Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Niende tu kwenye mada kwani kichwa imevurugika hata sielewi.
Nilifunga ndoa ya kanisani miaka kadhaa nyuma. Baada ya kama miaka mitatu yandoa tukashindwana kila mtu akawa na maisha yake. Mwaka jana nikafunga ndoa ya serikali na mke mwingine bila kuvunja ile ndoa ya kwanza.
Tatizo limekuja baada ya kumkatia huyu mwanamke bima ya NHIF na kuanza kupokea huduma za matibabu.Ugonjwa wake unatumia garama kubwa sana nadhani hilo ndo lilichangia watu wa bima kuniita.
Nimeitwa nikaambiwa wamechunguza nakugundua kuwa nina ndoa ya kanisani ambayo haijavunjwa na ndoa hiyo ni ya mke mmoja hivyo hii ndoa ya pili ni batili na nimefunga kwa malengo ya kunufaika na bima.
Nimejaribu kuwaelewesha kuwa ndoa ya kwanza imebaki tu kwenye cheti ila hawajataka kuelewa hadi niwaoneshe hati ya talaka.
Mwisho wamenambia watanitumia utaratibu wakulipa gharama zote zilizotumiwa na huyu mwanamke ambazo sio chini ya milioni10.Pamoja na hilo wamesema watafungia kadi za wategemezi wangu wote ikiwemo mimi mwenyewe hadi hilo deni ltakapolipwa lote ndo watazifungulia isipokuwa ile ya mke.
Wamesema nikishindwa kulipa shauri hili litaenda kwa mwajiri na hatimaye mahakamani.
Hapa nilipo napata shida kwani pamoja na kulipa hilo deni bado natakiwa kugharamia matibabu ya mke kwa cash kwani bado hajapona.

Wakuu,kama kuna namna naweza kutoka kwenye hili nisaidieni, ila kama haiwezekani napenda kuwashauri kuwa kilichonipata kikawe funzo kwa kila mwenye kesi inayofanana nahii ya kwangu.
Mimi najiuliza iliwezekana vipi kufunga ndoa nyingine ya kiserikal wakati bado hujavunja h
 
  • Thanks
Reactions: Nus
Kubali wakupeleke mahakamani ukiwa na ndoa ya kanisani ni ruksa kufunga ndoa nyingine ya serikali labda zote zingekuwa za kanisani ndio kosa.
Kwanini wanakuzuia kuongeza mke wakati wewe umeshahasi dini?
Ingewaambia umeachana na kanisa imerudia dini ya asili na kuongeza mke unao wawili sasa simple tu nenda mahakamani.
Alafu utawadai na fidia ya kufunga kadi zako aaah aaah aaah unakuwa milionea
Mkuu, huwezi kufunga ndoa nyingine ilihali una ndoa ya Kanisani. Ndoa zote ni za serikali,huko makanisani ni kama mawakala tu. Ila ukifunga ndoa haijalishi umefunga wapi, ni ndoa ya kiserikali maana serikali ndo inatoa cheti. Usije kumwambia mtu anaweza funga ndoa nyingine juu ya ndoa ya Kanisani,atalizwaa.
 
Sijatumia njia ya mkato mkuu. Hata yule afisa wa bima nilimuuliza kuwa kwanini cheti changu kilionesha wazi ni ndoa ya wake wengi ila hawakuniuliza kuhusu hilo? Wakakazia tu kuwa nina makosa
Shida mkuu ni kwamba tayari ulikuwa na ndoa ya Kanisani ambayo inajulikana ni ndoa ya mke mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: Nus
Ndo huwa nawaza hawa bima ya afya hawapo kiafya isipokuwa afya ni mgongo wa kukusanya hela za masikini tu. Kama mke wa kwanza si mnufaika wa bima inakuaje mke mnufaika wamtilie shaka? Sela zao ni mke mmoja wa ndoa sasa huyu mwingine yeye anawahusu nini wakati hayupo kwenye bima.

Wameona gharama zimekuwa kubwa kiasi upigaji unapungua hivyo wakafukua makaburi ili tu wakukomeshe upigaji wao uendelee kama kawaida. Najiuliza kina watu toka wapate bima ya afya utakuta miaka kumi au zaidi inakata bila hata kuhudhuria hospitali ya wilaya mbona hawawaiti ili angalau wapewe kamisheni kwa kuwa wanakatwa ila gharama zao hawazitumii?
Ndio maana nimemwambia wampeleke mahakamani anatoboa hii kwasababu mke wa kwanza sio mnufaika wa bima ,wenyewe wanamzuiaje kuongeza mke ?
 
Mimi najiuliza iliwezekana vipi kufunga ndoa nyingine ya kiserikal wakati bado hujavunja h
Watu wengine wanahama Kanisa wanaenda kufunga ndoa Kanisa jingine, ikitokea jambo kama hili ndo wanashangaa kumbe ilihitajika talaka kwa ajili ya ndoa ya kwanza.
 
