Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Mada na kichwa Cha mada vinapingana maana hata usiposomesha lazima wataenda kutafuta maisha sehemu nyingine na kuwaacha wazazi.
KITENDO Cha watoto kutoka bomani ni ishara ya mafanikio haijalishi nini anapitia.
Kwa mazingira yetu ya kitanzania watoto walioshindwa maisha ndo hubaki bomani na wengine Huwa mwiba kwa wazazi.

Nimependa hiyo paragraph ya mwisho wenzetu wanaoishi na watoto, wakwe na wajukuu kweli inapunguza upweke wakati wa uzee.
 
Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.

Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.

Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.

Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.

Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.​

Karibuni wakuu, kwa maoni.
Mtoa uzi upo sahihi kwa sehemu fulani lakini kwanini usomeshe watoto wako ukisubiri kupewa faraja huko uzeeni na bahati mbaya sana unakuja kupata matarajio usiyoyafurahia na kupelekea kufa mapema. Kama mzazi umebarikiwa kupata watoto basi fanya kwa uwezo wako kuwatunza, kuwasomesha na yote yanayowastahili kama watoto wako lakini usiwafanyie watoto wako yote hayo ili upate kitu in return kutoka kwa hao watoto wako utajifia mapema sana. MAISHA NI KUISHI, Wasomeshe watoto ila usisahau KUISHI, Enjoy the World.!
 
Kuna kipind nilimshauri mzee akaniona fala nikakwacha tu nilimwambia kama pesa unayo fanya business yeyote ile ambayo itakuwa home maana nyumba yake Ina kiwanja kikubwa hata kuweka mabanda ya kuku .... Sasa kaleta ujuaji kuku kapelekwa shamba ambapo ni wilayani kama km 40 kutoka anapokaa akitaka kwenda apande gari kwa nn asingeweka karibu mbaya kuna mtoto wa ndugu yake tulimwacha akae nae sasa huyo ndo anakaa huko shamba kutazamia mazao na mifugo home kabaki na mama wote umri umeenda

Dada watoto wake hawataki kukaa hapo maana mume wa dada anaona kama kupeleka watoto kwa babu yao kukaa ni kushindwa majukumu.

Kabaki mpweka wote tumetoka tunajitafutua.
 
Ila suala la Upweke katika umri mkubwa ni jambo ambalo litatutafuna sana siku za usoni. Mambo haya yamekuwa mengi sana huko Ulaya na Nchi zilizoendelea lakini hata huku Afrika linabisha hodi Kwa kasi kubwa.

Suala la kuwa na wafanyakazi wa ndani au kuoa Uzeeni bado sio solution, sana sana unaweza kupigwa tukio litakalokufanya ufe haraka kwani wenza wengi katika umri huo wanakuwa wanafata Mali kuliko kukupenda.

Binafsi nimeanza maandalizi ya kuja kuwaajiri watoto wangu kwenye kampuni zangu ili kupunguza uwezekano wa kufa Kwa upweke nyakati za Uzee wangu. Najua kampuni nawafungulia watoto but lazima wawe sehemu ya management nikiwa CEO huku tukiishi compound Moja.

Maandalizi ya Kujenga maboma makubwa yanaendelea ili vijana wangu wote waoe na kuwa na familia wakiishi kwenye Boma la Baba yao.
 
Nafikiri ni suala la kila mmoja kujipanga kwa namna yake, kila mtu anafahamu kuwa Kuna uzee mbeleni hivyo si suala la kulisubiri na kulitafutia ufumbuzi uzeeni. Hata mzazi mzee naye pia aliondoka nyumbani kwao akaenda kuishi kwake ndiyo akakuzaa wewe, waacheni watt nao watoke majumbani kwenu ili wajitegemee Kama nyinyi...ni suala la kujipanga vizuri ila si kwa kutegemea watt ndiyo watakaa nyumbani kukufariji maana itakuwa ni ubinafsi wa hali ya juu...kuhusu wahindi wao wana sababu zao zaidi ya kuondoa upweke.
 
Eti upweke
Upweke mwingine ni dalili ya ujinga.

Ni dalili ya mtu kutoweza kuwa na mawazo yanayojiongeza kupata vitu vya kum keep busy.

Ulimwengu huu una mambo mengi sana ya kuchunguza, kujua, kusoma, kufanya mazoezi, kuangalia movie, kukaa na marafiki wa rika lako, sasa hapo upweke wa kulazimisha kuwa na mtoto uzeeni unakuja vipi?

Wenzetu wanasherehekea watoto kukua, wanaishi kwa uhuru wa kupunguza majukumu ya kulea.

Sisi mara nyingi tatizo linakuwa watu wanafanya familia kuwa kama biashara.

Yani, wazazi wanalea na kusomesha watoto ili hao watoto waje kuwatunza wazazi siku wazazi wakiwa wazee.

