Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Kubali wakupeleke mahakamani ukiwa na ndoa ya kanisani ni ruksa kufunga ndoa nyingine ya serikali labda zote zingekuwa za kanisani ndio kosa.
Kwanini wanakuzuia kuongeza mke wakati wewe umeshahasi dini?
Ingewaambia umeachana na kanisa imerudia dini ya asili na kuongeza mke unao wawili sasa simple tu nenda mahakamani.
Alafu utawadai na fidia ya kufunga kadi zako aaah aaah aaah unakuwa milionea
Cheti cha ndoa kwa sasa ni kimoja tu na kinatambulika na serikali, kwa hiyo ndoa ya kwanza kama alijaza ni ndoa ya mke mmoja bado tatizo lipo.
 
Ndio maana nimemwambia wampeleke mahakamani anatoboa hii kwasababu mke wa kwanza sio mnufaika wa bima ,wenyewe wanamzuiaje kuongeza mke ?
Wao watajuaje si mnufaika wakati hajapeleka vithibitisho? Je kama bima anayo lkn hajaumwa zaidi ya miaka kadhaa kuna ulazima aumwe ili ionekane active? Kuna bima permanent na hizi za kulipia kwa mwaka.

Bora ingekuwa bima ya kulipia kwa mwaka moja kwa moja baada ya kutolipia ingekuwa inactive ila hiyo ni permanent na zinakuwa zaidi kwa watumishi wa serikali.
 
Blaza mbona unapandisha sukari 😄😄😄😄😁

WAZUNGU AU NYIE ELITES MTUSAIDIE TU HAKUNA NAMNA.BABU ZAO HAO WAZUNGU WAMEIBA MALI NYINGI SANA HUKU AFRIKA.

INFACT HAMTUSAIDII KITU MNARUDISHA WHAT YOU STOLE FROM AFRIKA.AM PRETTY SURE MNARUDISHA THUMNI YA MLICHOKIIBA.

ANYWAYS,NAONA UMEUKANA NA UTANZANIA WAKO.

NIKUHAKIKISHIE TU NIKIJA HUKO STATES NTAISHI KULINGANA NA MIFUMO.ILA HUKU BONGO LAND TUMEFUNDISHWA KUISHA KULINGANA NA SITUATION/MAZINGIRA.

KIRANGA MSOMI USITUCHUKIE SISI WALALAHOI WAZALENDO TULIOBAKI BONGO, NDIO SISI NI MASKINI ILA NDO HIVYO MKITUKIMBIA MKAACHA KUTUWEKEA MIFUMO SAHIHI MJUE TUTAWAFATA HUKOHUKO YUUUESS😁😁😁😁

#Ok labda nikudokezee tu,mimi ni muumini wa falsafa za NICOLLO MACHIAVELI na FRIEDRICH NIETZSCHE.Falsafa zao ni very practical kwenye hii dunia tambara bovu.
Ungekuwa muumini wa falsafa practical angalau ungetetea hata self interests zako.

Machiavelli na Nietzche wote walitetea mtu kutafuta self interests zake, wewe hata hujawaelewa unawataja majina tu.

Huelewi hata falsafa practical ni nini.
 
Hao NHIF walikuwa wanaangaika na nini kumtafuta mke wa kwanza ingali mleta mada hajapeleka document yoyote kumtambulisha?
Au waliona gharama zinakuwa kubwa za matibaki wakatafuta chaka la kujificha na kukatiza huduma kwa mwanachama wao?
Ndio maana namwambia aende mahakamani ili mahakama iamua kosa lake unaweza kukuta hapo mahakama ikasema alipe 1M tu au akapewa onyo na kuambiwa apeleke talaka kuliko hayo mamilioni angetafuta mwanasheria kwanza kwa ushauri kabla ya kuanza kulipa.
Hapo labda mke wake kama ni mwajiliwa aliwai kupeleka cheti cha ndoa yao kama wana watoto nae wananufaika na NHIF linaweza kuwa tatizo
Ni utaratibu wao wa mara kwa mara kufanya uhakiki wa wanufaika wa mfuko huo, nishawahi kufika hospitali kubwa pale dirishani mapokezi wanakuwepo wanahakiki kama ni mwanachama hai au sivyo ili kuondoa udanganyifu wowote ndani ya mfuko.