Hawakugundua na cheti kilitaja wazi kuwa ni ndoa ya wake wengi. Hata wale walionifungisha ndoa sijui walipitiwaje wakati hata kwenye tangazo la ndoa niliandika nindoa ya wake wengi

Sijatumia njia ya mkato mkuu. Hata yule afisa wa bima nilimuuliza kuwa kwanini cheti changu kilionesha wazi ni ndoa ya wake wengi ila hawakuniuliza kuhusu hilo? Wakakazia tu kuwa nina makosa
Zingatia ushauri wa kanulege. Nakuwa nahisia za upigaji iwapo utakaa kizembe. Kama ni kosa kweli kisheria usingeitwa Private mngeonana kwa pilato. Sasa huo utaratibu utakaopewa eti ulipe hizo gharama unatoka wapi. Toka lini serikali ikafanya negotiations na mvuja sheria. Kama upo vizuri tafuta mwanasheria akusaide na ukiwashinda wakulioe fidia ya kusimamisha huduma
 
Ndio maana nimemwambia wampeleke mahakamani anatoboa hii kwasababu mke wa kwanza sio mnufaika wa bima ,wenyewe wanamzuiaje kuongeza mke ?
Hawamzuii kuongeza mke, cheti chake cha ndoa ya Kanisani ndo kinamzuia kuongeza mke. So hapo kafanya kuidanganya bima kwamba huyu ni mke wake wakati ni ndoa batili.
 
Mkuu, huwezi kufunga ndoa nyingine ilihali una ndoa ya Kanisani. Ndoa zote ni za serikali,huko makanisani ni kama mawakala tu. Ila ukifunga ndoa haijalishi umefunga wapi, ni ndoa ya kiserikali maana serikali ndo inatoa cheti. Usije kumwambia mtu anaweza funga ndoa nyingine juu ya ndoa ya Kanisani,atalizwaa.
Kanisa ndio haliwezi kufungisha ndoa mbili lakini serikali hata ndoa kumi linakupa cheti .
Huyo ameshaasi kanisa tayari ruksa kuwa na wake wengi tu ndoa za serikali anapiga hata 20
 
  • Thanks
Reactions: Nus
sijui mambo ya sheria ila nimegundua tu mtoa mada una roho nzuri. Mungu amponye mkeo na akufanyie wepesi kwenye hili la bima. wadau wametoa mawazo mazuri ni imani yangu mwisho wa siku kila kitu kitakuwa sawa.
 
Kama ulichoandika ndicho ukweli wenyewe hapa NHIF wamejipachika kazi isiyokuwa yao, wewe haujafoji cheti una ndoa halali kisheria, hizi dosari zako zingine haziwahusu.

Lakini hiki unachokieleza hapa kinakataa kuniingia akilini kazi ya NHIF ni verification tu ya majina.

Mimi Mzee wangu kabla ya kufariki nilimuombea kwenye bima yangu kulikuwa na shida ya majina sisi kwetu tuna majina mawili mawili karibu kila mtu sasa kukawa na complication ya majina nilipeleka hati ya kiapo cha mahakama tu kuthibitisha majina yangu.

Sasa hapa kwako sioni logic hili haliwahusu NHIF.
Nmimi niliwaambia mambo ya kuwa na ndoa mbili kanisa ndo lilitakiwa liniwajibishe ila nikaona mambo nimengi ngoja nikubaliane nao tu
 
Kanisa ndio haliwezi kufungisha ndoa mbili lakini serikali hata ndoa kumi linakupa cheti .
Huyo ameshaasi kanisa tayari ruksa kuwa na wake wengi tu ndoa za serikali anapiga hata 20
Wanataka hati ya talaka mkuu vinginevyo wanasema ndoa wanayoijua ni ie ya kwanza ambayo ni yamke mmoja
 
Zingatia ushauri wa kanulege. Nakuwa nahisia za upigaji iwapo utakaa kizembe. Kama ni kosa kweli kisheria usingeitwa Private mngeonana kwa pilato. Sasa huo utaratibu utakaopewa eti ulipe hizo gharama unatoka wapi. Toka lini serikali ikafanya negotiations na mvuja sheria. Kama upo vizuri tafuta mwanasheria akusaide na ukiwashinda wakulioe fidia ya kusimamisha huduma
Wewe unaposikia pre bargain huwa unaelewa nini?
 
sijui mambo ya sheria ila nimegundua tu mtoa mada una roho nzuri. Mungu amponye mkeo na akufanyie wepesi kwenye hili la bima. wadau wametoa mawazo mazuri ni imani yangu mwisho wa siku kila kitu kitakuwa sawa.
Shukrani san
 
Hawamzuii kuongeza mke, cheti chake cha ndoa ya Kanisani ndo kinamzuia kuongeza mke. So hapo kafanya kuidanganya bima kwamba huyu ni mke wake wakati ni ndoa batili.
Hakuna ndoa batili hapo labda vyote vingekuwa vya kanisa.
Labda alifunga ndoa kanisa A alafu akaenda tena kufunga kanisa B.
Lakini kama amefunga serikalini ni ruksa tu kanisa ndio haliwezi kufungisha ndoa juu ya ndoa.
 
Mimi najiuliza iliwezekana vipi kufunga ndoa nyingine ya kiserikal wakati bado hujavunja h
Inawezekana serikalini unaandikisha ndoa na kulipia, siku 21 ni za pingamizi kama lipo, kama hakuna pingamizi unafunga ndoa na mnapewa vyeti vyenu.

Kwahili NHIF wamejipachika kazi isiyo ya kwao, ingekuwa logic kama huyu mtu angekuwa ameshamuandika mke wa kwanza lakini hakuwahi kumuandika hili linawahusu vipi NHIF kwa mke wake mpya? Cheti cha ndoa ni fake?
 
  • Thanks
Reactions: Nus
Back
Top Bottom