Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Chukua mjukuu wa kwanza toka katika kila uzao wako.

Tuseme umebahatika watoto watatu
Kati ya hao wawili wamefanikiwa kuzaa

Chukua wajukuu uishi nao, niamini Mimi hautokuwa mpweke.

Watakuudhi ila hautobaki peke yako,
Hii ni dawa ambayo itafaa sana kwenye mazingira yetu ya kiafrika.
Mzazi gani mwenye uwezo analelewa wanae na babu/bibi sikuhizi?
 
Unaiandika kama mtu ambaye hajasoma au ambaye hujapata exposure yoyote kuna umri unafika pesa c chochote zaidi ya watu nyumbani tulikuwa 17 kipindi nakuwa, nyumba ilikuwa na vyumba 9 Leo hii kabaki Bibi na dada yake na mfanyakazi na mtoto WA mjomba ana kila kitu pesa gari mashamba analimisha na anapata mazao kibao Tu Ila kila siku anataka wajukuu wake akakkae nawo Ila ndyo ivyoo ata ujipange VIP kuna umri utafika utaitaji watu wa Kula nawo meza, kucheka nawo, na kujifariji hasa pale unapoumwa ndyo maana wahindi au waarabu wengi wanakaa kama familia wengi tunaona kama ushamba Ila lile ni Jambo jema sana kwenye kutunza wazee wenu
I can feel the loneliness of my parents too
4 bedrm
3 rms zimebaki hakuna mkaaji
 
Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.

Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?

Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.

Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.

Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Hujamuelwa mtoa mada. Yeye amezungumzia upweke siyo utegemezi kwa watoto.
 
Hujamuelwa mtoa mada. Yeye amezungumzia upweke siyo utegemezi kwa watoto.
Ukiwa mpweke, ukategemea watoto wakutoe upweke, hujaweka utegemezi kwa watoto hapo?

Kwani utegemezi kwa watoto ni lazima uwe wa kiuchumi?

Endelea kusoma posts zangu nimeandika sana kuhusu upweke katika dunia hii yenye megi ulivyo aina moja ya uzembe.
 
Kwamba nisisomeshe kuepuka upweke🤔..hapana!..nitaomba hata wajukuu niishi nao na Kama haitoshi nitaomba hata watoto wa ndugu niishi nao pia.
 
Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.

Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?

Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.

Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.

Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Wewe umelenga sana kwenye hitaji la kiuchumi kitu ambacho si sawa sana...
Nafikiri hiki kitu ni mzunguko tu wa maisha..lkn jamii nyingi ambazo ni za kijasiliamali wameweza sana kupunguza hili tatizo...Wahindi,Waarabu etc wanaishi nyumba moja wengi forever
 
Tena nyinyi wazazi wa kizazi hiki ambao watoto wenu mnawapeleka wakakulie kwenye vituo vya Day Care kisa nyie mpo busy kutafuta pesa ndio mjipange kisawasawa. Msipojipanga vizuri na wao lazima wawapeleke kwenye elderly centers.
Yap waliwapeleka watt day care watt nao wanakuwa wanawapeleka wazazi elderly centers 🙂
 
Wazo zuri sana
Kuna my frnd 51 yrs bado kazaa
Means hadi 75 yrs(51+24) binti anaweza kuwa bado nyumbani anachangamsha mji😅

Na bado yaelekea anataka amalizie akiwa 55😅😅
Kuchelewa kuzaa kuna faida pia, ingawa kwa wanawake ni vigumu kuchelewa
 
Kwamba nisisomeshe kuepuka upweke🤔..hapana!..nitaomba hata wajukuu niishi nao na Kama haitoshi nitaomba hata watoto wa ndugu niishi nao pia.
Kuletewa wajukuu ni mtihani pia
 
Ukiangalia tamthilia nyingi za kituruki, utagundua kua wao wanautaratibu mtoto wa kiume haondoki nyumbani. Ataoa na kumleta mke nyumbani kwao. Atapewa chumba chake maisha yanaendelea kama kawaida.
Ndio maana maisha yao yanakua mazuri, kwani watoto hawafikiri kujenga tena, wakati nyumba ipo ya babu yao.
 
Maisha ni bahati.
Acheni kupoteza pesa nyingi kwenye elimu mkidhani hii ndio itawafanya watoto, watoke kimaisha!
Apparently the most paid CEO nchini, ametoka huku! Hajasoma Ilboru, Mzumbe wala UDSM
Screenshot_20220812-150628.jpg
 
Back
Top Bottom