Kama kadi yako ina changamoto wana block na hautapata huduma mahali popote hadi ufanye uhakiki upya.

Wako makini kabisa katika hili.
 
Nini kinathibitisha ndoa?
Cheti cha serikali imekitoa unasema hawala?
Yeye amefunga ndoa za wake wengi serikalini ni ndoa halali hiyo .
Mwanzo alikuwa na ndoa ya kanisani baadae akaingia ndoa ya wake wengi ya serikali na wakati anafunga ndoa ya pili alisema tayari ana ndoa.
Jamaa ni milionea tayari kuna loophole ya kisheria.
Wewe anza kumuita kwa jina la Qnet.
GOOD MORNING MILIONI aaaah aaaah aaaah
Hakuna ndoa ya kanisani mkuu, ndoa zote ni za kiserikali, kanisani ni kuthibitisha tu uhalali wa ndoa hiyo kwa misingi ya dini uliyopo.
 
Uliambiwa mpk kifo kiwatenganishe nyie mkajiamulia mambo kuachana,hayo ni malipo ya kumpotezea mda mchungaji ,kila la heri ktk mapambano ya afya ya mke w serikali.
 
Hakuna ndoa ya kanisani mkuu, ndoa zote ni za kiserikali, kanisani ni kuthibitisha tu uhalali wa ndoa hiyo kwa misingi ya dini uliyopo.
Ndoa zote ni za serikali mkuu nakubali, nachomaanisha ndoa zinazofungiwa Kanisani ni ndoa za mke mmoja,huwezi funga ndoa nyingine bila kutoa talaka.
 
hivi kwani ukisema una wake wawili na ukaandaa makubalioano ya kisheria kati yako na bimkubwa kuwa mlikubaliana kuwa na ndoa za wake wengi( sijui atakubali?) kwani kutakuwa na shida gani huko bima? nahisi kama shida itaisha.

Mkuu,

1. Ndoa zonasajiliwa serikalini.

2. Unaposajili ndoa, kuna nafasi za kusajili ndoa tofauti. Kuna ndoa za namna tofauti, kuna ndoa ya mke mmoja kama hizo za kanisani, ambazo huwezi kuongeza mke mpaka utoe talaka (au ubadilishe ndoa kutoka ndoa ya mke mmoja kwenda ya wake wengi, ubadilishe na mkeo, kwa Sheria ya Ndoa, Cap 29). kuna ndoa ya mke mmoja ambayo unaweza kuongeza mke, na kuna ndoa ya wake wengi, mitala.

3. Ndoa ya Kikristo ya Kanisani ikiyisajikiwa kama ndoa ya mke mmoja haibadilishiki kutoka ndoa ya mke mmoja kuwa ya wake wengi

4. Sasa, ukishasajiki ndoa kama ya mke mmoja ambayo haiwezi kuongeza mke, huwezi kukubaliana na mke wako muongeze mke mwingine hapo, kwa sababu ndoa yenu ikivyosajikiwa haikuwa hivyo.

5. Unauliza swali la kufikirisha sana. Kwani ukikubaliana na mkeo wa kwanza mbadilishe ndoa hapo, iweze kuwa ya wake wengi, kitakuwa na shida kwenye bima?

Kwanza kabisa, kwa muda ambao wanandoa ni Wakristo, ndoa ya Kikristo haibadilishiki kutoka ndoa ya mke mmoja kuwa ya wake wengi. Hii ni kisheria.

Kwenye swali lako.Shida itakuwapo.

Kwanza swali lako lina sehemu mbili.

A) Ukubaliane na mkeo wa kwanza kuonesha kuwa mlikubaliana naye mke wa pili aongezwe, kabla hujaoa. Hapa mnachokubaliana si muhinu, muhimu ni usajili wa ndoa yenu ya kwanza serikalini, ndoa hii haikusajiliwa kama ndoa ya wake wengi, kwa hivyo hayo makubaliano yenu, unless mlikuwa mmeyafanya kimahakama na kupangua usajili wa awali wa ndoa, yatakuwa batili.

