Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Acha uvivu jaribu kushirikisha kichwa chako japo kidogo tu..... Watu wanaenda mikutanoni kusikiliza Sera za wagombea ili wafanye maamuzi vyema... Pale walikuwepo watu wa vyama tofauti kusikiliza Sera za ukawa unfortunately they were so disappointed.

Watu wengine kama huyu jamaa wanaenda kuangalia watu sio kusikiliza sera za wagombea ndio mana ukiwauliza wanataka nini watakujibu "MABADILIKO" hamna kitu kingne
 
kama unampenda mchukue ukanywe naye chai (by mwl. nyerere 1995).
hapa tunachugua kiongozi na sio mtu maarufu. elewa hilo.


 
Ukawa sometimes mpo kimzaa mwaka huu muamue kumpa Magufuri nyinyi wenyewe lakini siyo sisi wananchi. Msirudie tena ujinga wa jana. Mbowe unapwaya sana unaongelea mabadiliko bila uchambuzi.Mnashindwa kutambua hadhira ya vijana inataka nn! Hata Mwanza mlipwaya sana. Mbowe anaongea kwa sauti kubwa but no point. Watanzania wanataka point. Magufuri anapoint out! Come on dudes!
 

Huu uhuni wa LE kupewa dakika chache za kuongea na kudai ati muda hautoshi kwa upande wangu nimeustukia kipo tunachofichwa, wasifikiri wote mambumbumbu walijua kabisa watu wanakiu ya kumsikia akiongea kilichowafanya wampe muda mchache ni nini kama si uhuni? Narudia tena na tena hakuna kitu hapo, uhuni mtupu
 
Kulikuwa ma vichekesho...mabadiliko Lowassa Lowassa mabadiliko....nilitegemea mengi toka kwa mgombea wetu ambayo hatukuyapata tukaambiwe tukasome kwenye www..
 
Watu wengine kama huyu jamaa wanaenda kuangalia watu sio kusikiliza sera za wagombea ndio mana ukiwauliza wanataka nini watakujibu "MABADILIKO" hamna kitu kingne

Kwel kabisa mkuu watz tuna safari ndefu sana kuelekea kwenye maendeleo..... Wengi wanafuata mkumbo wako kama nyumbu hawajui watokako wala waelekeapo yaaan wapo wapo tu ili mradi.
 
Habari za Leo wanajamvi. Ni matumaini yangu kuwa jana mlifwatilia kwa ukaribu Sana mkutano Wa UKAWA pale jangwani. Je nini maoni yako kuhusu mkutano Wa Jana wa UKAWA?
Nilichobaini ni kuona chama kikubwa kama CDM kutumia masheikh na maaskofu uchwara na kuacha kutumia viongozi wa wa dini wenye maadili katika madhehebu yao. Mathalani nilishangazwa pale sheikh alipotoa dua kwamba "wazibe mkojo" pia ","wapate kansa ya damu" kwa hakika huu ni udhalilishwaji wa dini ya kiislam kwani ktk msaafu hakuna mahubiri kama hayo
 
MAFURIKO
Mi nafikiri huu msemo una maana kubwa sana, ni kweli wengi wamepitiwa na "mafuriko" hata hawajui yatafikisha wapi kama hujapelekwa mafuriko umeshajua tayari hakuna mabadilko kwa ukawa ya e.l
Siipendi ccm lakini sina namna Nisubiri chama cha upizani kingine sio hiki
 
Siasa ni kupigana zengwe.lakini lowasa alitaja vipaumbele vyake.watu wanataka nini??
 
Nimeipenda. Mkulima akikopesha marejesho na riba juu. Makufuli anatudanganya eti ni marufuku selikali kukopa kwa mkulima uongo mchana kweupe.
 
Kama muda ulikua hautoshi walmleta jukwaani Tambwe hiza wa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…