Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Kusema ukweli siyo uchawa, Wala kumpongeza mh Rais kwa kujenga umoja wa kitaifa haliwezi kuwa kosa la jinai
Nachozungumzia mimi ni wingi wa picha ambazo walizigawa wenyewe uwanjani na hoja iliyotolewa, sio kwamba namnanga Rais no asikubali watu wanaompa sifa za kijinga kijinga ambazo huwezi kuprove kitaalam kuwa ndio kigezo cha kukubalika.
 
Ila nikusifu maana hupanic, unajibu kistaarabu. Ingawa sipendi theme za mada zako.
Sina sababu za kupanic Wala kumtukana mtu hata akinutukana matusi ya aina yoyote Ile maana sote tuna Nia njema ya kuona Tanzania inakuwa Bora Zaid ya Leo na kwamba kila mtu anainuka kiuchumi, siyo tufe na njaa wakati tuna Mito kila mahali na maziwa ambayo tunaweza fanya kilimo Cha umwagiliaji tukapata chakula Cha kutosha na tukauza kingine na kupata fedha za kigeni zitakazo tusaidia katika manunuzi ya vitu vingine Kama vile baadhi ya madawa hospitalini

Hatutaki kuona wanafunzi wetu wakikaa chini wakati tuna Miti ya mbao maelfu kwa maelfu huko iringa tunayoweza kupasua mbao na kutengeneza madawati ya wanafunzi wetu na wakakaa vizuri wakati wanajifunza darasani

Hatutaki mtoto wa masikini akae nyumbani kwa kukosa Ada wakati tuna uwezo wa kufuta Ada ili kila mtoto apate haki na fursa ya Elimu

Ndio maana nampongeza mh Rais wetu mpendwa mama Samia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kuona kila mtanzania ananufaika na fursa zinazopatikana katika nchi yetu, lakini pia serikali ya mama Samia inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa inagusa maisha ya mtanzania mnyonge anayehitaji kusaidiwa, maana kazi ya serikali Ni kusaidia watu na siyo kuumiza watu wake, hiki ndicho afanyacho mama Samia kuhakikisha anasaidia watanzania kuinuka kiuchumi
 
Nachozungumzia mimi ni wingi wa picha ambazo walizigawa wenyewe uwanjani na hoja iliyotolewa, sio kwamba namnanga Rais no asikubali watu wanaompa sifa za kijinga kijinga ambazo huwezi kuprove kitaalam kuwa ndio kigezo cha kukubalika.
Hakuna ubaya wowote ule kwa mtu kupongezwa afanyapo vyema, ndio maana ya uanzishwaji wa tuzo mbalimbali Duniani Kama sehemu ya kutoa motisha kwa watu
 
Sina sababu za kupanic Wala kumtukana mtu hata akinutukana matusi ya aina yoyote Ile maana sote tuna Nia njema ya kuona Tanzania inakuwa Bora Zaid ya Leo na kwamba kila mtu anainuka kiuchumi, siyo tufe na njaa wakati tuna Mito kila mahali na maziwa ambayo tunaweza fanya kilimo Cha umwagiliaji tukapata chakula Cha kutosha na tukauza kingine na kupata fedha za kigeni zitakazo tusaidia katika manunuzi ya vitu vingine Kama vile baadhi ya madawa hospitalini

Hatutaki kuona wanafunzi wetu wakikaa chini wakati tuna Miti ya mbao maelfu kwa maelfu huko iringa tunayoweza kupasua mbao na kutengeneza madawati ya wanafunzi wetu na wakakaa vizuri wakati wanajifunza darasani

Hatutaki mtoto wa masikini akae nyumbani kwa kukosa Ada wakati tuna uwezo wa kufuta Ada ili kila mtoto apate haki na fursa ya Elimu

Ndio maana nampongeza mh Rais wetu mpendwa mama Samia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kuona kila mtanzania ananufaika na fursa zinazopatikana katika nchi yetu, lakini pia serikali ya mama Samia inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa inagusa maisha ya mtanzania mnyonge anayehitaji kusaidiwa, maana kazi ya serikali Ni kusaidia watu na siyo kuumiza watu wake, hiki ndicho afanyacho mama Samia kuhakikisha anasaidia watanzania kuinuka kiuchumi
Umeandika ila inategemea upande uliopo kwenye shilingi, upande wa uongozi au kwa wananchi.

