Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.

Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?

Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.

Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.

Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Inafikia kipindi hela haifanyi kazi katika kukuondolea upweke; bali unakuwa unataka uwe karibu na uzao wako, ila inashindikana kutokana na uzao wako kuwa mbali kwenye maisha mengine
 
Ni kweli,hiyo situation imetokea kwa bi mkubwa wangu mara baada ya sisi watoto wake kuwa na maisha yetu na kuishi mbali na nyumbani na mzee kufariki. Tunajitahidi kumtafutia watu wa kukaa naye ambao ni wafanyakazi na watoto wa ndugu ila changamoto zimekuwa Ni nyingi hivyo hujikuta anabaki mwenyewe.Hii imenifanya nifikiri sana maisha yangu yatakavyokuwa baada ya watoto wangu wote kuondoka nyumbani na kwenda kujitegemea.
Ili kukabiliana na hii hali nimeamua kuanzisha vitega uchumi ndani ya eneo langu la makazi maana ninaishi kwenye mojawapo ya majiji hapa nchini.Kati ya hivyo vitega uchumi nitafungua ofisi ambayo itanifanya nikutane na watu Mara kwa mara na hizo ofisi nyingine nitazipangisha hivyo muda mwingi nitakuwa na communicate na watu.Ikifika muda nikawa mzee sana kiasi Cha kushindwa kutoka hata nje ya nyumba basi watoto wangu itabidi wabebe jukumu la kujua nitaishije maana nitakuwa nimepoteza nguvu na uwezo wa kufikiri.
Umeona mbali mkuu; nilikuwa najiuliza kwa nini wahindi huwa wanakaa kwenye boma moja? mwisho wa siku nikagundua, ni kuweka mazingira ya kutokuwa wapweke huko mbeleni
 
Ukiwa na miaka 70+ ni mtihani mkuu
Ukiwa na maiak 70+ unatakiwa uwe unafurahia pensheni na wenzako walio 70+.

Sio unalazimisha watu wakutoe upweke. Hii ni tabia ya ubinafsi sana.

Wewe unaweza kujiona unapenda watu, kumbe ni mbinafsi unataka attention yote iwe kwako.
 
Ila suala la Upweke katika umri mkubwa ni jambo ambalo litatutafuna sana siku za usoni. Mambo haya yamekuwa mengi sana huko Ulaya na Nchi zilizoendelea lakini hata huku Afrika linabisha hodi Kwa kasi kubwa.

Suala la kuwa na wafanyakazi wa ndani au kuoa Uzeeni bado sio solution, sana sana unaweza kupigwa tukio litakalokufanya ufe haraka kwani wenza wengi katika umri huo wanakuwa wanafata Mali kuliko kukupenda.

Binafsi nimeanza maandalizi ya kuja kuwaajiri watoto wangu kwenye kampuni zangu ili kupunguza uwezekano wa kufa Kwa upweke nyakati za Uzee wangu. Najua kampuni nawafungulia watoto but lazima wawe sehemu ya management nikiwa CEO huku tukiishi compound Moja.

Maandalizi ya Kujenga maboma makubwa yanaendelea ili vijana wangu wote waoe na kuwa na familia wakiishi kwenye Boma la Baba yao.
Wazo lako linaweza kuwa suluhisho kwenye hili tatizo; na ndivyo wenzetu wa Asia wanafanya.
 
Mwanaume atawaacha wazazi wake naye ataambana na mkewe...

Hapa neno la Biblia linaonyesha kuwa kuna wakati wazazi watabaki peke yao maana watoto wataenda kuanzisha familia zao...
Inaumiza sana, ulishazoea kelele za vijana wako, hatimaye wanakuja kukutenga
 
Ni kweli tupu mimi nilifikiri hali ya upweke kwa wazazi ni tatizo la Ulaya na lingechukua muda mrefu sana kufika Africa lakini tayari lipo sana tena linakuwa hatari kuliko hata Ulaya kwani umaskini hulifanya tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.
Tena nyinyi wazazi wa kizazi hiki ambao watoto wenu mnawapeleka wakakulie kwenye vituo vya Day Care kisa nyie mpo busy kutafuta pesa ndio mjipange kisawasawa. Msipojipanga vizuri na wao lazima wawapeleke kwenye elderly centers.
 
Mi napenda nikizeeka tujenge nyumba eneo kubwa Ili tufuge mifugo yote mpaka nyoka ... nikiwa Mimi na mume wangu🤸🤸🤸🤸😘
Kwa mazingira hayo; mkiwa na miaka 70+ upweke hautawatatiza?
 
Wazo lako linaweza kuwa suluhisho kwenye hili tatizo; na ndivyo wenzetu wa Asia wanafanya.
Mzee Mengi alifanikiwa kwenye hili pia, hadi anafariki vijana wake walikuwa ni Watumishi kwenye biashara zake pale IPP.

Muda wa kuweza kujiandaa na kufika huko upo, muhimu kujipanga na kuomba uhai tu.
 
Back
Top Bottom