Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Mbona nina mwanangu mmoja yupo KADCO analamika njaa.
 
Kwakweli hali ni mbaya,huyu mjomba sijui hajui kama watu wanateseka na ugumu wa maisha?
Kuna walimu walianza kazi mwaka 2014,hawa walimu wapo kazini miaka mitano (5) sasa,lakini hajawai kuwaongezea hata nyongeza ya mshahara ,mbaya zaidi walisomeshwa na boards ya mikopo akawalazimishwa wawe wanalipa 100,000 kila mwezi mwalimu wa degree ana katwa inarud serikalini.

Jamani awamu hii watu wanateseka sana,sema kuna watu wanautetea sana utawala huu kuwa ni mzuri,nahisi hao watu wanafaidika na mfumo au wako ndani ya system ya awamu ya tano lakini kwa mwananchi wa kawaida tu tunateseka sana,malengo hayatimii kabisa yaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona nina mwanangu mmoja yupo KADCO analamika njaa.
hebu ulizia wanaofanya taasisi nilizitaja mwanzo na malipo unaweza kuta huyo jamaa anawalipa mishahara ya miezi miwili kwa mshahara wake wa mwezi mmoja kwa mtu waliye na level sawa za mishahara
 
mkuu hawa watumishi wanahitaji faraja kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote
 
hebu ulizia wanaofanya taasisi nilizitaja mwanzo na malipo unaweza kuta huyo jamaa anawalipa mishahara ya miezi miwili kwa mshahara wake wa mwezi mmoja kwa mtu waliye na level sawa za mishahara
Mwana aliniambia take home ipo around 900,sasa sijui kanipiga kamba.
 
Bila kufanya kilimo,.biashara na ufugaji..mtumishi kutoka kimaisha Ni ndoto za alinacha..mi nlishasahau kuhusu nyongeza ya mshahara

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tatizo ni mitaji,unaweza kukopa mara moja ukaweka ela kwenye biashara alafu biashara yenyewe isiimarike,au wengine walishakopa tangu awali sasa kukopa tena inakuwa haiwezekani,labda jamaa angeongeza mishahara hapo unaweza kukopa,lakini wapi.Take home imebaki laki 2 sasa hapo utakopa nini tena?[emoji3166][emoji3166]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna baadhi ya ofisi zinatambua hili so zinawafavour wafanyakazi wao kwa Allowance ili wasiwe na misongo ya mawazo.
na taasisi nyingi zinazofanya na zile zinazolipa vizuri
 
kuna baadhi ya ofisi zinatambua hili so zinawafavour wafanyakazi wao kwa Allowance ili wasiwe na misongo ya mawazo.
na taasisi nyingi zinazofanya na zile zinazolipa vizuri
Hizo kazi za maana na taasisi kubwa hizo wanaofanya kazi ni watoto wao,sisi watoto wa wakulima kazi zetu hizi hizi za ualimu,udakaktari na unesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…