Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Utaratibu wa kujaza nafasi za Utumishi wa Umma ni tofauti na private kama ungekuwa na kampuni yako ni sawa. Ila kwenye Utumishi wa Umma Ajira ni kwa ushindani,usawa na uwazi na ninaposema Ushindani ni lazima uangalie waliopo ndani na waliopo nje. Naomba kama una nafasi usome na kupitia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali inayoguide masuala ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
😁 nikuulize swali jepesi tu dogo sana.

TISS recruitment yao inatangazwa wapi? Ukinipa majibu hapo sitaendelea na Mjadala.
 
Umesoma tangazo vizuri mkuu?
Unajua maana ya wafanyakazi wenye " Fixed contract" ndio wanatakiwa waombe.
Hawa wenye fixed contract wanatakiwa kurenew contract sio kuomba kazi. Hili tangazo maana yake wanaingia kwenye ajira ya kudumu na sio promotion kama unavyosema hapà
Mashrti ya Kudumu unafkiri kibali chake ni chepes kias hicho ee?
 
Kuna mda unafanya jambo ukiamini utainekana una akili kumbe nduo unatamgaza ujinga wakom Internal vacancy ni process legal kabisa na mara nyingi huwa inalenga kupandisha watu madaraja maana unaomba kazi iliyo juu yako. Then hizo nafasi zinazoachwa ndio wanapewa new comers ambao hawajui kazi wanaanza. Ila hizo za internal zinataka wanaojua kazi za NSSF zinafanywaje daily, yaani hapo unapata kazi halafu hamna ataeanza kukuambia majukumu yako ni haya. Kama ulikuwa msaisizi wa boss sasa unakuwa boss so unajua cha kufanya.
Umerukia mada bila kujua kinachoongelewa kwa undani!! Hatuzungumzii kupandisha watu madaraja, hatuzungumzii watu ambao tayari ni waajiriwa wa NSSF na wanataka kupewa nafasi nyingine ndani ya NSSF. Tunazungumzia habari ya waajiriwa wapya na NSSF kuamua kutoa nafasi hiyo kwa "wanaojitolea na wenye mikataba mifupi-(hawa si waajiriwa, hawafanyiwi kupandishwa madaraja kama unavyodai, au kubadilishiwa nafasi)". Wewe ndo umetangaza ujinga kwa kurukia bila kujua undani na huenda hata hilo tangazo hujalisoma binafsi.
Hizo kazi zilizotangazwa kwa mujibu wa sifa zinazohitajika zilizoainishwa hawakusema inabidi uwe na uzoefu wa miaka kadhaa (eg compliance officer II, Accounts officer II, Assistant compliance officer II etc,) hizi kazi zote ni za first appointment, na mtu yeyote mwenye sifa stahiki anaweza kuzifanya. Maelekezo kwa mwajiriwa mpya ni ya lazima kupitia induction program/course (kama hujui maana ya induction course pole!!. Post walizotangaza NSSF zimekuwa zikitangazwa mara nyingi na PSRS kwa taasisi mbalimbali.
 
Mashrti ya Kudumu unafkiri kibali chake ni chepes kias hicho ee?
Kwamba kuna kibali cha masharti ya kudumu na vibali vingine? Mimi ni nguli wa masuala haya kaka. Nimegundua unajibu tu ili ujibu. Rejea issue nilizoeleza hapo juu. Hiyo ndio best practise na haijawahi kubadilika. Nsssf wamechemka big time.
 
😁 nikuulize swali jepesi tu dogo sana.

TISS recruitment yao inatangazwa wapi? Ukinipa majibu hapo sitaendelea na Mjadala.
Yaani kwa akili yako unalinganisha TISS na NSSF. Unataka kanuni zinazoendesha TISS ndo ziigwe na taasisi zingine? Unaijua TISS kweli au unaisikia tu!! Kama ndo akili zako zinakutuma hivyo, basi unastahili kusamehewa bure!!
 
Hii ndo maana halisi ya connection sasa tunayoipinga umu
Endelea kukaza fuvu, kwa hii MENTALITY yako wewe ukiajiriwa utaleta shida sana ktk maeneo ya kazi.

Ndio maana watu wanakuja humu JF wanaandika nyuzi za kuomba kusaidiwa kazi au kibarua. Mimi mwenyewe niliwahi kuandika kuomba huo MSAADA humu.

Sasa kama hujui maana ya NETWORKING endelea kukomalia huo ujinga wako.
 
Kwamba kuna kibali cha masharti ya kudumu na vibali vingine? Mimi ni nguli wa masuala haya kaka. Nimegundua unajibu tu ili ujibu. Rejea issue nilizoeleza hapo juu. Hiyo ndio best practise na haijawahi kubadilika. Nsssf wamechemka big time.
Unataka kusema nini KATIBU anatoa VIBALI kulingana na aina ya MKATABA wewe una unguli gani bhana hujui kitu simpo hicho na ww kumbe TAKATAKA tu wacha nifanye mambo ya msingi.
 
Yaani kwa akili yako unalinganisha TISS na NSSF. Unataka kanuni zinazoendesha TISS ndo ziigwe na taasisi zingine? Unaijua TISS kweli au unaisikia tu!! Kama ndo akili zako zinakutuma hivyo, basi unastahili kusamehewa bure!!
Umetumia neno UTUMISHI wa UMMA.

turudi mezani MIONGOZO ya UTUMISHI wa UMMA hata RAIS mwenyewe vinamhusu moja kwa MOJA. AU Tiss sio UTUMISHI WA UMMA?

Umejiona ulivyo na Akili fupi
 
Endelea kukaza fuvu, kwa hii MENTALITY yako wewe ujiajiriwa utaleta shida sana ktk maeneo ya kazi.

Ndio maana watu wanakuja humu JF wanaandika nyuzi za kuomba kusaidiwa kazi au kibarua. Mimi mwenyewe niliwahi kuandika kuomba huo MSAADA humu.

Sasa kama hujui maana ya NETWORKING endelea kukomalia huo ujinga wako.
Mmh! sijipambani Mimi Mwenywe kuna wengine pia kama Mimi wanahitaji izo nafasi, nikifanya unavyotaka wewe vitatokea vitu vya ovyo ovyo sana, fikiria vizazi vinavyofwata kwa huu upuuz wako nini kitatokea, anyway sio lazima wasomi wote waajiriwe atleast kuwe na Mfumo wa haki Ajira ni haki ya kila mtu
 
Kuna TAASISI hizo hizo za serikali ww hauna HAKI ya kupata AJIRA.

AJIRA sio haki ya Kila Mtanzania.

Ajira upate basi UFITI na vigezo na masharti yanayoambatana na AJIRA husika.

Toeni hiyo DHANA ya Ajira ni haki kwa kila MTANZANIA na muamini kwamba AJIRA NI KWA YULE MWENYE VIGEZO husiku/STAHIKI.
Sasa vigezo unavipima Kwa ku-restrict wengine au Kwa kufanya MCHAKATO ulio wazi ambao una EFFECTIVE competition?
 
Kuamua kuajiri wa ndani au nje ni uamuzi wa Taasisi maana unakuta ana watu wako na mikataba ya muda mfupi na wanaojitolea (interns) zikitokea fursa lazima awatazame kwanza wale maana wameshafundishwa na wanauzoefu.
 
Back
Top Bottom