Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Yaani uliposema umepoteza kuskia ladha na harufu nikajua tu tayari. Pole mkuu hii kitu imesambaa kuliko watu wanavyodhani
 
Vitu vingine ni matokeo ya hofu,kuogopa kitu kupitiliza kunaumba taswira ya kitu hicho.hayo maradhi ya mafua makali mpaka kukosa ladha na mara nyingine homa yalikuwepo kitambo sana na hata mimi huwa naugua mara kadhaa,siyo lazima ihusike na corona.

By the way corona ni ugonjwa kama magonjwa mengine utakapougua na kuthibitika utajua jinsi utakavyopambana nao.usiku mwema
Mkuu mafua nimeumwa sana lakini sijawahi poteza Sense of Smell, kwa uchunguzi nimeona tatalizo hilo limekua kubwa hivi karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari watanzania? Wiki iliyopita nilipata homa kali ghafla na nikapoteza hali ya kuweza kunusa harufu yoyote ile (Sense of Smell). Nilipata hofu sana na kwenda hospital kupima Malaria na UTI, vipimo vyote vikasoma negative basi ikanibidi nikae tu nyumbani na kuendelea kutumia malimao na machungwa baada ya kupata ushauri toka kwa watu mbali mbali huku nikisikilizia hali kwani huku nilipo mpaka kupata kipimo cha Corona ni process ndefu.

Baada ya wiki sasa ile hali imepotea na ninapata mafua na kikohozi kwa mbali. Jambo lilonifanya kuleta taarifa hii kwenu nimeona watu wengi mtandaoni hasa Facebook na Twitter wakilalamika hali hiyo na wengi wanasema iliwapata wiki iliyopita kwa kutumia tiba ya malimao wamepata nafuu.

Maswali yangu ni Je hiyo inaweza kuwa Corona? Maana napata hofu kwani mke wangu na watu wengine wa familia tangu siku hiyo mpaka leo yupo vizuri na hajapatwa na tatizo lolote wakati bado tunashare kila kitu.

Rai yangu serikali na taasisi zote za afya ziendelee na uchunguzi wa bidhaa zote hasa Sanitizers kuona kwamba zinakidhi vigezo na zisije zikawa Chanzo cha matatizo mengine mapya tukadhani ni Corona.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo ni dalili moja wapo ya Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu hamjapata suluhisho la hili tatizo?

Je munaosumbuliwa na hilo tatizo bado munaendelea vizuri?
 
Nilipigwa na hyo kitu wiki karibu tatu sisikii harufu wala ladha ku google nakuta eti wanasema dalili ya COVID 19 aseee...

Nilikua nakohoa sana pia

So nikapiga

Amplicox Dozi nzima

Asubuhi maji ya limao

Kusukutua na Chumvi na maji vuguvugu kwny koo kila bada ya masaa kadhaa

Kunywa Tangawizi mbichi ya kusaga iliyochanganwa na vitunguu saumu..

Kumung'unya viksi kingo

Baada ya wiki karibu tatu ndio harufu na ladha vikarudi na kifua kukohoa kukakoma mana ilikua kukohoa hadi mbavu zinauma.
Vita ilikua kali sana sa sujui ndio corona au lah
NB niliji lock down mwenyewe kama mkulu


Sent using Jamii Forums mobile app

Congratulations.....Covid9 hiyo.
 
Back
Top Bottom