B) Kukubaliana na mkeo wa kwanza kuwa muongeze mke wa pili baada ya kumuoa mke wa pili ni tatizo kubwa zaidi. Kwa sababu hapo umeoa kinyume na usajili wa ndoa yako ya awali.

Kwa vyovyote vile, makubaliano yoyote uliyofikia na mkeo wa kwanza, yalitakiwa kuwekwa wazi kwenye maombi ya bima kuonesha una wake wawili, na kutoyaweka wazi makubaliano hayo awali kabisa kunaifanya ndoa ya pili kuwa batili kwenye mfumo wa bima.

Pengine bima ina application maalum kwa watu wenye wake wawiki, oengine unatakiw akulioa zaidi iki juwa katika nfumo huu, ukimuibgiza mke wa piki kinyemela umekiuka mfumo huu.

Kimsingi hapo inaonekana umeudanganya nfuno wa bima iki kumpa mke wako wa piki nafasi katika nfumo ambao unakuruhusu kumpa nafasi mke mmoja.

Kuna watu wanaweza hata kusema hiki jambo kinaweza kutumika kufanya ndoa za nchongo kwa watu wanaohitaji huduma za bima ambao hawana bima tu.

Kwenye sheria kuna kanuni moja kubwa sana inayopinga retrospective laws na retrospective processes.

Retrospective provmcesses hapa ni jambo ambalo linafanyika leo ili kutatua wajibu wa kisheria uliokuwapo jana.

Yani ni hivi, kama mke wa pili alikuwa batili jana kwa sababu mke wa kwanza alikuwa hajaachwa, au hajakubali, au taarifa kamili zilikuwa hazijawakilishwa kwenye mfumo wa bima, kurekebisha tatizo hilo kwa kumpa talaka mke wa kwanza, kwa kuifuta ndoa ya kwanza, au kwa kumfanya mke wa kwanza akubali ndoa ya wake wengi, hakuondoi tatizo.

Kwa sababu tatizo ni kwamba, wakati mke wa pili anaingizwa kwenye bima, wakati mke wa pili anatumia bima, mke wa kwanza alikimuwa bado ameolewa na hivyo kwa provess aliyoifanya mwamba kum qualify mke wa pili kama mke pekee, hapo kulikiwa na kosa ambalo kimfumo linagambulika kama insurance fraud, hata kama mume alifanya hivyo bila kujua tu.
 
hivi kwani ukisema una wake wawili na ukaandaa makubalioano ya kisheria kati yako na bimkubwa kuwa mlikubaliana kuwa na ndoa za wake wengi( sijui atakubali?) kwani kutakuwa na shida gani huko bima? nahisi kama shida itaisha.
Walikubaliana vipi kuwa na ndoa ya wake wengi wakati ndoa yao walifunga Kanisani mkuu?. Kama hayo makubaliano yangekuwepo wangetakiwa kufunga ndoa ya wake wengi bomani au kimila sio kwenda Kanisani. Ukifungia Kanisani maana yake ni ndoa ya mke mmoja pekee..
 
Inawezekana serikalini unaandikisha ndoa na kulipia, siku 21 ni za pingamizi kama lipo, kama hakuna pingamizi unafunga ndoa na mnapewa vyeti vyenu.

Kwahili NHIF wamejipachika kazi isiyo ya kwao, ingekuwa logic kama huyu mtu angekuwa ameshamuandika mke wa kwanza lakini hakuwahi kumuandika hili linawahusu vipi NHIF kwa mke wake mpya? Cheti cha ndoa ni fake?
Asante sana, mimi sio mtumishi wa serikal ila nina kesi kama hiyo hapo ngoja nikafunge ndoa.
 
Ungekuwa muumini wa falsafa practical angalau ungetetea hata self interests zako.

Machiavelli na Nietzche wote walitetea mtu kutafuta self interests zake, wewe hata hujawaelewa unawataja majina tu.

Huelewi hata falsafa practical ni nini.
Aise wewe jamaa unastress na unatatizo la kisaikolojia linaitwa GRANDIOSE DELUSIONS😄😄😄.Ulisoma ila hukuelimika bure kabisa.

