Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Ni kweli tuwasaidie wazazi wetu....lakini wanaomba kwa kutumia nguvu kama vile kuna kitu alikuwekesha....
Mzazi hatakiwi kuomba, yani inatakiwa aweze kumlea mtoto wake vizuri kiasi huyo mtoto aweze kumsaidia mzazi kabla mzazi hajaomba.

Ukishaona mzazi anaomba ujue kakosea sehemu fulani kubwa mbili.

1. Kwanza kakosea hajajipanga kujitosheleza yeye mwenyewe.
2. Pili kakosea hajajipanga kuwa karibu na mtoto na kumuwezesha mtoto kusaidia kabla hajaombwa.
 
Upweke mwingine ni dalili ya ujinga.

Ni dalili ya mtu kutoweza kuwa na mawazo yanayojiongeza kupata vitu vya kum keep busy.

Ulimwengu huu una mambo mengi sana ya kuchunguza, kujua, kusoma, kufanya mazoezi, kuangalia movie, kukaa na marafiki wa rika lako, sasa hapo upweke wa kulazimisha kuwa na mtoto uzeeni unakuja vipi?

Wenzetu wanasherehekea watoto kukua, wanaishi kwa uhuru wa kupunguza majukumu ya kulea.

Sisi mara nyingi tatizo linakuwa watu wanafanya familia kuwa kama biashara.

Yani, wazazi wanalea na kusomesha watoto ili hao watoto waje kuwatunza wazazi siku wazazi wakiwa wazee.

Hapo ndipo tatizo linapoanza. Watoto wamekuwa investment ya kutunzwa uzeeni.

Hii strategy imepitwa na wakati.
Unaiandika kama mtu ambaye hajasoma au ambaye hujapata exposure yoyote kuna umri unafika pesa c chochote zaidi ya watu nyumbani tulikuwa 17 kipindi nakuwa, nyumba ilikuwa na vyumba 9 Leo hii kabaki Bibi na dada yake na mfanyakazi na mtoto WA mjomba ana kila kitu pesa gari mashamba analimisha na anapata mazao kibao Tu Ila kila siku anataka wajukuu wake akakkae nawo Ila ndyo ivyoo ata ujipange VIP kuna umri utafika utaitaji watu wa Kula nawo meza, kucheka nawo, na kujifariji hasa pale unapoumwa ndyo maana wahindi au waarabu wengi wanakaa kama familia wengi tunaona kama ushamba Ila lile ni Jambo jema sana kwenye kutunza wazee wenu
 
Unaiandika kama mtu ambaye hajasoma au ambaye hujapata exposure yoyote kuna umri unafika pesa c chochote zaidi ya watu nyumbani tulikuwa 17 kipindi nakuwa, nyumba ilikuwa na vyumba 9 Leo hii kabaki Bibi na dada yake na mfanyakazi na mtoto WA mjomba ana kila kitu pesa gari mashamba analimisha na anapata mazao kibao Tu Ila kila siku anataka wajukuu wake akakkae nawo Ila ndyo ivyoo ata ujipange VIP kuna umri utafika utaitaji watu wa Kula nawo meza, kucheka nawo, na kujifariji hasa pale unapoumwa
Nimeandika mengi, zaidi ya pesa.

Kuwa tegemezi ni tatizo pia, hata ukiwa na pesa.

Mtu kuwa needy, yani huwezi kuwa peke yako ukafanya mambo yako, kuhitaji hitaji watu kila saa, ni tatizo la kisaikolojia pia.

Na tatizo hili ni zaidi ya pesa, ni mindset problem.

Yani mtu kukaa nyumbani peke yake, au na mkewe tu, anaona tatizo tayari.

Maana yake mtu huyu hana uwezo wa kuwa self contented, hawezi kusoma kitabu, hawezi kuanzisha urafiki mpya na watu wapya.

Watu wako tegemezi sana, na hili ni tatizo lililozidi pesa.

Tatizo la self confidence, tatizo la kushindwa kuwa na utashi, tatizo la kushindwa kuwa na hobby, ni tatizo la watu wenye akili ndogo.

Sasa kati ya mimi mtu anayejua kwamba unaweza kuondoa upweke kwa kusoma na wewe unayekubali mtu kuingia upweke kwa kuwa peke yake, unaniambia mimi sijasoma, kati yetu nani hajasoma?
 
