Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

Inasikitisha sana aisee.

Kama kijana aliaga kwao anakuja mjini kutafuta maisha ndugu watabakia na dhana kwamba bado anatafuta kumbe alishakufa na kuzikwa kitambo. ☹️
 
Shida ninazo nyingi sana, hilo halifichiki.

Namuomba Mungu anisaidie katika kunitatulia shida zangu. Amen.
 

Hizo jeneza si ajabu zimeenda pigwa bei mbele ya safari...

Hao maiti wakazikwa na sanda tu...
 
Watu hawana huruma, wanakupigiaje honi katika mazingira hayo, ningekuwa mimi nisingemsikiliza na honi yake
Nilikuwa getini. Alikuwa sahihi kutaka apite ili nimpishe.

Huenda alikuwa daktari anawahi kuwahudumia wagonjwa.

Haikuwa sahihi kuleta foleni kwa Mshangao wangu kwa kinachofanyika.
 
Mimi nikifa hata wanitupe porini niliwe na fisi sijali. Hata nizikwe kwenye jeneza la bilioni moja na mbwembwe za kila aina sijali. I am dead. Sihisi cho chote. Sipo!

Zingine zote hizi ni mbwembwe tu za binadamu za kupotezeana muda na resources...

Sasa hata misiba imekuwa ni sehemu ya kuonyeshea jeuri ya pesa. Mijeneza ya bei mbaya, sare, maua na aina ya viongozi wa dini na kisiasa watakaohudhuria...Huwa nawaonea wivu sana Waislamu. Unakata moto saa tatu asubuhi ukizubaa by saa nane mchana tayari ushazikwa...hakuna cha mbwembwe wala nini!

Haya dunia nzima ilikusanyika Afrika Kusini kumzika Mandela. Mbwembwe zote zile zilimsaidia nini Mandela?

Rubbish!
 
Naam kwake yeye haimuumizi. Kwako je?

Utajisikiaje kuuona mwili wa mzazi wako au mwanao unaenda kufukiwa bila ya utaratibu wowote? Be honest, how would you feel? Kama utaona ni sawa, Muombe Mungu akusaidie kwa sababu huruma imeondoka ndani yako. Mwili wa nduguyo ni sawa na mwili wa binadamu wowote. Usione huruma kwa nduguzo tu.
 
Mkuu,

Kwa maiti ni sawa. Hakuna shida, aibu na maumivu haipo tena kwake. Wewe kama wewe unajisikiaje? Huhisi maumivu?

Mama yako kwenda kutupwa namna hiyo utaona ni sawa kwa sababu ameshafariki? Upo tayari mwili wa mwanao mpendwa ukatupwe jalalani fisi washambulie? Upite kwa bahati mbaya ukute mkono au kichwa chake?

Kila mtu ana namna yake ya kuona. Na naheshimu hilo sana.
 
Hapo tatizo ni ufahamu.

Maamuzi ya kibinadam sio sahihi. Walipaswa kumzika vema Mungu ataamua
 
Huyu mtoa mada sio aina ya watu ambao hutoa mediator. Mediator sharti awe na roho inayohimili kuona magumu na kufanya maamuzi sahihi yasiyochangiwa na huruma zisizo za msingi.

Unaenda mediate unaonyeshwa miili ya watu 30 waliokufa unalazimisha basi tu Iddi Amin aichukue sehemu ya Kagera ili vita iishe unakuwa mjinga. Mediator anazingatia akisimamisha vita wakati usawa hamna anatengeneza chuki itakayodumu na upande wa Tanzania ambayo baadae watataka kurejesha eneo lao kwa vita itakayoua watu zaidi. Its not over until it's over.

Sasa hao wasio na ndugu wakae humo mortuary kujaza nafasi. Bila kuzikwa na manispaa hakuna option nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…