cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 2,169
- 2,540
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?
1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.
N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi
===============
Kuchanganya tu hapa. KIla mtu ashike hamsini zake. Wao wanajitambua kama zanzibar na sisi tujitambue kama TANGANYIKA taifa huru lisilo na mashiko yoyote na zanzibar. Hii Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ifutwe mara moja.
Tutaishi nao kama vile tunavyoishi na majirani zetu wa kenya, uganda, burundi, rwanda, Zambia, Zimbabwe, na msumbiji, mbona freshi tu hakuna ubaya wowote utakaoleta shida. Mambo ya kubembeleza watu wenye entitlement mentality ni kujitesa na kupoteza muda plus kucompromise usalama wa taifa letu teule la Tanganyika ambalo kutwa kucha linaonewa wivu sababu ya umaridadi wake, umoja wake,utulivu, uvumilivu na uhimilivu.
Muungano hauna faida kwa sasa na umepoteza ladha, tunafosi sana umoja na watu wanaojiona ni first class human. Muungano uvunjwe tuishi kwa ujirani mwema tuache marumbano na visa visa vya kijinga kila siku.
Mkuu inawezekana watoto kwenye familia kuitisha kura ya maoni ili kuamua kuwa wanamtaka baba yao aendelee kuwa baba au la?
Watanganyika tumechoka kujitoa sadaka utaifa wetu kuokoa Muungano it is either One Tanzania or Shirikisho la serikali 3, hakuna njia nyingine.
Ni kuuvunja...Hili linawezekana...mojaa hasa, mbili na tatu ni siasa
Haujitoshelezi...Maana hakuwauliza ambao wanata uvunjwe.....Au kufanya Referendum kupata mawazo ya Wananchi..... Kuuvunja inawezekana pia, ili kuepusha migogoro baadaye.....Sisi hatukuwa wa kwanza kuvunja Muungano...Serikali 3. Uchambuzi wa mzee Warioba unajitosheleza.
Wazenji wapo 1.5 million tu ! Lakini ni wajanja zaidi wamewekeza kwenye Ubunge Uwaziri na vyeo vingi tu wao ni wachache lakini Viongozi ni wengi sana ambapo wanalipwa na pesa ya Jasho la Tanganyika kisha wakishiba wanaanza kulalamikia lalamika ili kuwapumbaza watanganyika wasijitfmbue Kuwa Wanachunwa Kama buzi
Serikali 3 ndiyo mpango mzima.... Mimi nashangaa CCM wanampango gani na WaTanganyika. Serikali Mbili ni Kichaka cha kugawana vyeo na Kuuza hovyo Resources za Tanganyika kwa Mgongo wa Muungano.
Hata Hivyo kama JK amemaliza Miaka yake miwili ama akiwa Angani au Nchifulani maana yake ni kwamba hatuna Rais wa kuhangaika na Mambo yetu watanganyika.
Ni mara ngapi maamuzi mazito yakawa yanasuburi ama Rais atue au Arejee kutoka nje? Je kwa nini tusiwe na Rais wa kufanya majukumu ya Tanganyika...
Kwa ni mawazo ya wananchi yakachukuliwa? India na Pakstani walijitenga.....au umesahau Soviet Union....Moja ndo mpango mzima
Gharama zote hizo za nini...Na hiyo administrative complexity itaturidisha hapa tulipo....Fanya referendum kujua wananchi wanataka nini.....Option ya kuuvunjua ni njia nyepesi zaidi, Ulimwenguni hatutakuwa wa Kwanza....India Pakistan, Bangladesh....Au mnasahau Soviet UnionSerikali iwe moja ambayo itaongozwa na Rais mmoja then kuwepo na waziri mkuu wa Zanzibar na Tanganyika hapo mambo yataenda sawa lakini eti maraisi watatu mmmmhhh hapana kwakweli
Kwani Kuna ubaya gani kuvunjika Kama hauleti faida yoyote zaidi ya hasara ya kuuliwa watu , na ikiwa watu hawautaki hasa Wazanzibari waliolazimishwa kwa mtutu wa bunduki ?serkal 2 ili kuepusha kuvunja muungano siku za usoni
Mi naona serikali ya Zanzibar na desolven na visiwa vyote view part ya Tanzania kiunumla kwamba unguja na oemba iwe mikoa na wilaya zake, na zote ziwe chini ya serikali 1 kuu, la sivyo cha zaidi hapo labda serikali 3: serikali ya bara, serikali ya Zanzibar na serikali ya muungano, ila hapo bado naona hii yote itafanyq mambo kuwa mengi namakubwa, sasa serikali 3 wafanyakazi wengi na expenses kubwa na tunavyowajua wanavyopemda kuspend hela kwenye expenses za ajabu ndio itakuwa balaa zaidi.WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?
1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.
N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi
===============
Kwanini isiwe serikali mbili kila nchi iwe na nchi yake , Muungano haupo huu ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar. Hakuna Mzanzibari wala mTanganyika aliyeulizwa kuhusu huu muungano. Hili ni balaa kubwa kwa Zanzibar tokea 1964 tunateseka. Wacha ufilie mbali Kama Cape Verde na Guinea bissau. Kila nchi ishughulike kujenga nchi yake iliyooza kwa sera Za CCMSerikali 3 ndo mpango mzima!