Kuoa Kumbe Siku Hizi ni Upumbavu Kabisa

Haya yanatokea siku hizi sababu baadhi ya wanaume wamejipa forum ya kuyazungumza. Hivi mnafikiri wanawake wa zamani wakiwemo mama zetu walikuwa tofauti sana na waliopo sasa. Tofauti ya Sasa ni kuwa wanaume wa leo sisi ni wepesi wa kukimbia. Wanaume wa kitambo walikuwa wanakufa na tai shingoni.
 
Hivi uoe mtu kama Aunt Ezekiel, Kajala, Lulu Diva, na mademu wengine uchawi wa bongo movie unategemea nini sasa?
 
Kumbe ujanja kwako ni kuolewa au? Unapilamamikia kutoa ina maana unataka ukae upande wa kupokea... na huko ni kwa mke... hebu fikiria vizuri mjomba. Hayo ni mawazo hatarishi.
 
Zamani pesa haikuwa ina dhamana kama leo mkuu, silaha ni pesa mjini saivi.

Mambo siku hizi ni mengi, anasa na starehe zimezidi, demu unamlisha vizuri kila siku sasa ukija kumpa ugali dagaa na tembele mara 2 mara 3 umemkimbiza mazima.

Kwa hiyo pesa bhna ni hatari.
 
Usilinganishe babu zetu na hawa wavulana wa siku hizi
Babu zetu wenyewe walikua wanaume wa shoka, marijali waliooa hadi wake 2, 3 tena wakiwa na uchumi mzuri
Kumbuka na leo hii wapo wanao jituma lakini wapi wanatemwa au kuuliwa na wake zao. Watu wamejitosheleza nyumba na magari plus mali za kutosha.
 
Single Maza ni sawa na sumu isiyo na expired date.....SASA shauri yako........maana hiyo haifai hata Kwa matumizi ya kujiua..........utakuwa kufa ufi lakini upo Kati Kati........kama unaamka au unakufa
daa! wabongo.hivi tungekuwa tunaongea kiingereza tu huu udambwi udambwi tungeupata?
 
Uzi wako uko vyema sana. Ni kweli kwamba sasa hivi kujenga familia iliyo bora ni ngumu sana kutokana na sababu mbali mbali ambazo shetani anazidi kuzi- implement miongoni mwa watu na hasa jinsia KE.

Kwa wakati tulio nao nashauri tu kwa wale wanaotaka kuona, ukishapata mwenza bora umfanyie interview, akifaulu lipa mahari, chukua watu wawili au watatu kafunge ndoa kutokana na imani yako. Hakuna haja ya vikao sijui kadi kibao za michango na vikao. Sherehe kubwa. Haina haja kabisa. Mwisho wa siku hakuna amani ndani ya nyumba kila mtu analala chumba chake.

Sasa hapo hata mkiachana hakuna hasara.



Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…