsingi ni adui wa Mwenyez Mungu na yale yote yanayompendeza, kwa vile ndoa ni moja ya mema hayo, kizazi hiki kilichooza hakitegemewi kuikubali wala kuipenda kama vile kisivyoyakubali Wala kuyapenda mema mengine yote. Ni kizazi kiovu, hivyo maovu na waovu ndivyo vinavyopendwa, kusifiwa na kushangiliwa, mambo mema na matakatifu yanatukanwa, yanadhihakiwa, yanadharauliwa na kukejeliwa hata kutiwa kufuru, Mungu wa mbinguni akisaidie kizazi hiki chetu, kinachoangamia kwa kukosa maarifa. Mimi na nyumba yangu (ndoa yangu) tutamtumikia Bwana, nyinyi wengine chagueni hii leo, ni nani mtakayemtumikia ktk kipindi hichi kifupi Cha maisha yenu hapa duniani....Nawatakieni jpili njema.
 
Sawa mchungaji
 
Mimi napenda harusi tu
Kuna mwamba kaoa uchagani, kumbe mama mkwe na binti yake wanataka zawadi za send off tu. Ndoa imedumu miezi miwili, mwanamke karudi kwa mama yake, hoja eti mme wake mwizi, kaiba power bank.

Kwenye sendoff zawadi zilizotoka si chini ya mil 40,000,000/- na mwanamke hakusafiri nazo kwa mme, baada ya kuvunja ndoa ndo amegeuza mtaji.

Kuoa mchaga napo jipange
 
Pole sana ila m nahisi uliishi kwa kukariri jama yangu chukua hii mwanamke huwa haonyeshwi pesa isipokuwa anaonyeshwa pesa ya matumizi we kam uliishi nae kwa kumuonyesha kila kiwango Cha pesa ulichokuwa unakipata kazini hilo ndilo kosa lako jitahidi usizoee kumuonyesha kiwango Cha pesa unachokiingza hata kma unapokea mshahara Kama unapokea 700k jitahidi mwambie unapokea 3.5k maana huwa wanaasili ya kujiongezea matumizii pia ucpende kuacha kiwango maalumu Cha pesa mezaniii zngatia nyoka hafungwi akiwa na meno
 
Haya yote nitoka vitabu walivyotuletea. ..before that mababu zetu walisemaje?..mwenye ufahamu kwenye historia atusaidie...
 
Kuna ndoa zingine za kijinga tu, ebu fikiria mwanamke unakubali kuolewa na mtu kama Haji Manara ili akutangaze kwenye mitandao ya kijamii na kupata kick. Atakuonyesha sinema za ngono na kuiga kila machafuko yote yaliyoko humo alafu anaenda kuwaambia washikaji zake kila mnayoyafanya.....utaweza ishi na mwanamme kama huyu kweli?
 
Shida mnaoa mashangingi ya baa
Mmekutana usiku baada ya wiki unaoa .

Nawatangazia vijana wote kuwa ndoa ni kwa wenye akili zao sio nyie na ujinga na upumbavu wenu wa Simba na Yanga

Ila mkikaidi mkao hivyo hivyo uzee kwenu kitakuwa kitendawili kigumu maana tutawazika mkiwa na nguvu zenu .

Jumapili njema vijana rudini kwa baba zenu wawaambie wao walioaje na waliangalia nini .

.
 
Haya yote nitoka vitabu walivyotuletea. ..before that mababu zetu walisemaje?..mwenye ufahamu kwenye historia atusaidie...

Usilinganishe babu zetu na hawa wavulana wa siku hizi
Babu zetu wenyewe walikua wanaume wa shoka, marijali waliooa hadi wake 2, 3 tena wakiwa na uchumi mzuri
 
Usilinganishe babu zetu na hawa wavulana wa siku hizi
Babu zetu wenyewe walikua wanaume wa shoka, marijali waliooa hadi wake 2, 3 tena wakiwa na uchumi mzuri
Hili nalitambua but nia yangu nikupata mtiririko km uliandika wazee wetu before mkoloni aliishije/aliwaasia nn vizazi vijavyo..
Natambua walikua nanguvu nauchumi imara pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…