Kuota mambo ya shule ni nini tafsiri yake?

Kuota mambo ya shule ni nini tafsiri yake?

Kuna jamaa nimemsoma leo humu jukwaani ameelezea vzr sana kila aina ya kila ndoto,kwa mujibu wa maelezo ya jamaa ni kwamba"mtu akiota anafanya mitihani ni kwamba kuna jambo baya linategemea kumtokea muhusika muda siyo mrefu,ndoto za mitihani ktk ulimwengu wa roho zinawakilisha matatizo mbalimbali ktk ulimwengu wa nyama/kimwili"

Huyo jamaa anaitwa 'Mtarimbo org' jitahidi usome threads zake kuna mengi ya kujifunza ktk ulimwengu wa roho!
 
Naomba kutoa jibu la kiroho zaidi (kwa akili za kawaida halitaeleweka).

Wengi mnao ota hivyo maisha yenu bado kabisa na yamkini wengine wanasota haijawahi kutokea hata kufikia kukata tamaa....

In fact mnakabiliwa na changamoto fulani fulani ku achieve your life goals and missions.

Swali: Sasa, kitu gani kifanyike kwa akili za kawaida?

Sikia......
 
Kwa wale wote ambao wanaota wapo shule au wanafanya mtihani au mazingira yoyote ya shule hii ni ishu ya kiroho na jibu ni hili hapa;

Inakukumbusha kwamba kuna Jambo ulikuwa unalifanya na sasa either umeliacha au umeamua kupotezea,so kiroho unakumbushwa kulirudia maana Lina manufaa sn kwako endapo utafanikisha

Tupo duniani,na dunia ina mambo mengi sn ambayo shetani anapenda tusifanikiwe,so unapoota hivi maana yake ni Yule mtu wa ndani anakukumbusha kuirudia Ile njia(Jambo) ambayo umeiacha,na sasa ni km imeota majani..Kaa tafakari ni Jambo gani ambalo haujalikamilisha na sasa linakuhitaji ulirudie..Na pengine ndy Jambo ambalo lingeweza kuyabadilisha maisha yako endapo utaamua kukomaa nalo Ila negative false ( shetani) anataka usifanye hiko kitu

Satoh Hirosh
 
Wandugu hivi hii ishu ya kuota mambo ya shule mara kwa mara huwa ina maana gani kiroho!??

Nimekua nikiota ndoto kua nipo shule eidha o'level au advance na mara chache primary na chuo ila za o'level na advance ni kama kila siku tu.

Mwanzo nilikua napuuza lakini naona sasa inakua too much, karibu kila siku naota nipo shule mara nafanya pepa, nasubiri matokeo, nipo class nasoma, napiga story na wana yani zile moments nlizokua nafanya skuli ila zinakua advanced. Kama ni pepa linaweza kua gumu sana au jepesi sana.

Kuna tafsiri yoyote juu ya hizi ndoto??
Mshana Jr changia neno hapa.
 
Kwa wale wote ambao wanaota wapo shule au wanafanya mtihani au mazingira yoyote ya shule hii ni ishu ya kiroho na jibu ni hili hapa;

Inakukumbusha kwamba kuna Jambo ulikuwa unalifanya na sasa either umeliacha au umeamua kupotezea,so kiroho unakumbushwa kulirudia maana Lina manufaa sn kwako endapo utafanikisha

Tupo duniani,na dunia ina mambo mengi sn ambayo shetani anapenda tusifanikiwe,so unapoota hivi maana yake ni Yule mtu wa ndani anakukumbusha kuirudia Ile njia(Jambo) ambayo umeiacha,na sasa ni km imeota majani..Kaa tafakari ni Jambo gani ambalo haujalikamilisha na sasa linakuhitaji ulirudie..Na pengine ndy Jambo ambalo lingeweza kuyabadilisha maisha yako endapo utaamua kukomaa nalo Ila negative false ( shetani) anataka usifanye hiko kitu

Satoh Hirosh
Sasa kama ni hivi, kwanini basi mtu usiote maisha na mazingira mengine ya nyuma ambayo siyo shule?

Yani kwanini iwe shule tu?
 
Hiii ndoto uwa naota sana na cha kushangaza uwa naota nikiwa na jamaa mmoja ambaye class alikuwaga boya ila from no where jamaa akanyanyuka kimasomo na akawa mtu hatareee sana,uwa najiuliza huyu mtu kwa nn nimuote sana na mara nyingi uwa namuota tunataka kufanya mitihani
 
Kuna sehem nilisoma kuwa kama unaota sana mambo ya shule ya msingi au sekondari basi Kuna vitu havijakaa sawa,ukitaka kukamilisha jambo lako basi halifanikiwi ndo maan unaweza kuota unafanya mtihan haumalizi au umechelewa kwenye mtihan,ilimrdi tu hufanikiwi.
Aisee sasa suluhisho ni nini? Huwa naota hivo sana tu
 
Aisee sasa suluhisho ni nini? Huwa naota hivo sana tu
Tatizo la kiroho linatatuliwa kiroho,Mungu huongea na watu wake kupitia ndoto hivyo ni muhimu kujua namna yakushughulikia tatizo lako jua nguvu yako ya kiroho angalia wakati unapoomba na kumlilia Mungu na uangalie aina ya ndoto unazoota,tafsiri ya kiroho na kimwili ni tofati kabisa.....soma kisa cha ibrahim na isaka ilikuwa ndoto iliyotimia,soma ndoto za mama jusi na Yusuphu......
 
Back
Top Bottom