Unaiandika kama mtu ambaye hajasoma au ambaye hujapata exposure yoyote kuna umri unafika pesa c chochote zaidi ya watu nyumbani tulikuwa 17 kipindi nakuwa, nyumba ilikuwa na vyumba 9 Leo hii kabaki Bibi na dada yake na mfanyakazi na mtoto WA mjomba ana kila kitu pesa gari mashamba analimisha na anapata mazao kibao Tu Ila kila siku anataka wajukuu wake akakkae nawo Ila ndyo ivyoo ata ujipange VIP kuna umri utafika utaitaji watu wa Kula nawo meza, kucheka nawo, na kujifariji hasa pale unapoumwa ndyo maana wahindi au waarabu wengi wanakaa kama familia wengi tunaona kama ushamba Ila lile ni Jambo jema sana kwenye kutunza wazee wenu
Uzuri wa JF hata Baba yako aliekuzaa,akakulea,akakusomesha unaweza kumwambia hajasoma na hana exposure.
 
Ila suala la Upweke katika umri mkubwa ni jambo ambalo litatutafuna sana siku za usoni. Mambo haya yamekuwa mengi sana huko Ulaya na Nchi zilizoendelea lakini hata huku Afrika linabisha hodi Kwa kasi kubwa.

Suala la kuwa na wafanyakazi wa ndani au kuoa Uzeeni bado sio solution, sana sana unaweza kupigwa tukio litakalokufanya ufe haraka kwani wenza wengi katika umri huo wanakuwa wanafata Mali kuliko kukupenda.

Binafsi nimeanza maandalizi ya kuja kuwaajiri watoto wangu kwenye kampuni zangu ili kupunguza uwezekano wa kufa Kwa upweke nyakati za Uzee wangu. Najua kampuni nawafungulia watoto but lazima wawe sehemu ya management nikiwa CEO huku tukiishi compound Moja.

Maandalizi ya Kujenga maboma makubwa yanaendelea ili vijana wangu wote waoe na kuwa na familia wakiishi kwenye Boma la Baba yao.
Tamaduni za wahindi hizo.
 
Kila Kona shimo kuu wewe😳 huko uani si ulozi wake ndo unampeleka.Na hatosameheka na Mwenyez Mungu 😏
Haaaya, nilitaka kujua tu unaongelea nyoka au nyoka?

Sasa nishakufahamu. Sasa unataka nyoka kila kona na watoto kibao nyumbani uzeeni itakuwaje hapo?

Huoni hatari?
 
Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.

Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.

Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.

Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.

Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.​

Karibuni wakuu, kwa maoni.
Huu uzi umekaa kibaguzi sana
 
Mtoa uzi upo sahihi kwa sehemu fulani lakini kwanini usomeshe watoto wako ukisubiri kupewa faraja huko uzeeni na bahati mbaya sana unakuja kupata matarajio usiyoyafurahia na kupelekea kufa mapema. Kama mzazi umebarikiwa kupata watoto basi fanya kwa uwezo wako kuwatunza, kuwasomesha na yote yanayowastahili kama watoto wako lakini usiwafanyie watoto wako yote hayo ili upate kitu in return kutoka kwa hao watoto wako utajifia mapema sana. MAISHA NI KUISHI, Wasomeshe watoto ila usisahau KUISHI, Enjoy the World.!
Wewe hujamuelewa mtoa mada upweke na huduma ni vitu viwili tofauti mtoa mada kaelezea upweke hajaelezea kukosa huduma unaweza kuwa na kilakitu ndani lakini upweke ukakusesha faraja, na unaweze kua na upungufu wa huduma lakini maliwazo yakakupa faraja
 
Haaaya, nilitaka kujua tu unaongelea nyoka au nyoka?

Sasa nishakufahamu. Sasa unataka nyoka kila kona na watoto kibao nyumbani uzeeni itakuwaje hapo?

Huoni hatari?
Hata Ivo nimeghairi...uzee nitapanga then nyumba yangunitapangisha😔
 
Wewe hujamuelewa mtoa mada upweke na huduma ni vitu viwili tofauti mtoa mada kaelezea upweke hajaelezea kukosa huduma unaweza kuwa na kilakitu ndani lakini upweke ukakusesha faraja, na unaweze kua na upungufu wa huduma lakini maliwazo yakakupa faraja
Upweke kuupata uzeeni wakati maisha yote ulijua upweke wa uzeeni unakuja ni ujinga fulani hivi.

Maana yake mtu kashindwa kujiandaa vizuri na maisha ya uzeeni.

Yani kashindwa hata kununua vitabu ambavyo hakuwa na muda wa kusoma ujanani akavisoma uzeeni?

Upweke mwingine ni dalili ya mtu kukosa hobby na kutokuwa mtashi/ interesting.Mtu mwenye hobby na aliye mtashi/ interesting hawezi kuwa mpweke.
 
Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.

Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.

Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.

Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.

Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.​

Karibuni wakuu, kwa maoni.
Mimi sitojutia na nimejiandaa kwa hilo,kwani mtaani hakuna vijiwe?
 
Back
Top Bottom