Umesema mafanikio mengi tunashukuru ungeweza kutuletea data zinazo onyesha positive move towards maendeleo unayozungumzia kama elimu (ubora wa elimu), fursa, njinsi serikali imegusa wanyonge n.k.
 
Hapo umeamka zako saivi godoro ulilo lalia limebonyea katikati ukilala chaga zinagusa mbavu, dagaa wameisha na tu-unga tumebaki kidogoo kwenye kamfuko keusi. Wapangaji wenzako wanakudai buku mbili ya umeme unawapiga chenga tu siku ya nne leo, endelea kulala usingizini kenge wewe
Yote Ni maisha tu yawe Ni ya dagaaa au samaki au mlenda au mihogo, lakini pia hata Kama mtu anadaiwa siyo dhambi maana ndio ukubwa wenyewe na utu uzima, Sasa Kama wewe unamcheka mtu ukiona anadaiwa Basi utakuwa hujaanza kuyaishi maisha halisi na hujapitia shida, pia usimcheke Wala kumdharau mtu kwa kuwa anapitia shida au matatizo ya kiuchumi hata Kama umepanga Naye jirani chumba

Ukiwa na nafasi na ukaona mtu anateseka au anahangaika msaidie kwa kadri ya uwezo wako japo huwezi kumsaidia kila mtu lakini unaweza ukasidia hata mmoja ambaye akafurahi katika moyo wake na kubaki anakuombea kila siku ili mwenyezi Mungu akubariki

Pia hata ukimsaidia mtu usisubiri fadhira kutoka kwake maana awezaye kukulipa wewe Ni Mwenyezi Mungu pekee, hivyo usimdharau mtu kwa kipato chake au Hali yake ya umaskini maana kupata Ni Majaliwa,Aliyekupa wewe ndio aliye mnyima Yule unayemdharau na hujuwi atampa lini

Naona umeniita kenge, Hata hivyo Naheshimu mtizamo wako na ninaendelea kuheshimu michango yako humu maana tunaweza kubishana kwa hoja bila kutukanana
 
Umeandika ila inategemea upande uliopo kwenye shilingi, upande wa uongozi au kwa wananchi. Umesema mafanikio mengi tunashukuru ungeweza kutuletea data zinazo onyesha positive move towards maendeleo unayozungumzia kama elimu (ubora wa elimu), fursa,njinsi serikali imegusa wanyonge n.k.
Nakupa mfano mmoja unaonihusu Mimi mkulima, mwaka Jana mbolea ilikuwa Bei juu Sana mfano mbolea ya DAP iliuzwa kwa laki na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70 tu baada ya utolewaji wa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini, Hapa mh Rais Amegusa maisha ya mtanzania mnyonge moja kwa moja kwa kuwa secta ya kilimo ndio mahali utakapokuta kundi kubwa la watanzania linategemea secta hii kuendesha maisha yao, hapa Ni Kama wakulima tulipewa pumzi Safi
 
Ni ujinga tu mkuu, siku zinavyozidi kwenda ndio watanzania wanazidi kuwa wajinga. Tumekuwa na shule na vyuo vingi nchini lakini unashangaa watu wanazidi kuwa wajinga tu, tena inashangaza zaidi wale waliopata bahati ya kupita huko vyuoni ndio wametoka wakiwa wajinga wabobevu.

Chunguza uone hilo wazo la kubeba picha za marais kwenye mpira huwa linatoka kwa nani utashangaa.

Kubali tu kuwa mh Rais Samia anakubalika na kupendwa Sana na watanzania
 
Sasa ndio inavyotakiwa kutoa hoja zako safi sana, Angalia na vingine virkezee hivyo hivyo hoja inapata mashiko zaidi
 
Ndugu zangu Rais Samia hakika amefanikiwa kujenga umoja wa kitaifa, amefanikiwa kuliunganisha Taifa, amefanikiwa kuwaweka watanzania pamoja, amefanikiwa kuishi katika mioyo ya watanzania , Amefanikiwa kupanda mbegu ya Uzalendo katika mioyo ya watanzania

Sasa picha ya Rais Samia inashangiliwa uwanjani Tena katika mchezo mkubwa siyo tu Tanzania Bali katika Bara Zima la Afrika, picha ya Rais Samia inaleta furaha na Tabasamu kwa mashabiki uwanjani, picha ya Rais Samia inakuwa sehemu ya burudani na furaha ya mchezo, mashabiki wote wa timu zote wanafurahi kuona picha ya Rais Samia ikiwa inapepea uwanjani

