Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Culture culture ndio upuuzi gani wewe ? .Hayo ni mashirika ya umma ,kila mtu ana haki ya kuomba na kushindana kupata kazi ,acha upuuzi wenu huo wa kujihisi nyie ndio wateule mnaijipa entitlement ya kupata hizo kazi .
Who the fvck are you ?
Kazi zirudishwe psrs kila mtu apewe Chande sawa ya kushindana.
Ninyi ndio vilaza vyeti feki na watumishi hewa ,mnataka muingie kwenye system kinyemela tu .
Unajua hata madhumuni ya kuanzishwa mfumo wa PSRS wewe ? ,Au unadhani psrs ilianzishwa kama pambo tu ?
Mnakera sana
 
Lkn hoja hiyo hai- legitimize process ya recruitment internally Kwa nafasi zote hizo Kwani NSSF ni Public Entity yenye masilahi mapana ya Kila mwananchi.
Hata hivyo,ruhusa Kwa Taasisi hizo kuajiri wenyewe badala ya PSRS sidhani ilimaanisha wapunguze ushindani Kwa kuzuia wengine wasiombe,bali wangetangaza Kwa Kila mwenye sifa aombe na wao wangekuwa strict kwenye SHORTLIST na INTERVIEW na kuzingatia uzoefu wa kazi husika ambapo obvious watu competent wangepatikana ikiwemo Hawa walioko INTERN na Wenye FIXED CONTRACT,otherwise hiyo ni kama kupeana ushindi wa mezani
 
Kwani ww ulipoomba hapo internal ulikuwa unajua au ndo baada ya kujua unaleta dharau zako....
Nini maana ya kutoa training kwa waajiriwa wap!!!
Alafu unasisitiza MIMI sio Mnafiki
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Ukianza kazi kama Intern ni taasisi chache sana zitakazopoteza RESOURCES kukupa training, hata ktk MPANGO wa Mafunzo (TP) TRAINEE huwa Haingii.
KWANZA una kiwango gani cha Elimu? Nisiwe natwanga maji kwenye kinu hapa.
 
Hongera sana kwa kuwa tajiri, ni ili linaonyesha ni namna gani ulivyo mbinafsi, na wewe pia najua ni mmojawapo wawapenyezaji watu wako wa intern uko..
 
Haya Majinga yamejazana ktk Magrp ya Whatsapp yanatagemea link itumwe au PDF itumwe ndio wakimbilie kuomba.

Wenzao wanasaka mlango kwa mlango. Alafu wanakuja kupiga makelele
 
Huo uzoefu uliopata kama Intern inatakiwa ukusaidie kushinda kwenye FAIR Competition lakini siyo kulilia ushindi wa mezani Kwa ku- restrict wengine wasiombe nafasi
 
Kuna TAASISI hizo hizo za serikali ww hauna HAKI ya kupata AJIRA.

AJIRA sio haki ya Kila Mtanzania.

Ajira upate basi UFITI na vigezo na masharti yanayoambatana na AJIRA husika.

Toeni hiyo DHANA ya Ajira ni haki kwa kila MTANZANIA na muamini kwamba AJIRA NI KWA YULE MWENYE VIGEZO husiku/STAHIKI.
 
Ukianza kazi kama Intern ni taasisi chache sana zitakazopoteza RESOURCES kukupa training, hata ktk MPANGO wa Mafunzo (TP) TRAINEE huwa Haingii.
KWANZA una kiwango gani cha Elimu? Nisiwe natwanga maji kwenye kinu hapa.
Kwa mtu aliyesoma fani akaelewa,kazi nyingi kama hizo za NSSF siyo Sky- Rocketing ni za kawaida sana mtu akipewa ORIENTATION ya one or two weeks ana master Kila kitu tusiwanyime wengine ridhiki Kwa cheap justification
 
Namashaka Sana na elimu yako pitia vizuri Uzi mkuu Acha kutunisha misuli ya kichwa shirikisha na ubongo pia elewa Uzi huu unasemaje, serikali haina uwezo wa kuajiri wasomi wote, Ila kuwe na Mfumo wa haki katika utafutaji wa izo Ajira.
 
