Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Wanataka hati ya talaka mkuu vinginevyo wanasema ndoa wanayoijua ni ie ya kwanza ambayo ni yamke mmoja
Mahakama itaamua wenyewe wanaijuaje wakati haujawapelekea cheti cha ndoa ya kwanza?
Kwahiyo kama mtu alifunga ndoa ya jadi ya kwanza baadae akafunga ndoa nyingine ya serikali akapeleka cheti nae huyu watamwambia wanatambua ndoa ya jadi ?
Hao wamejichanganya kwako wapeleke kwa pilato naiona pesa ndefu ya fidia unakula hapo wewe ni milionea mtarajiwa aaah aaah aaah
 
Pole sana bro, kuna kipindi nilikuwa kama wewe nahubiri haki natenda haki.Ila mwisho wa siku haki haipo duniani.

Pesa(grisi) ndio kila kitu na apenyezae rupia mambo yake mukide ila wapenda haki kama TAL wapo jela wananyea debe na dunia yote ipo kimya watu wanaendesha magari ya mamillioni na mabillioni katika nchi maskini isiyo na msaada kwa walahoi huku huduma za msingi bado ikionekana kama anasa.

The fact jamaa anataka kutoka kwenye hicho kitendawili mimi nimempa uhalisia wa ground na wa hapo nyumbani Tz.

The system is wrecked, no way out but just do anything to survive.

Mkali wa FACT na FALSAFA UTANIWIA RADHI.BONGO KWA SASA TUPO KWENYE SURVIVAL MODE!!!

Hujaelew hoja. Hata tukiondoa haki na kuongelea self interests za watu na surival mode, ushauri wako hauna mantiki.

Kila mtu ana uwezo wa kuboresha mfumo uliovunjika. Hata nchi ambazo mifumo hii inafanya kazi vizuri hazikuanza hivyo, ni watu wamechukua ownership ya mifumo na kuiboresha, wanaheshimu sheria, na mpaka leo wanailinda mifumo.

Yani hapa ilitakiwa mtu akiongelea kutoa rushwa ili asilipe anachotakiwa kulipa, watu wamshambulie, kwa sababu anawaibia wao. Hizi resources za bima ni watu wanachangia.

Sasa huko kwetu watu mnaochangia ndiyo kwanza mnafundishana kutoa rushwa ku abuse mnachochangia, hamjielewi.

This is the tragedy of the commons on steroids.

Nyie huko wananchi wenyewe mnaotumia mifumo mnafundishana kutumia rushwa kuharibu mifumo.

Kumpa mtu ushauri wa kutoa rushwa badala ya kulipa anachotakiwa kulipa kunauharibu mfumo wote, kunakuharibia hata wewe mwananchi mwingine.

Hili suala hata mtu akisema hataki haki anataka kuweka mbele self interests zake tu, ushauri wako ni mbovu.
 
Mahakama wanaweza kupata taarifa za ndoa ya kwanza maana zipo RITA, mbona NHIF wamepata ilihali hakuwaambia?.
Pili ingekuwa ndoa ya jadi isingekuwa shida maana inajulikana ni ndoa ya wake wengi, ndoa ya Kanisani inajulikana ni ya mke mmoja pekee. Huwezi kufunga ndoa moja juu ya ndoa nyingine ya Kanisani.
 
Wabongo wengi kama wewe ni watu wa kupenda rushwa, hata katika jambo linalowaumiza wao.

Rushwa imekuwa ni kama mfumo wa maisha tu. Na jambo la umma linaonekana kama jambo lisilo na mwenyewe.

Yani unamshauri kabisa mtu akatoe rushwa kwenye jambo ambalo ame abuse mfumo wa bima kwa ujinga wake, kwa namna ambayo inawaharibia watuniaji wengine wa mfumo huo.

Ndiyo maana mifumo hii inashindwa kufanya kazi.

Jamii nzima inakubali rushwa na njia za mkato. Wewe hata huoni aibu kuandika ushauri wa kumaliza suala hili kwa rushwa.

Huyu mwingine OP naye anaoa oa tu, hata haachi, hata hajui maana ya kuoa bila kuacha ni nini.

You can't be serious.
Mkuu mimi kulileta humu nikwasababu niliongea na wahusika na tukakubaliana kuwa nilikosea kutokuwa na talaka hivyo nitawajibika.Mwisho wa andiko langu nilishauri wenzangu wenye kesi kama yangu wajifunze. Sikutaka shortcut zaidi yakutekeleza maelekezo ya bima
 
Pole sana bro, kuna kipindi nilikuwa kama wewe nahubiri haki natenda haki.Ila mwisho wa siku haki haipo duniani.

