Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Kwanini michakato yote ya ajira kwenye taasisi isisimamiwe na sekretarieti ya ajira? Huu uhuni usingekuepo
Na huo uhuni ndio ulisababisha lile tatizo la vyeti feki (watumishi wasio na sifa ) + watumishi hewa ambapo genge la wahuni wanapata pesa kupitia watumishi ambao hawa exist katika mfumo .
Imetumika miaka zaidi ya sita kipindi cha Magufuli , serikali haiajiri sababu inashughulikia hilo tatizo la vyeti feki na watumishi hewa , vitu ambavyo vimekuwa vikiicost nchi katika kutengeneza ufanisi hafifu katika hizo Taasisi na mashirika ya uma + kufyonza mapato ya nchi ambayo yalikuwa yanaingia mifukoni mwa wahuni flani .
At the same time ikazalisha tatizo la wasomi kurundikana mitaani , kwani ni miaka 6+ serikali haijairi wakati vyuo vinazidi kuzalisha wasomi mtaani .
Leo hayo yote kuna wapumbavu hawaoni , wanataka warudishe tatizo lile lile ambalo limeicost nchi kipindi cha nyuma .
Huu ni utaahira na haikubaliki .

PSRS wasimamie mfumo wa ajira kwa public sector na Institutions , Period !
 
Huu mfumo wa kuruhusu kila taasisi za serikali ku recruit kwa njia zake wenyewe.. hakuna fair competition.. ni rahisi sana rushwa na undugu pamoja na kucreate nafasi za wafanyakazi hewa
Haya naomba nikujibu kwa experience.

Hayo uliyoyataja hayaepukiki yapo na yatendelea kuwepo isipokuwa hapo ktk wafanyakazi HEWA.

Hakuna loopholes za kupenyeza wafanyakazi hewa. Why?

Mifumo inasomana kwa sasa endapp utakuwa na ajira mpya utamuingiza muajiriwa huyo ktk MFUMO wa usimamizi rasilimali watu. Huo mfumo upo integrated na NIDA. Hivyo hakuna duplications au Ghost employees. Pia kuna UKAGUZI wa mara kwa mara unafanywa na Msajili wa HAZINA Kuverify watumishi, data zao na stahiki wanazopata.

Pia NECTA verification (Vetting) ni lazima na inafanywa kwa kila ajira mpya. Hivyo si rahisi kuingiza ghost employee.

Natumaini nimekujibu kwa Hoja na kama utauliza au utapingana na hoja zangu nakuomba ujibu kwa HOJA.
 
Kodi unalipia matak😠😠 wakati huna ajira, hembu kaa kimya maskini wewe
Wewe utakuwa umezaliwa juzi ndio maana unafikiri kutukana ndio majibu! Nikufundishe kuwa kulipa kodi si mpaka uajiriwe hata kununua bidhaa ni moja ya njia ya kulipa kodi! Kwanza
Kwenye ajira kuna kodi kidogo sana ulilinganisha na kwenye huduma ,bidhaa na manunuzi…ili mradi unaishi na unapata
Huduma basi kila leo unalipa kodi!
Kuna kodi za moja kwa moja na kodi zisizo za moja kwa moja! Muwe mnajipa muda kusoma kidogo!
 
Point mkuu, nakazia zaid ata iyo vocha aliyonunua akaweka bando aje atukane hapa ina Kodi pia arejea msg baada ya kuiweka ataaona
 
Katk recruitment processes kuna INTERNAL AND External sources za kupata hao wanaowataka.

Mie sioni shida hapo. Na navyofikiri.. hao NSSF wanamamlaka ya kuajiri Kwa MKATABA wa muda fulani na sio ule mkataba wa PERMANENT.

hivyo kuna aina nyingi za mikataba ikiwemo huo wa Specific TASK ambao ukimaliza hiyo shughuli ndio basi unasepa na kuna mkataba wa Muda yaan mwaka/miaka.

Naona wanataka kuwabadirisha mkataba wale wanaowataka. Na sio kama ni PERMANENT (Kwa navyoona).

Ni zoez la kuhuisha mikataba hapo.

Serikal inapoelekea inatoa AJIRA sawa ila AJIRA nyingi zitakuwa za MIKATABA mifupi mifupi na sio zile za PERMANENT.

Hapa umeweka mawazo yako wewe na sio hitaji la tangazo linavyotaka.
 
HAPANA!! Huko NSSF kuna interns wengi sana walioingizwa huko kwa gia za kujitolea, na baadhi yao wakapewa hiyo mikataba mifupi mifupi. Zoezi zima lilianza pasipo uwazi na kwa upendeleo!! Sasa wanataka waingie "king"!! Ajira kwenye utumishi wa umma lazima ziwe wazi kwa watanzania wote bila kubagua!! Hapa panafuka moshi!!

