Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Sijui Kama nieeleweka yaani harufu ni harufu kuanzia mavi mpaka manukato namaanisha
 
Kwanza kabisa, mkuu unaelewa kwamba hiyo ni moja ya dalili kubwa kabisa za Covid-19?
 
Kama ni kweli wengi tutakua tumeugua corona..me wiki ya 3 sasa ndo naanza kupata harufu kwa mbaliii
 
Mi kwakweli nahisi Nina korona juzi Kati niliamka nimechoka viungo vinauma heri hata hangover!
Nimepiga dicloper na matangawizi jioni nikaona fresh alfajiri nikahisi Koo limekauka nikapiga maji

Asubuhi nimeamka poa juzi Jana Niko fresh kabisa Sina homa na matakataka mengine ila kusikia harufu ndo mziki
 
Nilijaribu kutafuna hadi pilipili kichaa ndo nikawa nasikia kamuwasho kwa mbaliii, na limao ndo nahisi ladha kwa mbaliii, hii ni baada ya kupitia changamoto zifatazo; kuumwa kichwa kusikoeleweka yaani kichwa kizito tuu, kichomi, mgongo kuuma, misuli, kikohozi, mafua yasiyoeleweka yaani pua haikuziba. Matibabu niliyo tumia.ciproflaxin dozi, orodar, ampiclox dozi, metro dozi, brufen, limao, tangawizi,kitunguu sahumu, juice ya ukwaju, juice ya pera, peasi.

Baada ya kupata nafuu nikabaki na hii dalili chakushangaza leo wamekuja kunyonya choo jirani kila mtu analalamika harufu nawashangaa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipata same issue. Kuanzia leo nimeanza kupata harufu na ladha.

Imenipa shida sana asubuhi kunusa nguo ili nijue kama chafu au safi. Maana me nguo uwa nanusa kwanza ndio navaa. Week izi mbili nikawa natupia tu bila kujua harufu yake.

Fanya mazoezi mzee, otea jua na Maji sana ya moto na chai.
 
Niliona kama nakufa vile,mwili ukawa kama umepondwa na mawe,
nabanwa ndani kwa ndani macho yanatoa machozi tu,
harufu hata ya chooni sisikii..
mliopitia haka kaupepo poleni naelewa shida zake
 
Mkuu nguo unanusa kwa siku ngapi na nado unaivaa tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ikifikia stage ya kutosikia harufu au ladha ndo imesepa ivyo? Na kuambukiza haiwezekani? Mi ndo leo nimeanza kutohisi ladha au harufu yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hizo antibiotics nyingi sana?
 
Acha tu mkuu... Mdomo unakuwa kama umepigwa ganzi, kama kidonda ndugu hv.
Sometimes unaweza kumlaum mpishi wa chakula hajatia chumvi kumbe hapana,
Nimewahi kula chapati + maharage wiki 3 mfululizo asubuhi+mchana+usiku maharage yenye pilipili nyingi ndio nilipenda chakula cha namna hii.. sikuwa na hamu ya chakula tofauti na hiki karibu mwezi mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…