Inabidi Tujue ni Nafasi Gani hasa. Hilo moja.

Kuna kazi hata ufanyeje watatoka watu wa humo humo ktk pool. Na hao ndio priority ya kwanza..

Wakisema waweke experience 2yrs utaskia MALALAMIKO ohh SISI WATOTO WAMASKINI sijui nn
 
Hivi ni kweli mama Samia utakaa kimya katika hili? Hili la kuwatenga watanzania walio wengi kwenye fursa ya ajira huko NSSF? Au utajiunga na baadhi ya wana CCM wenye roho ngumu ambao husema "kelele za chura hazimzuii mtu kuteka maji". Kilio na malalamiko haya ni makubwa sana, na tegemeo la wananchi ni kuona Rais wao akiwatetea dhidi ya vigogo wanaojali matumbo yao tu na yale ya watoto wao basi!! Vigogo hao tayari walishapeleka watoto wao na jamaa zao kwenye taasisi mbalimbali za umma "kwa gia ya kujitolea" na mikataba mifupi. Halafu yakaanza kampeni hadharani kutaka waliojitolea wapewe kipaumbele!! Rais wetu mpendwa chonde chonde usilalie upande wa vigogo hao wenye uroho na ubinafsi uliokithiri. Ninajua NSSF wakiachwa waendelee na ubaguzi huu, mashirika mengine yatafuata!
 
Hongera sana kwa kuwa tajiri, ni ili linaonyesha ni namna gani ulivyo mbinafsi, na wewe pia najua ni mmojawapo wawapenyezaji watu wako wa intern uko..
Ukiwa KICHWA why nisikufanyie RECOMMENDATIONS?? Binafsi nahusudu sana mfumo wa HEAD HUNTING haujawahi kufeli huo mfumo.

Ila huu ujinga wa KUITANA watu 30k mnafanyishwa mitihani ni upuumbavu kabisa. Sitaki hata kuusikia
 
Namashaka Sana na elimu yako pitia vizuri Uzi mkuu Acha kutunisha misuli ya kichwa shirikisha na ubongo pia elewa Uzi huu unasemaje, serikali haina uwezo wa kuajiri wasomi wote, Ila kuwe na Mfumo wa haki katika utafutaji wa izo Ajira.
Wewe si nimekuuliza uliomba nafasi gani hujanijibu? Uliomba lini? Na kwa njia gani?

Na uniambie hilo tangazo ulipata wapi wakati unasema Hawatangazi nafasi.
 
Kwa mtu aliyesoma fani akaelewa,kazi nyingi kama hizo za NSSF siyo Sky- Rocketing ni za kawaida sana mtu akipewa ORIENTATION ya one or two weeks ana master Kila kitu tusiwanyime wengine ridhiki Kwa cheap justification
Mfano kazi gani labda. Ya kufundishwa wiki moja au mbili?
Itaje.
 
Ukiwa KICHWA why nisikufanyie RECOMMENDATIONS?? Binafsi nahusudu sana mfumo wa HEAD HUNTING haujawahi kufeli huo mfumo.

Ila huu ujinga wa KUITANA watu 30k mnafanyishwa mitihani ni upuumbavu kabisa. Sitaki hata kuusikia
Head Hunting mostly hufanyika kwa nafasi chache na unique and Very Specialized Jobs like Neuro Surgeon etc lakini siyo Kwa hizi Entry Jobs Kwa wingi huu wa 300+ kama hizi za NSSF
 
Wewe si nimekuuliza uliomba nafasi gani hujanijibu? Uliomba lini? Na kwa njia gani?

Na uniambie hilo tangazo ulipata wapi wakati unasema Hawatangazi nafasi.
Nilipita mlango kwa mlango majibu niliyopewa basi...kwa nafasi za intern walizotangaza pia niliomba na nilitwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…