Pesa(grisi) ndio kila kitu na apenyezae rupia mambo yake mukide ila wapenda haki kama TAL wapo jela wananyea debe na dunia yote ipo kimya watu wanaendesha magari ya mamillioni na mabillioni katika nchi maskini isiyo na msaada kwa walahoi huku huduma za msingi bado ikionekana kama anasa.

The fact jamaa anataka kutoka kwenye hicho kitendawili mimi nimempa uhalisia wa ground na wa hapo nyumbani Tz.

The system is wrecked, no way out but just do anything to survive.

Mkali wa FACT na FALSAFA UTANIWIA RADHI.BONGO KWA SASA TUPO KWENYE SURVIVAL MODE!!!
Kiranga anaishi kwenye mfumo ambao kila mtu anafuata sheria tofauti na Bongo hali halisi haiko hivyo.

Sidhani kama Marekani akisimamishwa na traffic atatowa dollar 50 kumpa ya soft drink, lakini akiwa Bongo akisimamishwa na traffic mwenyewe atatowa mwekundu wa Msimbazi hiyo ni fact.
 
Hata mimi binafsi sioni mantiki ya Bima kumlipisha gharama za matibabu na ingali mke wake wa kwanza hakuwa mnufaika kabisa wa Bima.

Ningeona foul kama mke wa kwanza angekuwa mnufaika. Hapa tatizo ni la Bima wanaona gharama wamefukua cheti cha jamaa RITA wakakuta ana cheti cha ndoa ya mwanzo.

Sasa hapo akipata divorce yake akapeleka Bima watakubali huyu mke mpya apate huduma?
Muda kama huu ilibidi jamaa akae karibu sana jf kwasababu yawezekana humuhumu jf kuna maafisa wa NHIF Kama hajapewa hati ya maandishi ya kudaiwa hiyo pesa , anaweza kuiomba ikiwa na muongozo wa kifungu cha sheria then aconsult na mwanasheria kwa ufafanuzi. Faini huwa haizidi 1M

Mimi Pdf ya NHIF ninayo labda kama hiyo sheria ipo kwenye policy wording.
 
Mkuu walikupa hati ya maandishi inayoeleza kifungu cha sheria kuhusu hiyo penalty au maelezo ya mdomo?
Pale
Pole sana mkuu.Hilo limetufundisha wote kwamba,mambo ya kiofisi,hasahasa serikali,huendeshwa kwa taarifa rasmi kimaandishi/documents halali.Haukuachana na mkeo kiofisi rasmi/talaka mkononi.Kosa kubwa sana.
NB:Kuna mkono wa shetani katika hilo shauri lako hadi watu wa NHIF wakafuatilia na kutafuta kwa kukugonga nyundo za utosi.Narudia tena,pole sana mkuu.Mara nyingine kuwa makini na ucheze kwa steps!Sasa baada ya hapo yule mke wa kwanza inakaaje?
Mke wa kwanza hana shida yoyote kwenye hili. Anaendelea na maisha yake na wala hasumbui kwa chchote
 
Mkuu mimi kulileta humu nikwasababu niliongea na wahusika na tukakubaliana kuwa nilikosea kutokuwa na talaka hivyo nitawajibika.Mwisho wa andiko langu nilishauri wenzangu wenye kesi kama yangu wajifunze. Sikutaka shortcut zaidi yakutekeleza maelekezo ya bima
Mkuu,

Kwenye hili la kulaumu wanaopenda shortcut hili hata si lako, nilikuwa nalaumu wanaokushauri utoe rushwa.

Najua wanaweza kujiona kama wanakuonea huruma, lakini kama kweli wanakuonea huruma wakuchangie tu hiyo milioni 10 utakazoshindwa kulipa.

Vinginevyo hapo kushauri utoe rushwa ni kushauri mtu a abuse the system.
 
Mkuu,

Kwenye hiki la kulaumu wanaooenda shortcut hili hata si lako, nilikuwa nalaumu wanaokushauri utie rushwa.

Najua wanaweza kujiona kama wanakuonea huruma, lakini kama kweli wanakuonea huruma wakuchangie tu hiyo milioni 10 utakazoshindwa kulipa.

Vinginevyo hapo kushauri utoe rushwa ni kushauri mtu a abuse the system.
Kumbuka huyu jamaa ni mwachama wa NHIF anayakatwa michango yake kila mwezi.

Scenario nzima ya hili tukio hakuna intention yoyote ya udanganyifu ni lack of proper information hakuna elimu kwa umma.
Si kila kosa ni la kumuadhibu mtu hata makosa ya barabarani traffic Wastaarabu anakueleza tu bila kukupiga ticket wala kuomba rushwa.