MZEE WA LOGICAL FALLACIES ITAKUWA HUKO UNABEBA SANA BOX.RUDI NYUMBANI KAMA HUKO U.S.A PANAZIDI KUKUCHANGANYA.
 
Umeacha kujadili hoja kwamba hukuwaelewa Machiavelli na Nietzsche, unanijadili mimi kwa kunishambulia kwa logical fallacy.

You can't focus.

Hujui kuwa hiyo kunishambukia mimi badala ya kujadili hoja nayo ni logical fallacy.

Ad hominem logical fallacy.
 
Mkuu kuwa mzalendo achana na rushwa lipa hicho kiasi walichokuambia, waombe wakupe control number ya malipo ulipie.

Pia watu wasikudanganye kwamba mahakamani utatoboa ni waongo hautotoboa. Ninaongea kutokana uzoefu nimefanya sheria katika sheria za ndoa na familia. Naongea kama wakili huwezi ukafunga ndoa ya serikali juu ya ndoa ya kanisani never. Ni kweli vyeti vyote vinatoka serikalini lakini kwenye sheria ya ndoa type of marriage ceremony ina determine aina ya ndoa unayofunga. Ukifunga ndoa ya msikitini cheti cha ndoa utakachopewa kinaonesha kuwa hiyo ni ndoa ya wake wengi hivyo sheikh ataenda rita kusajili cheti chako kama ndoa ya wake wengi. Ukifunga kanisani padri au mchungaji atasaini kwenye cheti chako kuwa ni ndoa ya mke mmoja hata rita kitasajiliwa hivyo. Kinachotokea ni kwamba kwa vile cheti chako ni cha mke mmoja mke mwingine yeyote utakayeoa bila kumwacha wa kwanza atakuwa batili chini ya sheria.

Tunasema ndoa nyingine yoyote itakuwa batili kwa sababu kisheria kwa kuwa na ndoa ya mke mmoja umezuiwa (barred) kuoa mke mwingine. Kisheria inaitwa capacity to marriage, ili ufunge ndoa ni lazima uwe na capacity to marriage vitu vinavuoathiri capacity ni
1. Age, ukiwa chini ya miaka 18 (kwa sheria ya sasa huna sifa ya kuingia kwenye ndoa.
2. Sound mind, lazima uwe na akili timamu.
3. Subsisting marriage for christians. Kwa mkristo kama una ndoa ya mke mmoja huruhusiwi kuingia kwenye ndoa nyingine.
Pia hii subsisting marriage inaapply pia kwa wanawake wa kiislamu maana nao hawaruhusiwi kuwa na wanaume wengi.

Swala la mwisho NHIF wapo sahihi kabisa kuhakiki taarifa zako na ni jukumu lao kujiridhisha juu ya ndoa zako. Kwanini ionekane siyo kazi yao kujiridhisha na taarifa za wateja wao? Je mwanamke akipeleka vyeti vya ndoa ameolewa na wanaume watano wakijiridhisha itakuwa kosa? Je wanapojiridhisha kuhusu majina, vyeti vya kuzaliwa vya wategemezi etc wanapata wapi mamlaka? Siku hizi mifumo inasomana it means ukisubmit cheti chako cha ndoa wanaingiza majina yenu kwenye mfumo wa rita wanakutana na idadi zako za ndoa.

Mwisho: Walipe fidia yao, nhif ni yetu sote huu mfuko ukishindwa kujiendesha ukafa tutakaoumia ni sisi na tutaanza kulaumu.
 