Kuna taasisi hata interns tu wanazitangaza.. volunteers pia zinatangazwa. Sasa hawa jamaa zetu wanataka kuhalalishana kirahisi tu.
 
Upo sahihi kabisa watu wanapotosha maana na sababu ya kufanya Internal recruitment.Kwanza internal recruitment inahusu wale walioajiriwa kwa mkataba wa kudumu..permanent employees na sio interns wala wa kujitolea...maana internal recruitment haipunguzi nafasi za ajira kwani akitoka nafasi moja kwenda ingine ile aliyoiacha inakuwa wazi....kama ni kujazia nafasi interns,waliojitolea na wengine wana haki sawa kabla ya interview kuajiriwa
Soma tangazo mkuu kama msomi usicomment tu kwa kufuata comment za watu. Je kwenye tangazo kuna neno "Permanent " umeliona au umeamua kujiongeza?
 
Haya naomba nikujibu kwa experience.

Hayo uliyoyataja hayaepukiki yapo na yatendelea kuwepo isipokuwa hapo ktk wafanyakazi HEWA.

Hakuna loopholes za kupenyeza wafanyakazi hewa. Why?

Mifumo inasomana kwa sasa endapp utakuwa na ajira mpya utamuingiza muajiriwa huyo ktk MFUMO wa usimamizi rasilimali watu. Huo mfumo upo integrated na NIDA. Hivyo hakuna duplications au Ghost employees. Pia kuna UKAGUZI wa mara kwa mara unafanywa na Msajili wa HAZINA Kuverify watumishi, data zao na stahiki wanazopata.

Pia NECTA verification (Vetting) ni lazima na inafanywa kwa kila ajira mpya. Hivyo si rahisi kuingiza ghost employee.

Natumaini nimekujibu kwa Hoja na kama utauliza au utapingana na hoja zangu nakuomba ujibu kwa HOJA.
Walipoingia kwenye mkataba walishindanishwa na nani?
Unakumbuka wafanyakazi wa taasisi moja ya kilimo waliouawa na wanakijiji Morogoro wakizaniwa ni wanyonya damu?
Kati ya wale wafanyakazi alikuwepo mtoto wa kigogo wa hiyo taasisi alikuwa anajitolea ndio alikuwa amemaliza kidato cha sita tu.
Huu ni mfano mmoja mdogo tu.
 
na
Kuna taasisi hata interns tu wanazitangaza.. volunteers pia zinatangazwa. Sasa hawa jamaa zetu wanataka kuhalalishana kirahisi tu.
na icho ndo tunachokitaka kwanini taasisi zingine zitangaze alafu nyingine hamna, mfumo uliopo sio rafiki, kuna wengine wapo mbali na hayo maeneo na wanataman sana izo intern na uko kuvolunteer eeh wao wanapataje taarifa?
 
Walipoingia kwenye mkataba walishindanishwa na nani?
Unakumbuka wafanyakazi wa taasisi moja ya kilimo waliouawa na wanakijiji Morogoro wakizaniwa ni wanyonya damu?
Kati ya wale wafanyakazi alikuwepo mtoto wa kigogo wa hiyo taasisi alikuwa anajitolea ndio alikuwa amemaliza kidato cha sita tu.
Huu ni mfano mmoja mdogo tu.
hii ni hatari sana,
 
Ulafi na unafiki mwingine hadi aibu!! Wanajifanya wanahurumia waliojitolea kumbe ni gia ya kutoa ajira kwa ndugu zao waliowapachika kwenye taasisi za umma kwa gia ya kujitolea na mikataba mifupi mifupi! NSSF hatukubali katika hili. Watu wa ndani ni watanzania wote, na si watoto wa vigogo tu mnaowalea huko baada ya kushindwa ushindani kupitia PSRS!!
 
Tunakutegemea sana Rais Samia kusimama upande wa Watanzania wote na si upande wa walafi wanaotaka fursa zote za ajira ziwe kwa ndugu zao tu!! Hili la NSSF kuwaona watanzania wengine kuwa wako nje halikubaliki!!
Rais wetu ni msikivu na anapenda haki, na ndo sababu ata akatoa ajira nyingi kwa vijana, kwa izi baraka za mama rais wetu kuna baadhi ya watu wasio waaminifu wenye nia ya kumchafua wanapitia umo umo, ili halikubaliki ata kidogo aingilie kati
 
Inawezekana Sasa Hawa wamewezaje kutangaza? Kila mtu aone
Screenshot_20230920-214207~2.png
Screenshot_20230920-214112~2.png
 
Na Nina hakika ata ukienda sehemu izo walizozitaja kwenye notes board zao za matangazo utalikuta pia. Ichi ndicho tunachokitaka ata nafasiza kujitolea ziwe wazi watu waombe Kwa kufuata taratibu, na hii itasaidia ata Kwa walioko mbali kuziona wanaotaka kujitolea.
 
Back
Top Bottom