Hii ni kutokana na kuwa kila mtu na kila shabiki wa mpira anamuona Rais Samia kuwa Ni Rais wake na kiongozi wake, Hakuna mwenye chuki na Rais Samia, Hakuna mwenye kinyongo na mama Samia, hakuna mwenye Hasira na mama Samia. Kila Shabiki akiona picha ya Rais Samia mbele ya uwanja anaona furaha na Tumaini, kila mtu anahisi Rais Samia Ni mshabiki wa timu yake na anajisikia fahari,

Hakika Rais Samia Ni kipenzi Cha watanzania, Ni Tumaini la watanzania, furaha ya watanzania ,kiongozi aliyeteka mioyo ya watanzania, kiongozi anayekubalika na watu wote vijana kwa wazee. Ukifanikiwa kupenya katika mioyo ya wanamichezo maana yake umefanikiwa kukaa katika mioyo ya watanzania maana mchezo wa mpira ndio mchezo unaopendwa na watu wengi Sana Tanzania na unao waunganisha watu bila kujari itikadi zao za kisiasa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Duuh!! Unashindwa kusifu, kuabudu, kumuimbia na kumchezea Mungu wako,badala yake unamgeuza binadamu mwenzako "mungu"!!!???

Kweli umasikini wa akili na kipato ni vitu vya kutorithisha watoto wetu.
FB_IMG_1666485775346.jpg
 
Nasubili kuja kumpigia kura uchaguzi ujao na kumpigia kampeni mitaani nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa kwa miguu yangu

Hahitaji kura, anahitaji vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi kumtii basi. Akipata hayo anakuwa rais kwa kishindo hata kama hakuna mtu yoyote atajitokeza kupiga kura.
 
Ndugu zangu Rais Samia hakika amefanikiwa kujenga umoja wa kitaifa, amefanikiwa kuliunganisha Taifa, amefanikiwa kuwaweka watanzania pamoja, amefanikiwa kuishi katika mioyo ya watanzania , Amefanikiwa kupanda mbegu ya Uzalendo katika mioyo ya watanzania

Sasa picha ya Rais Samia inashangiliwa uwanjani Tena katika mchezo mkubwa siyo tu Tanzania Bali katika Bara Zima la Afrika, picha ya Rais Samia inaleta furaha na Tabasamu kwa mashabiki uwanjani, picha ya Rais Samia inakuwa sehemu ya burudani na furaha ya mchezo, mashabiki wote wa timu zote wanafurahi kuona picha ya Rais Samia ikiwa inapepea uwanjani

Hii ni kutokana na kuwa kila mtu na kila shabiki wa mpira anamuona Rais Samia kuwa Ni Rais wake na kiongozi wake, Hakuna mwenye chuki na Rais Samia, Hakuna mwenye kinyongo na mama Samia, hakuna mwenye Hasira na mama Samia. Kila Shabiki akiona picha ya Rais Samia mbele ya uwanja anaona furaha na Tumaini, kila mtu anahisi Rais Samia Ni mshabiki wa timu yake na anajisikia fahari,

Hakika Rais Samia Ni kipenzi Cha watanzania, Ni Tumaini la watanzania, furaha ya watanzania ,kiongozi aliyeteka mioyo ya watanzania, kiongozi anayekubalika na watu wote vijana kwa wazee. Ukifanikiwa kupenya katika mioyo ya wanamichezo maana yake umefanikiwa kukaa katika mioyo ya watanzania maana mchezo wa mpira ndio mchezo unaopendwa na watu wengi Sana Tanzania na unao waunganisha watu bila kujari itikadi zao za kisiasa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Nonsense.
 
Hahitaji kura, anahitaji vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi kumtii basi. Akipata hayo anakuwa rais kwa kishindo hata kama hakuna mtu yoyote atajitokeza kupiga kura.
Hata ije tume kutoka marekani kusimamia uchaguzi bado Rais Samia atashinda kwa kishindo maana anakubalika na kupendwa Sana na watanzania
 
Mimi bado nashangaa Kama wengine wanavyoshangaa.....kuwa ukiwa na picha ya Rais unashinda mechi yako.au kutoa draw. Nashauri Yanga waende nazo Tunisia
 
Back
Top Bottom