The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Assuming sina mpango wa kufariki, hapo unanisaidiaje?
Unazaa mtoto mwingine wa kukufariji na kuchangamsha nyumba.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Assuming sina mpango wa kufariki, hapo unanisaidiaje?
Uko sahihiUnaiandika kama mtu ambaye hajasoma au ambaye hujapata exposure yoyote kuna umri unafika pesa c chochote zaidi ya watu nyumbani tulikuwa 17 kipindi nakuwa, nyumba ilikuwa na vyumba 9 Leo hii kabaki Bibi na dada yake na mfanyakazi na mtoto WA mjomba ana kila kitu pesa gari mashamba analimisha na anapata mazao kibao Tu Ila kila siku anataka wajukuu wake akakkae nawo Ila ndyo ivyoo ata ujipange VIP kuna umri utafika utaitaji watu wa Kula nawo meza, kucheka nawo, na kujifariji hasa pale unapoumwa ndyo maana wahindi au waarabu wengi wanakaa kama familia wengi tunaona kama ushamba Ila lile ni Jambo jema sana kwenye kutunza wazee wenu
Hii ni akili ya kitoto sana.upendo unazidi kushuka siku zinavyozidi.ilawewe ukiugua na kuwa kilema kabisa ukafilisika unataka mzazi aendelee kukulea mpaka kifo chako?Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.
Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?
Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.
Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.
Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Ili upate faraja kwa kusikia kelele za wapangajiHata Ivo nimeghairi...uzee nitapanga then nyumba yangunitapangisha😔
Wazee wa kucheza baoMimi sitojutia na nimejiandaa kwa hilo,kwani mtaani hakuna vijiwe?
Ukiwa na familia na ukawaza kwa mapana hayo mambo lazima uyaone.mfano mm nimeshajua chanzo Cha kwa nn watoto wa kiume huwatelekeza wazazi wao wa kiume na kumjali mama yao.wakipiga cm inaanzia kwa mama kwanza .nikajiuliza kama mm nafanya hv Ina maana na mm nitafanyiwa na watoto wangu.hvyo nilibadilisha mfumo wa maisha kuwa rafiki wa watoto wangu na kuwatekelezea mahitaji Yao kalibu 80% nawapatia mm mwenyewe Moja kwa Moja sio kumpatia mama Yao.Ni kweli,hiyo situation imetokea kwa bi mkubwa wangu mara baada ya sisi watoto wake kuwa na maisha yetu na kuishi mbali na nyumbani na mzee kufariki. Tunajitahidi kumtafutia watu wa kukaa naye ambao ni wafanyakazi na watoto wa ndugu ila changamoto zimekuwa Ni nyingi hivyo hujikuta anabaki mwenyewe.Hii imenifanya nifikiri sana maisha yangu yatakavyokuwa baada ya watoto wangu wote kuondoka nyumbani na kwenda kujitegemea.
Ili kukabiliana na hii hali nimeamua kuanzisha vitega uchumi ndani ya eneo langu la makazi maana ninaishi kwenye mojawapo ya majiji hapa nchini.Kati ya hivyo vitega uchumi nitafungua ofisi ambayo itanifanya nikutane na watu Mara kwa mara na hizo ofisi nyingine nitazipangisha hivyo muda mwingi nitakuwa na communicate na watu.Ikifika muda nikawa mzee sana kiasi Cha kushindwa kutoka hata nje ya nyumba basi watoto wangu itabidi wabebe jukumu la kujua nitaishije maana nitakuwa nimepoteza nguvu na uwezo wa kufikiri.
Inawezekana ikawa sababu kuu, watoto kutokwenda kwa babu/bibi zaowatamfundisha uchawi[emoji23]
[emoji23][emoji23] mawazo hayo mda huo yanatoka wapi, ? Mnakua mnawaza kuzaa tuSomesha ila zaa katika interval fulani itakayokufanya muishi na katoto kenu ka mwisho muda mrefu mpaka kufikia kaoe mnakuwa mmeshafariki
Ndio janga lijalo!Tena nyinyi wazazi wa kizazi hiki ambao watoto wenu mnawapeleka wakakulie kwenye vituo vya Day Care kisa nyie mpo busy kutafuta pesa ndio mjipange kisawasawa. Msipojipanga vizuri na wao lazima wawapeleke kwenye elderly centers.
Kwanza kabisa, umewanyanyapaa watoto kwa kauli yako "hii ni akili ya kitoto sana".Hii ni akili ya kitoto sana.upendo unazidi kushuka siku zinavyozidi.ilawewe ukiugua na kuwa kilema kabisa ukafilisika unataka mzazi aendelee kukulea mpaka kifo chako?
Mchepuko ndio kazi yake hiyoKupeleka mtoto wako akalelewe na baba yako ni uzembe. ufumbuzi ni mzee asikubali mpangilio wa watoto wanne(4)tu eti basi zalisha mpaka mbegu ziishe
Kuna watoto wengine hawapendi kuwaacha watoto wao kwa wazazi waoWajukuu si wapo, shida nini
Labda uchelewe kuzaa ndio utaishi na watoto mpk uzeeni wako karibuWazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.
Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.
Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.
Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.
Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.
Karibuni wakuu, kwa maoni.
Kwani watoto si ni baraka?🤣au imekuaje tena?Yasije yakatokea kama yale ya Arusha......mzee kafungiwa ndani, hapewi chakula siku nyingi, mpaka kaanza kula haja yake. Yote hiyo mtoto anataka kurithi. Anyway, yote ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
Mbona hujamuelewa Kiranga? Yeye kaongelea upweke na faraja, hayo mambo yakunipanga sijui nini....Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.
Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?
Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.
Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.
Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Hata hayo ya upweke na faraja mbona nimeyaandika, hujasoma?Mbona hujamuelewa Kiranga? Yeye kaongelea upweke na faraja, hayo mambo yakunipanga sijui nini....
umeleta wewe na hii inapaswa kuwa maada nyingine. Ukiweza anzisha.