Kupitia mafanikio ya Diamond Platnumz nimegundua Watanzania wengi wana roho mbaya

Unafiki na tabia yake ya kulazimisha ku-monopolise soko la muziki.

Yaani inshort anapambana kujifanya Ruge part 2.
Showbiz industry ni battle field, you fight to thrive. Unataka akae legelege kama wale midebwedo wanaoshindwa kushindana naye, kila mshiriki kwenye hiyo industry apambane kadri ya uwezo wake na wanye ubavu ndiyo watakuwa juu siku zote.
Unamchukiaje mtu kwa kupambana kijasiri ili kulimiliki soko.
 
Waswahili walishasema mkuki kwa nguruwe.

Asilimia kubwa ya hii mijitu ni minafiki.

Yaani unakuta jitu lenyewe linamchukia mtu fulani ila likiona kuna watu wengine na wao wanachukia mungu mtu wao yanaanza kubonga.
Kweli maisha bila unafiki hayaendi.
 
Huna akili
 
Wapo wanaomchukia diamond bila sababu,na wapo wanaomchukia kwa sababu

Hata yeye hajakamilika pia,hutumia nafac yake kuwafanyia wenzie mabaya pia

Vitu vingine wala havihitaji mtu akwambie tazama,mfano wa maisha ya sasa ya harmonize na WCB utaona dhahiri upande wa WCB hawana raha juu ya huyu mmakonde wanatamani leo kesho wampoteze kwa gharama yoyote ile lkn kijana nae anakomaa kama anavyokomaa diamond kwa hao wanaomchukia...WORLD IS BATTLEFIELD.
 
Unampoteza vipi msanii anayepata airtime ktk radio zote kubwa Tz na WCB wanaopata airtime Wasafi pekee.
 
Duu saikolojia yako hatar Sana, hebu tuambie ni nini hasa kinachowakosesha raha? Au wewe ndiyo huna raha kuona bwana mdogo akijitutumua bila mafanikio?
 
Watu wameshindwa kuelewa Diamond ni msanii he is not a politician ambaye ataweza badilisha maisha yao au anapigania haki za watu, anapigania mkate wake na familia yake na atafanya kwa sanaa yake kwa vyovyote, japo anakosea kujitenga na wasanii wenzake na kujiona yuko on top of the chain kwa story za mtaani na ambazo zinaonekana hakubali kufanya collabo na wasanii wenzake anafanya tu kwa few that he wants, kwa mfano mtu kama Davido nadhani so far kwa nigeria hamna msanii mwenyewe collabo nyingi kama yeye na wasanii wadogo wadogo na ndio maana ata alivo kosa award ya BET kuna watu walibaki kusema he is the best izo award hazimaanishi kitu.
 
Kwa sehemu nimemsamehe Mond.. Kumbuka alikotokea na pengine mbele ya kayafa hakuwa na jinsi
Wengi hawajamsamehe, ...niliwahi kumshauri kupitia koment za humu JF kwamba awaombe radhi watanzania.... kwani yeye anawahitaji kuliko wanavyomuhitaji, inawezekana hakuisoma ile komenti yangu.

"Hajachelewa".
Nb. Watanzania wa mitandaoni ndio watanzania halisi wanaojielewa.
 
Duu saikolojia yako hatar Sana, hebu tuambie ni nini hasa kinachowakosesha raha? Au wewe ndiyo huna raha kuona bwana mdogo akijitutumua bila mafanikio?
Saikolojia yako wewe ndo hatari zaidi kufikiria kwamba watu waliofanikiwa huwa hawana habari na watu walio nyuma yao kuelekea walipo wao(moja ya sababu ya matajiri kubaki kuwa matajiri ni kuwaangalia waliopo nyuma yao wanafanya nini)

Wanaojua kinachowakosesha raha WCB juu ya mmakonde ni WCB wenyewe na machawa wao isipokuwa sisi wengine tunaangalia tu game pande zote mbili jinsi zinavyoenda bila ushabiki maandazi tunaona upande upi unaoteseka

Ukiwa shabiki maandazi huwezi kuona wasanii wengine ni wazuri au wana mafanikio,ushabiki maandazi ndo utakufanya useme harmonize anajitutumua na hana mafanikio lkn ukirudisha utimamu wa akili huwezi kusema hivyo....siamini kwamba saikolojia yako inakwambia mimi namaanisha hapa harmonize amefanikiwa zaidi Diamond,simaanishi ivyo ila kijana harmonize mafanikio kimuziki anayo...wanaompenda Diamond wanamchukia Harmonize, wanaompenda Harmonize wanamchukia Diamond huo ndo ukweli japokuwa ni mchungu unatakiwa uupokee
 
Kwa kweli. Na hii nimeona katika maisha yangu mwenyewe na hata maisha ya kisiasa. Watanzania walio wengi wana roho mbaya sana hawapendi maendeleo ya watu.
 
Hivi kipindi kile media zilimtenga msanii gani alimtetea?

Husimuone Diamond mjinga kwenda kuzindua album yake Kenya?

Hivi hujiulizi kipindi anaanza tamasha la Wasafi, wasanii waliokuwa wakipiga show ni wa WCB, wengine walikuwa wanakatazwa kisa watanyimwa airtime (ashalizungumzi hili Chemical).

Hivi hujiulizi kwanini Collabo anazofanya Diamond zinaoipigwa Wasafi na si hizo radio kubwa nyingine za kiburudani?

Dogo ana mengi sana ya kuongea na kapitia mengi na kapigana vita vyingi, mpaka unamwona pale basi jua jamaa ana moyo wa Chuma, akina Rama dee pamoja na talent yake kubwa alishindwa,Suma G nae sijui yupo chaka gani.
 
Simba na Yanga zote wadhamini wao ni ccm lakini sijaona hao mnaojiita wapigania haki mkijitahidi kujitoa kwenye hizo timu,

Ukiona mtu anakuchukia sana ujue kuna vitu umemzidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…