Wanabodi,
Kiukweli kabisa mfumo dume bado ni tatizo kubwa kwa baadhi ya Watanzania wenzetu na haswa wa Kanda yetu fulani!.
Japo Rais Nyerere, Mwinyi na Mkapa, walitunukiwa PhD za heshima za honoris causa lakini hawakuitwa kwa title za Dr. Lakini Rais Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa aliitwa Dr na hakuna aliyepinga wala kupiga kelele, ila baada ya Rais Samia kutunukiwa PhD na kuanza kuitwa Dr, kelele zimeanza,
Anastahili
Hili kweli is not right, PhD za honoris causa, hazibadili title ya mtu kuitwa Dr!. Mwalimu Nyerere alipewa na hakuitwa Dr, Ali Hassan Mwinyi alipewa na hakuitwa Dr. Benjamin Mkapa alipewa na hakuitwa Dr. Jakaya Kikwete alipewa na akaitwa Dr, sasa kama JK aliitwa Dr kwa PhD ya honoria causa, na hatukusema wala kupinga, now Mama kapewa, why sasa ndio tunasema na tunapinga?.
Tuiombe TCU ilifafanue hili, kwa kuzingatia hoja ya Prof. Kironde
View attachment 2778748
Usikute sio yeye, au usikute...
ila kwa vile JK aliitwa na hakugoma, why not her?.
Sisi washauri wa bure, tumeikubali hii title ni well befitting her na tumeshauri
Baada ya kutunukiwa PhD na kuwa Dkt. mnaonaje jina la "Mama" sasa tukaachana nalo ila Nyumbani wanaweza kuendelea kumuita Mama?
Paskali