Hapo ndipo tatizo linapoanza. Watoto wamekuwa investment ya kutunzwa uzeeni.

Hii strategy imepitwa na wakati.
 
Chukua mjukuu wa kwanza toka katika kila uzao wako.

Tuseme umebahatika watoto watatu
Kati ya hao wawili wamefanikiwa kuzaa

Chukua wajukuu uishi nao, niamini Mimi hautokuwa mpweke.

Watakuudhi ila hautobaki peke yako,
Hii ni dawa ambayo itafaa sana kwenye mazingira yetu ya kiafrika.
 
Upweke mwingine ni dalili ya ujinga.

Ni dalili ya mtu kutoweza kuwa na mawazo yanayojiongeza kupata vitu vya kum keep busy.

Ulimwengu huu una mambo mengi sana ya kuchunguza, kujua, kusoma, kufanya mazoezi, kuangalia movie, kukaa na marafiki wa rika lako, sasa hapo upweke wa kulazimisha kuwa na mtoto uzeeni unakuja vipi?

Wenzetu wanasherehekea watoto kukua, wanaishi kwa uhuru wa kupunguza majukumu ya kulea.

Sisi mara nyingi tatizo linakuwa watu wanafanya familia kuwa kama biashara.

Yani, wazazi wanalea na kusomesha watoto ili hao watoto waje kuwatunza wazazi siku wazazi wakiwa wazee.

Hapo ndipo tatizo linapoanza. Watoto wamekuwa investment ya kutunzwa uzeeni.

Hii strategy imepitwa na wakati.
Mi napenda nikizeeka tujenge nyumba eneo kubwa Ili tufuge mifugo yote mpaka nyoka ... nikiwa Mimi na mume wangu🤸🤸🤸🤸😘
 
mbona kusomeaha haihusiani na kua mpweke inategemea umekuzaje familia yako. wapo wazazi wameweka familia karibu watt wamesoma na wanapomaliza wanafunguliwa miradi ya familia na wanaiendesha vizur na wanakua karibu na familia muda wote ila familia maskini lazma watt watoke waende wakatafute(ninapoongelea familia maskini niko kwenye upande wa kutoweza anzisha biashara za kifamilia mbazo hao watt waliosoma wataweza au wataona wana thamani ya kuiendesha)
 
Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.

Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?

Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.

Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.

Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Ni kweli tuwasaidie wazazi wetu....lakini wanaomba kwa kutumia nguvu kama vile kuna kitu alikuwekesha....
 
Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.

Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?

Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.

Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.

Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Kweli akili ni nywele umeelewa alichoandika au umekurupuka kutoka usingizini
 
Kweli akili ni nywele umeelewa alichoandika au umekurupuka kutoka usingizini
Mimi siwezi kufikiri sawa na wewe kwa sababu tunatofautiana kwa mengi, sasa wewe kulazimisha tufikiri sawa ni ujinga wako, siwezi kukusaidia.

Wewe umejionesha kuwa sio tu huna akili, bali pia huna hata utashi.

Kwa sababu hata hukuweza kunieleza unapofikiri nimekosea ni wapi. Hukuweza hata kuniuliza kwa nini nafikiri kama ninavyofikiri.

Ukikosoa, onesha unakosoa kwa sababu hii, onesha hapa ni makosa, na hiki ndicho sahihi, ili hata wewe uwape nafasi watu kukukosoa.

Sio unakosoa kama mlevi wa boha, you don't have rhyme or reason!

You are a brutish Philistine.
 
Ni kweli,hiyo situation imetokea kwa bi mkubwa wangu mara baada ya sisi watoto wake kuwa na maisha yetu na kuishi mbali na nyumbani na mzee kufariki. Tunajitahidi kumtafutia watu wa kukaa naye ambao ni wafanyakazi na watoto wa ndugu ila changamoto zimekuwa Ni nyingi hivyo hujikuta anabaki mwenyewe.Hii imenifanya nifikiri sana maisha yangu yatakavyokuwa baada ya watoto wangu wote kuondoka nyumbani na kwenda kujitegemea.
Ili kukabiliana na hii hali nimeamua kuanzisha vitega uchumi ndani ya eneo langu la makazi maana ninaishi kwenye mojawapo ya majiji hapa nchini.Kati ya hivyo vitega uchumi nitafungua ofisi ambayo itanifanya nikutane na watu Mara kwa mara na hizo ofisi nyingine nitazipangisha hivyo muda mwingi nitakuwa na communicate na watu.Ikifika muda nikawa mzee sana kiasi Cha kushindwa kutoka hata nje ya nyumba basi watoto wangu itabidi wabebe jukumu la kujua nitaishije maana nitakuwa nimepoteza nguvu na uwezo wa kufikiri.
Shetani anataka ufikirie sana kuhusu kesho ili ushindwe kuishi leo
 
Back
Top Bottom