Hizi ofisi za umma zinahitaji watu wenye utu haya majinga ya NHIF hayana utu utadhani basi hakuna majizi humo yanavyojifanya yamenyooka ujinga mtupu.
 
Kiranga anaishi kwenye mfumo ambao kila mtu anafuata sheria tofauti na Bongo hali halisi haiko hivyo.

Sidhani kama Marekani akisimamishwa na traffic atatowa dollar 50 kumpa ya soft drink, lakini akiwa Bongo akisimamishwa na traffic mwenyewe atatowa mwekundu wa Msimbazi hiyo ni fact.
😄😄😄huu ndio uhalisia wenyewe mazingira yetu kivyetuvyetu tunasolve mambo namna hiyo hata kama hutaki mazingira yanakufosi.

Imagine jamaa akilipa hiyo M10 alafu hao maofisa wakalipana posho sisi ngumbaru dawa bado tunaaambiwa haitoki kwa bima lakini pia ukienda hospitali kama Mloganzira unaambiwa ukafate rufaa hospitali za pembezoni.Tofauti na hapo unaambiwa ulipie cash.Gademit jamaa alainishe tu vyuma kwa GRISI!!!

Yaani kwa mazingira ya Bongo bora ufanye linalowezekana, huku bado sana kustaarabika. Tunaishi kusogeza siku.
 
Pale

Mke wa kwanza hana shida yoyote kwenye hili. Anaendelea na maisha yake na wala hasumbui kwa chchote
Ni maelezo ya mdomo au ni ya maandishi, mkuu haya ni mambo ya kisheria hayawezi kwenda kienyeji.
 
Mahakama wanaweza kupata taarifa za ndoa ya kwanza maana zipo RITA, mbona NHIF wamepata ilihali hakuwaambia?.
Pili ingekuwa ndoa ya jadi isingekuwa shida maana inajulikana ni ndoa ya wake wengi, ndoa ya Kanisani inajulikana ni ya mke mmoja pekee. Huwezi kufunga ndoa moja juu ya ndoa nyingine ya Kanisani.
Hao NHIF walikuwa wanaangaika na nini kumtafuta mke wa kwanza ingali mleta mada hajapeleka document yoyote kumtambulisha?
Au waliona gharama zinakuwa kubwa za matibaki wakatafuta chaka la kujificha na kukatiza huduma kwa mwanachama wao?
Ndio maana namwambia aende mahakamani ili mahakama iamua kosa lake unaweza kukuta hapo mahakama ikasema alipe 1M tu au akapewa onyo na kuambiwa apeleke talaka kuliko hayo mamilioni angetafuta mwanasheria kwanza kwa ushauri kabla ya kuanza kulipa.
Hapo labda mke wake kama ni mwajiliwa aliwai kupeleka cheti cha ndoa yao kama wana watoto nae wananufaika na NHIF linaweza kuwa tatizo
 
Hujaelew hoja. Hata tukiondoa haki na kuongelea self interests za watu na surival mode, ushauri wako hauna mantiki.

Kila mtu ana uwezo wa kuboresha mfumo uliovunjika. Hata nchi ambazo mifumo hii inafanya kazi vizuri hazikuanza hivyo, ni watu wamechukua ownership ya mifumo na kuiboresha, wanaheshimu sheria, na mpaka leo wanailinda mifumo.

Yani hapa ilitakiwa mtu akiongelea kutoa rushwa ili asilipe anachotakiwa kulipa, watu wamshambulie, kwa sababu anawaibia wao. Hizi resources za bima ni watu wanachangia.

Sasa huko kwetu watu mnaochangia ndiyo kwanza mnafundishana kutoa rushwa ku abuse mnachochangia, hamjielewi.

This is the tragedy of the commons on steroids.

Nyie huko wananchi wenyewe mnaotumia mifumo mnafundishana kutumia rushwa kuharibu mifumo.

Kumpa mtu ushauri wa kutoa rushwa badala ya kulipa anachotakiwa kulipa kunauharibu mfumo wote, kunakuharibia hata wewe mwananchi mwingine.

Hili suala hata mtu akisema hataki haki anataka kuweka mbele self interests zake tu, ushauri wako ni mbovu.
Nakuelewa but your American way of life does not apply even a little huku BANANA REPUPLIC!!!

Yeye kama ataamua kulipa hiyo M10 ni yeye ila haibadili chochote.Na wala haitamfanya yeye kupata chochote zaidi ya kuendelea kupoteza hela kwasababu hata baada ya malipo bado wamembania kumuunga na mfumo wa NHIF.

Hapo ndio uone system haipo kukusaidia hata ukicomply zaidi watazidi kukukanyagia.

