Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Uko sahihi hakukuwa na maana yoyote kuunganisha ule uzi ulioanzishwa na StandaloneSAA 6 usiku ambayo ni siku mpya ya tarehe 29-08-2015 wakiunganisha na ule wa maandalizi wa Jana tarehe 28-08-2015
Maudhui si ni yale yale au mnataka kujaza mauzi jamvini?
 
Manyunyu ya Mvua yaliyo nyunyiza asubihi ni baraka kutoka kwa Mungu kupunguza jua na vumbi jangwani kama enzi za wanaisrael waliposafiri kutoka Misri, leo hata helkopta au ndege zilizo chakaa za kivita zikifanya mazoezi jangwani haondoki mtu mpaka mwisho
Mvua iliyo anza kunyesha asubuhi ya leo mkoa wa Dar es salaam imeharibu mkutano wa UKAWA.
 
Poleni sana.
 
Jamani tuliopo Dar usafiri rahisi ni bodaboda, mimi nipepaki mkweche wangu nyumbani nimeita bodaboda baada ya dakika 25 nitakuwa viwanja vya jangwani nitatupiamo updates. Leo kwa wakazi Dar si ya kukaa nyumbani wala kutegemea runinga mambo ni live uso kwa uso.
 
Jumamosi ilopita malory yalikuwa yanaonekana yamejaza wapenzi wa ccm,na pia kwenye sheli bodaboda na magari walikuwa wanajaziwa mafuta bure,pia bila kusahau 5000/= leo vp?
 
Kwa tabia hii bila kujibu tuhuma za uuzwaji wa CHADEMA kwa Lowassa.
Watu tumepigwa tumeisapoti Dr Slaa kazunguka nchi nzima kutuhamasisha leo chama kinauzwa kirahisi bila maelezo.
Hii inadhihirisha na sisi wanachama tumeshauzwa

Magamba mtakoma mwaka huu. Chadema hatuna mwanachama wa sampuli yako maana hakuna mwanachama au mpenzi wa chadema aliyewahi kupigwa mabomu kwa ajili ya kumpigania mtu binafsi (Slaa au Mbowe au yeyote yule). Ila tumeshawahi kupigwa mabomu kwa ajili ya kutetea chama chetu (CDC) pamoja na Tanzania kwa ujumla ili ikombolewe kutoka kwenye utawala dhalimu wa magamba.
 
Hahahaaaaa ikifika saa kumi huu uzi utakua na mtu zaidi ya buku unusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…