Kupika au kununua kwa mamantilie

Mix tu, Ukijisikia kupika upike, Usipojiskia basi nunua... kila kimoja kina Faida na Hasara.
 
Unawaza samaki gani atakula bachelor wa maisha ya kati?

Haya basi tufanye kilo moja ya sangara mkuu. Atakula hiyo kilo moja mara ngapi?
Sijui wewe ulikuwa unamaanisha samaki gani wanne unaweza kuwapata kwa 1500 au hiyo ni bei ya samaki mmoja mmoja
 
Kujipikia kuna faida zaidi kuliko kula kwa mama ntilie ila ukiwa bado unajitafuta pika vyakula vya moja kwa moja aisee utaiona hela yako
 
Pika, raha sana kujipikia as a bachelor. Ila pika zile za long shots🀣, ubwabwa na samaki...mboga ya samaki inaliwa leo mchana, usiku, kesho uchana na usiku..that's how we lived back then.
Kama unajua kupika vileπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Acha kumfundisha kijana uvivu. Yale majogoo ungekulaje sasa bila kujipikia. 🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Halafu nimeyamiss, nifanyie wepesi basi.

Kijana anunue chakula tuπŸ˜‚
 
Nikiwa na elfu 10 tu naingia tandika pale sokoni nabeba viazi sado elfu 3, ndizi bukoba elfu 3, mihogo elfu 2, viazi vitamu elfu 2.

Naweza kupika kwa siku 4 na vikabaki
Ndizi rost karanga
Ndizi mchemsho
Viazi rost
Viazi mchemsho
Viaz kukaanga/chip - very rarely
Mihogo mchemsho
Mihogo kukaanga
Viazi mchemsho
Viazi kukaanga - very rarely

Yani mimi napika kiasi kwamba bibie anaogopa kuja kunisalimia, hajui atapika nini kiwe kipya kwangu.
 
Wakuu wasalaam.

Moja kwa moja kwenye mada.

Ikiwa unaishi mwenyewe ghetto, ipi nafuu kati ya kujipikia mwenyewe au kununua chakula kwa mama~ntilie/ mgahawani.

Ukizingatia muhusika na mwanachuo ambaye bado kiuchumi anajitafuta.

Nawasilisha
Inategemea,kupika mara nyingi ni kuzuri maana unakula vile unavyotaka,lakini pia ni hakika kwani umekiandaa mwenyewe.Hayo ndio maoni yangu.
 
Sasa hivi Kuna rice cooker,gesi n.k,unaokoa siyo gharama tu ya pesa bali hata muda ukijipikia.
Vilevile unakula chakula kingi na bora,hakuna kuwekewa amira n.k
 
Kuna mahali huku wali maharagwe wa 1500 unakula mara mbili, chapati maharagwe humalizi, chai tsh 300!!!

Kupika ununue Mchele, mafuta,chumvi, mkaa, kiberiti, maji, kitunguu, karoti, hoho bado ukae kuchoche moto kutwa nzimaπŸ˜„πŸ˜„
Ukitaka kukwepa garama za kula, siku zote utakua unakula vitu vibovu, mama nitilie hawezi nunua mchele mchele mzuri zaidi sokoni, na hata bidhaa zingine.
Kula kwa mama mtilie ikilazimika sana, ila ubora wa chakula ni mdogo sana.
 
Kwa kweli kwa mama ntilie huwezi Shiba na ukitaka kushiba itakugharimu, kupika ni vuzuri kama mda unao cha msingi tafuta friji hutoona hizo gharama wanazosema make utaweza kuhifadhi vyakula visiharibike
 

N budget nzur though nafkir chakula kilichokaa muda mrefu sana kwenye frij kinakua sio fresh tena…n kama kitakua unhealthy
 
Pika mkuu , kuepuka makamasi na chembechembe za mavi zinazobaki kwa kucha , na Yale maji ya kupikia ambayo huosha nunu wanayatumia pia usisahau kupakuliwa chakula na kiganja cha binadamu , pia maji ya kuoshea waendazao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…