Mtoa uzi upo sahihi kwa sehemu fulani lakini kwanini usomeshe watoto wako ukisubiri kupewa faraja huko uzeeni na bahati mbaya sana unakuja kupata matarajio usiyoyafurahia na kupelekea kufa mapema. Kama mzazi umebarikiwa kupata watoto basi fanya kwa uwezo wako kuwatunza, kuwasomesha na yote yanayowastahili kama watoto wako lakini usiwafanyie watoto wako yote hayo ili upate kitu in return kutoka kwa hao watoto wako utajifia mapema sana. MAISHA NI KUISHI, Wasomeshe watoto ila usisahau KUISHI, Enjoy the World.!Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.
Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.
Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.
Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.
Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.
Karibuni wakuu, kwa maoni.
Upweke mwingine ni dalili ya ujinga.Eti upweke
Mi napenda nikizeeka tujenge nyumba eneo kubwa Ili tufuge mifugo yote mpaka nyoka ... nikiwa Mimi na mume wangu🤸🤸🤸🤸😘Upweke mwingine ni dalili ya ujinga.
Ni dalili ya mtu kutoweza kuwa na mawazo yanayojiongeza kupata vitu vya kum keep busy.
Ulimwengu huu una mambo mengi sana ya kuchunguza, kujua, kusoma, kufanya mazoezi, kuangalia movie, kukaa na marafiki wa rika lako, sasa hapo upweke wa kulazimisha kuwa na mtoto uzeeni unakuja vipi?
Wenzetu wanasherehekea watoto kukua, wanaishi kwa uhuru wa kupunguza majukumu ya kulea.
Sisi mara nyingi tatizo linakuwa watu wanafanya familia kuwa kama biashara.
Yani, wazazi wanalea na kusomesha watoto ili hao watoto waje kuwatunza wazazi siku wazazi wakiwa wazee.
Hapo ndipo tatizo linapoanza. Watoto wamekuwa investment ya kutunzwa uzeeni.
Hii strategy imepitwa na wakati.
Wajukuu si wapo, shida niniSomesha ila zaa katika interval fulani itakayokufanya muishi na katoto kenu ka mwisho muda mrefu mpaka kufikia kaoe mnakuwa mmeshafariki
Ni kweli tuwasaidie wazazi wetu....lakini wanaomba kwa kutumia nguvu kama vile kuna kitu alikuwekesha....Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.
Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?
Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.
Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.
Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Kumbe ilikuwa ni wajibu wake coz yeye ndo alikuleta dunianNi kweli tuwasaidie wazazi wetu....lakini wanaomba kwa kutumia nguvu kama vile kuna kitu alikuwekesha....
Kweli akili ni nywele umeelewa alichoandika au umekurupuka kutoka usingiziniKuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.
Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?
Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.
Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.
Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Nyoka unampendea kipi?Mi napenda nikizeeka tujenge nyumba eneo kubwa Ili tufuge mifugo yote mpaka nyoka ... nikiwa Mimi na mume wangu🤸🤸🤸🤸😘
Mimi siwezi kufikiri sawa na wewe kwa sababu tunatofautiana kwa mengi, sasa wewe kulazimisha tufikiri sawa ni ujinga wako, siwezi kukusaidia.Kweli akili ni nywele umeelewa alichoandika au umekurupuka kutoka usingizini
kweli kabisaWapo wengine wanatafuta hata watoto wa majirani, angalau wachangamshe mji
Shetani anataka ufikirie sana kuhusu kesho ili ushindwe kuishi leoNi kweli,hiyo situation imetokea kwa bi mkubwa wangu mara baada ya sisi watoto wake kuwa na maisha yetu na kuishi mbali na nyumbani na mzee kufariki. Tunajitahidi kumtafutia watu wa kukaa naye ambao ni wafanyakazi na watoto wa ndugu ila changamoto zimekuwa Ni nyingi hivyo hujikuta anabaki mwenyewe.Hii imenifanya nifikiri sana maisha yangu yatakavyokuwa baada ya watoto wangu wote kuondoka nyumbani na kwenda kujitegemea.
Ili kukabiliana na hii hali nimeamua kuanzisha vitega uchumi ndani ya eneo langu la makazi maana ninaishi kwenye mojawapo ya majiji hapa nchini.Kati ya hivyo vitega uchumi nitafungua ofisi ambayo itanifanya nikutane na watu Mara kwa mara na hizo ofisi nyingine nitazipangisha hivyo muda mwingi nitakuwa na communicate na watu.Ikifika muda nikawa mzee sana kiasi Cha kushindwa kutoka hata nje ya nyumba basi watoto wangu itabidi wabebe jukumu la kujua nitaishije maana nitakuwa nimepoteza nguvu na uwezo wa kufikiri.