Wakuu Habari.
Kama wiki 2 ziliopita nilikumbwa na mafua. Sio makali sana ila naamini ni kwa sababu nilitumia mashuka yenye vumbi.
Sasa bwana, narudi home nikapitia dukani nikanunua perfume fulani. Nafika home najipuliza haitoi harufu ata kidogo. Nikajua nimeuziwa feki. Nikasema kukikucha nitaenda lalamika. Duh, bahati mbaya umeme ulikatika jana yake, nikawa nimezima friji niliogopa ukirudi vibaya utaunguza friji (sina stabilizer) uliporudi nikawa nimesahau kuwasha iyo jioni nalifungua vitu vyote vimeoza Ila hakuna harufu ata kiduuuchu. Yaani ata kiduchu.
Hapo ndio wasiwasi ukaanza. Angalau sukari na chumvi kwa mbaaali nasikia ladha ila vitu vingine sio harufu wala ladha KABISA.
Dalili zingine ni kifua kwa mbaaali kinabana, mwili upo fresh tu.
Nikahisi naweza kua na Corona so nikajitahidi mazoezi kuruka kamba, malimao na machungwa kunywa, chai ya tangawizi.
Nimejifukiza mwarobaini na mpera ila nikaona vinanitesa tu nikaacha.
Case ya kupoteza izo sense mbili, kuna jirani yangu pia amepata na amesema ila yeye imerudi.
Nilitumua baadhi ya dawa za kifua, mafua na maumivu pia nilishauriwa. (AMPICLOX, CETRIZINE NA PARACETAMOL).
Sahivi naendelea poa kabisa ila nimejitenga. Niliogopa sana nikajua ni Corona.
PS: Kunusa na Ladha bado sijarudi ila izo dawa nimeacha kutumia.
Asanteni sana.