Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

Niko na wewe katika hili. Mimi nina wosia kabisa. Nitakakofia nizikwe huko huko kwa namna yo yote ile isiyoleta hasara na kupoteza muda kwa waliobaki. Na sitaki mbwembwe za aina yo yote maana nyingi ni unafiki wa binadamu tu.

Ni wajibu wangu kunyosha njia na mapito yangu nikiwa hai na kwa Neema ya Mungu naamini nitakwenda mbinguni baada ya kifo.

Mengine yote haya ni upuuzi tu!
 
Naomba kufahamishwa hii source 1 na source 2 ni aina gani ya mtindo mpya mjini hapa
Watumiaji wa app ya zamani tunalazimishwa tumia app mpya ambayo inatutaka kubonyeza next kusoma story
 
nachoamini mm ni bora kuwasaidia walio hai cos hakuna ibada wala baraka kwa kuwatendea mema waliotangulia,Najua hawakufanya kwa uwazi ila we uliona baada ya kupata view flan..
Mkuu sikufanya ili kupata baraka. Nilifanya ili nafsi yangu ipate amani. Si kwa nia nyingine yeyote.

Kuzika waliotutangulia ni ibada. Kwa waislamu ni faradhi.

Kwetu sisi Wakristo ni matendo ya huruma.
Mwisho;Ndugu tuwe responsible na miili ya marehemu wetu
Naam. Hili haswa ndilo linalopaswa kuwa. Lakini kama taarifa hawana, serikali iwasitiri katika namna ya faragha. Si kwa namna ile. Waheshimiwe walau kidogo.
 
Mwananyamala hospital hata kama hukupenda kuweka wazi jina la hospital husika... Je nimepatia?

Kwa bahati mbaya Serikali haina muda wa kufanya utambuzi wa DNA ili walau waondolewe kwenye kundi la waliopotea wasitafutwe zaidi na ndugu zao.
Ili DNA iwe sahihi yahitajika ndugu wa Marehemu pia ili waeze fanya cross match.

Tofauti na hapo ni Serikali ichukue DNA za watu wote kwa njia ambazo ni za kificho, waweke kwenye database ili wawe wanafanya crossmatch
 

Haina maana yoyote hata usipofanya. Yaani hakuna unachoongeza wala unachopunguza. Na ndio hapo tunasema workdone si equal to Zero.

Ila Kama unafanya Kwa Amani ya Moyo wako sio tatizo.
Hiyo inaitwa Imani ya umizimu.
 
Tatizo la Tanzania ni huduma mbovu.
Ukute wamesubiri wameona wawatoe kwwenye majokofu
 
Inakuaje mtu kukosa ndugu serikali ijiangalie kwa hilo. Ni mauzembe tu. Science ilisha advance ila sisi bado tupo nyuma. Lililokubwa hapa ni ndugu za maiti wawe na taarifa kwamba jamaa yao kashaondoka ulimwenguni ili wasibaki njia panda.
We jichanganye uone kama utazikwa na ndugu
 
Pole sana, ukute hayo majeneza yarirudishwa sokoni
 
Serikali imechelewa kidogo.

Inapaswa kuwa na database ya DNA ya wananchi wake wote. Kuanzia wanaozaliwa mpaka utu uzimani.

Hii itasaidia sana katika utambuzi na usalama wa raia wake. Hata pia katika swala zima la usalama.
DNA hadi Mahakama iruhusu, pia DNA inaweza tumika vibaya kwa kupunguza aina fulani ya watu.
 
Hapo mwisho umeandika uongo yani wasifukie.. Hv unajua mwili wa kiumbe chochote kilichokufa ni chanzo cha magonjwa mengi
 
Huyo jamaa ana matatizo ya akili hautawezana nae... Kuna kipindi alisema Marekani ndio walioumba hii dunia eti 😅😅
 
Katika mada kama hizi ni sehemu sahihi ya kufikisha uhalisia wa maisha yetu kwa maana kifo hakie epukiki kwa yeyote yule hata awe na cheo na mali kiasi gani

Mwenye kuamini uwepo wa mungu na mwenye kuto amini wote wote tutakufa .hili lipo wazi hakuna aliewai kupinga hili

Cha muhimu unakufaje na una acha athari gani katika jamiii inayokuzunguka.??

Napenda kutoa somo lifuatalo watakao amini sawa na wasio amini pia Allah atawafanyia wepesi watumie akili zao vizur ili kuliendea `

PINDI ANAPOKUFA MWANA ADAMU NA AMALI ZAKE ZOTE ZINAKATIKA ISPOKUWA MAMBO MATATU TU.NA MAMBO YENYEWE NI HAYA YAFUATAYO

1.SADAKA YENYE KUENDELEA ,hii inamaana wakati wa uhai wako labda ulichimba kisima kikawa manufaa kwa jamii yote ,hata kama ukitangulia kufa bado manufaa ya thawabu unayapata huko huko kaburini,labda ulijenga hospital watu wakawa wanatibiwa ,ulitoa vifaa hospital vikadumu kwa muda mrefu,ulijenga msikiti,madrasa,ulijenga vituo vya mayatima

2.ELIMU YENYE MANUFAA KWA WATU
Uliwafundisha watu elimu ikawanufaisha na jamii ikaelimika kwa ufanisi uliokuwa mkubwa,kwa mfano uliwafundisha watu kumjua Allah ,na mitume yake
Ulifundisha watu uadilifu,na haki na wakazifuata.

3.MTOTO MWEMA MWENYE KUWAOMBEA DUA WAKAZI WAKE

Unapokuwa ushakufa huku nyuma kitu kinachokusaidia ni watoto wako kama ni wema watakuwa wakikuombea dua kwa Allah akufutie makosa yako ya nyuma ,kuwa na mtoto mwema haitokei tu bahati mbaya ni maandalizi tangia unataka kuoa ,unatakiwa ujue unaenda kuoa mke wa namna gani? Sio unaenda kuoa mke kisa anatako kubwa ,lakin akhlak yake ni hovyo hapa unaenda kutengeneza kizazi cha hovyo ambacho hata ukifa unaongeezwa adhabu badala ya kunufaika na kizazi chako,





Napenda kuishia hapa ndugu zangu.haya ni baadhi tu ya mafundisho ya MTUME WETU MUHAMMAD SWALAHULLAHU ALIH WASALAMU
 
Izo ibada za wafu ni mapokeo tu na sio maagizo ya kwny maandiko,

Me sion shida iwe maiti kuchomwa,kuzikwa,kutupwa mbugani etc

Sometimes me huwa nawish tuwe km India tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…