Kwahiyo huku BANANA REPUBLIC lazima uwe na akili ya kusoma mazingira.Ukitia huruma nothing happens ukicheza michezo ya mjini walau you will save something. These wild dogs hawatakuzingatia,always jua you are the next on the menu!!!

Huyu jamaa ametafutiwa zengwe kutolewa kwenye mfumo kwakua wandewa wamebaini hayo matibabu yanawaingizia hasara badala ya faida.Keep this in mind Mr. MANTIKI!!
 
Kumbuka huyu jamaa ni mwachama wa NHIF anayakatwa michango yake kila mwezi.

Scenario nzima ya hili tukio hakuna intention yoyote ya udanganyifu ni lack of proper information hakuna elimu kwa umma.
Si kila kosa ni la kumuadhibu mtu hata makosa ya barabarani traffic Wastaarabu anakueleza tu bila kukupiga ticket wala kuomba rushwa.

Hizi ofisi za umma zinahitaji watu wenye utu haya majinga ya NHIF hayana utu utadhani basi hakuna majizi humo yanavyojifanya yamenyooka ujinga mtupu.
1. Sula la huyu jamaa ni mwanachama wa NHIF au si mwanachama halipo hapa, kwa sababu aliyetumia huduma si yeye, ni mke wake batili katika macho ya mfumo na sheria. Mke wake batili kwa muktadha huo hatambuliwi kuwa mnufaika halali wa mfumo. Kwa hiyo hoja ya huyu ni mwanachama wa NHIF haina mashiko hapa. Suala si uanachama wake, suala ni uhalali wa mke batili kuwa mnufaika wa bima kwa kupitia yeye.

2. Masuala ya intention ni magumu sana kuyajua vizuri, hususan yanapoletwa na upande mmoja, kwa maandishi, hapa JF.

Nataka kumuamini mtoa mada.
Inawezekana, kwa kiasi kikubwa kabisa, kwa kuangalia mada ilivyoletwa, kiukweli tatizo ni ujinga tu, watu hawachukulii mambo seriously, wanaachana kiholela bila talaka, talaka ina finality fulani ambayo ni very emotional mtu anaweza akawa anaijua process in the abstract, ila anaipotezea tu kwa cognitive dissonance mbaya sana, utamaduni wa documents sio wetu kivile, haya yote naelewa.

Lakini inawezekana pia hili likawa si suala la ujinga tu. Hatujamsikia mke wa kwanza atupe upande mwingine kwa nini hakuachwa. Kuna mambo mengi hatuyajui.

Kwa hiyo, bila kutaka kumuhukumu OP ambaye kwa maandishi anaonekana mstaarabu kwa kukubali kosa na kutoa funzo kwa wengine, suala la intention ni gumu ndiyo maana kuondoa utata wake tunasema "ignorance of the law is no defense". Yani hata kama hukuwa na nia mbaya, umevunja sheria bado unatakiwa ulipe.

3. Mimi pia sipendi hukumu ya kuadhibu, punitive (kuna zile elements za hukumu, punitive, restorative, deterrent, incapacitation, rehabilitative ), kifalsafa.

Hapa naangalia zaidi restorative kuliko punitive. Naangalia kurudisha pesa kwenye mfumo zaidi ya kumuadhibu mtoa mada.

Adhabu mara nyingi, hususan kwenye mifumo yetu, inatokana na kisasi na sadism, na kisasi si haki. Sadism si haki. Hapa kinachotakiwa si adhabu punitive. Kinachotakiwa ni kurudisha kilichochukuliwa bila uhalali. Ndiyo maana sioni msisitizo kwenye kumfunga OP kama mtu aliyefanya insurance fraud. Kama tulivyoona hapo juu na kukubaliana, mifumo hii ni mipya kwetu, inawezekana elimu ni ndogo, inawezekana hatuna utamaduni wa ku formalize mambo kwa documentation tunaoa na kuacha kiholela tu. Kwa hiyo kulipa milioni 10 si adhabu punitive, ni kurudisha tu kilichochukuliwa bila uhalali. Ni kuhakikisha mfumo una integrity na hauwi abused hata ikiwa abuse ilitokea unintentionally.

4. Najua watu wengi wanashauri mambo mengi, mpaka rushwa, kama namna ya kumuhurumia mtoa mada. Lakini njia hizi zinaharibu integrity ya mfumo mzima wa bima. Kama watu kweli wanamuonea huruma mtoa mada, wamchangie pesa aongeze kulipa.

Suala hili la kumchangia mtia mada hutalisikia likitajwa kwa sababu watu wengi wanaweza kumuonea huruma kwa kumshauri atoe rushwa tu, lakini wengi hawawezi kumuonea huruma kwa kumchangia alipe.

Watu wanapenda shortcut.
 
Back
Top Bottom