Habari watanzania? Wiki iliyopita nilipata homa kali ghafla na nikapoteza hali ya kuweza kunusa harufu yoyote ile (Sense of Smell). Nilipata hofu sana na kwenda hospital kupima Malaria na UTI, vipimo vyote vikasoma negative basi ikanibidi nikae tu nyumbani na kuendelea kutumia malimao na machungwa baada ya kupata ushauri toka kwa watu mbali mbali huku nikisikilizia hali kwani huku nilipo mpaka kupata kipimo cha Corona ni process ndefu.
Baada ya wiki sasa ile hali imepotea na ninapata mafua na kikohozi kwa mbali. Jambo lilonifanya kuleta taarifa hii kwenu nimeona watu wengi mtandaoni hasa Facebook na Twitter wakilalamika hali hiyo na wengi wanasema iliwapata wiki iliyopita kwa kutumia tiba ya malimao wamepata nafuu.
Maswali yangu ni Je hiyo inaweza kuwa Corona? Maana napata hofu kwani mke wangu na watu wengine wa familia tangu siku hiyo mpaka leo yupo vizuri na hajapatwa na tatizo lolote wakati bado tunashare kila kitu.
Rai yangu serikali na taasisi zote za afya ziendelee na uchunguzi wa bidhaa zote hasa Sanitizers kuona kwamba zinakidhi vigezo na zisije zikawa Chanzo cha matatizo mengine mapya tukadhani ni Corona.
Sent using
Jamii Forums mobile app