Nini kinathibitisha ndoa?
Cheti cha serikali imekitoa unasema hawala?
Yeye amefunga ndoa za wake wengi serikalini ni ndoa halali hiyo .
Mwanzo alikuwa na ndoa ya kanisani baadae akaingia ndoa ya wake wengi ya serikali na wakati anafunga ndoa ya pili alisema tayari ana ndoa.
Jamaa ni milionea tayari kuna loophole ya kisheria.
Wewe anza kumuita kwa jina la Qnet.
GOOD MORNING MILIONI aaaah aaaah aaaah
Hicho cheti chenyewe cha ndoa cha serikali amekipata kwa udanganyifu kwa sababu hakuna afisa wa serikali nchi hii mwenye akili timamu anayeweza akakubali kukufungisha ndoa nyingine huku akiwa anajua kuwa una ndoa nyingine ya kanisani ambayo haijavunjwa. Wafungisha ndoa kule bomani wanajua kuwa ndoa ya kanisani ni mke mmoja mume mmoja, kwahiyo kama wametoa cheti ni kwa sababu hajawaambia ukweli. Kwamba aliwadanganya hiyo haina mjadala kwa sababu lengo la kutangaza siku 21 ni ili kama kuna mwanandoa mwingine alete pingamizi. Na kama hakumdanganya basi alimpa rushwa. Sote tupo mitaani tunafahamu watu wakiwa desperate na cheti cha ndoa huwa wanahonga anapewa cheti within a minute bila hata kutangazwa siku 21 sasa ndoa ya hivyo ni halali kwa sababu ya cheti? Watanzania tunapenda sana kuvunja sheria ni mpaka mambo yatubadilikie kama hivi ndiyo tunaamka
 
Mkuu kuwa mzalendo achana na rushwa lipa hicho kiasi walichokuambia, waombe wakupe control number ya malipo ulipie.

Pia watu wasikudanganye kwamba mahakamani utatoboa ni waongo hautotoboa. Ninaongea kutokana uzoefu nimefanya sheria katika sheria za ndoa na familia. Naongea kama wakili huwezi ukafunga ndoa ya serikali juu ya ndoa ya kanisani never. Ni kweli vyeti vyote vinatoka serikalini lakini kwenye sheria ya ndoa type of marriage ceremony ina determine aina ya ndoa unayofunga. Ukifunga ndoa ya msikitini cheti cha ndoa utakachopewa kinaonesha kuwa hiyo ni ndoa ya wake wengi hivyo sheikh ataenda rita kusajili cheti chako kama ndoa ya wake wengi. Ukifunga kanisani padri au mchungaji atasaini kwenye cheti chako kuwa ni ndoa ya mke mmoja hata rita kitasajiliwa hivyo. Kinachotokea ni kwamba kwa vile cheti chako ni cha mke mmoja mke mwingine yeyote utakayeoa bila kumwacha wa kwanza atakuwa batili chini ya sheria.

Tunasema ndoa nyingine yoyote itakuwa batili kwa sababu kisheria kwa kuwa na ndoa ya mke mmoja umezuiwa (barred) kuoa mke mwingine. Kisheria inaitwa capacity to marriage, ili ufunge ndoa ni lazima uwe na capacity to marriage vitu vinavuoathiri capacity ni
1. Age, ukiwa chini ya miaka 18 (kwa sheria ya sasa huna sifa ya kuingia kwenye ndoa.
2. Sound mind, lazima uwe na akili timamu.
3. Subsisting marriage for christians. Kwa mkristo kama una ndoa ya mke mmoja huruhusiwi kuingia kwenye ndoa nyingine.
Pia hii subsisting marriage inaapply pia kwa wanawake wa kiislamu maana nao hawaruhusiwi kuwa na wanaume wengi.

Swala la mwisho NHIF wapo sahihi kabisa kuhakiki taarifa zako na ni jukumu lao kujiridhisha juu ya ndoa zako. Kwanini ionekane siyo kazi yao kujiridhisha na taarifa za wateja wao? Je mwanamke akipeleka vyeti vya ndoa ameolewa na wanaume watano wakijiridhisha itakuwa kosa? Je wanapojiridhisha kuhusu majina, vyeti vya kuzaliwa vya wategemezi etc wanapata wapi mamlaka? Siku hizi mifumo inasomana it means ukisubmit cheti chako cha ndoa wanaingiza majina yenu kwenye mfumo wa rita wanakutana na idadi zako za ndoa.

Mwisho: Walipe fidia yao, nhif ni yetu sote huu mfuko ukishindwa kujiendesha ukafa tutakaoumia ni sisi na tutaanza kulaumu.
Wewe ni Wakili? Tafadhali usichafuwe taaluma za watu.

Hakuna Wakili mwenye mwandiko kama wako kama kanya bata.

Heshimu taaluma za watu usiwapake matope.

Moja ya sifa ya Wanasheria ni kujuwa kuandika vizuri.
 
Back
Top Bottom