Hata mimi binafsi sioni mantiki ya Bima kumlipisha gharama za matibabu na ingali mke wake wa kwanza hakuwa mnufaika kabisa wa Bima.Kama ulichoandika ndicho ukweli wenyewe hapa NHIF wamejipachika kazi isiyokuwa yao, wewe haujafoji cheti una ndoa halali kisheria, hizi dosari zako zingine haziwahusu.
Lakini hiki unachokieleza hapa kinakataa kuniingia akilini kazi ya NHIF ni verification tu ya majina.
Mimi Mzee wangu kabla ya kufariki nilimuombea kwenye bima yangu kulikuwa na shida ya majina sisi kwetu tuna majina mawili mawili karibu kila mtu sasa kukawa na complication ya majina nilipeleka hati ya kiapo cha mahakama tu kuthibitisha majina yangu.
Sasa hapa kwako sioni logic hili haliwahusu NHIF.
Ningeona foul kama mke wa kwanza angekuwa mnufaika. Hapa tatizo ni la Bima wanaona gharama wamefukua cheti cha jamaa RITA wakakuta ana cheti cha ndoa ya mwanzo.
Sasa hapo akipata divorce yake akapeleka Bima watakubali huyu mke mpya apate huduma?