Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

wakuu mlioko kwenye tukio tupien picha huku iringa taaaaaabu kweli umeme wamekata
 
Wanasubiri Uwanja ujae Mkuu, wasipomfunika Magufuli imekula kwao
 
Mnawatesa wananchi bure ghairisheni
Mkuu wanaowatesa wananchi ni CCM.wanabeba wananchi kwenye malori na mafuso ya kusafirishia mazao na nguruwe..halafu bado wananchi haohao wanaitwa malofa na wapumbavu..sasa hapo wanaowatesa wananchi ni UKAWA AU CCM?
 
Tunahitaji updates za mara kwa mara. Huyu kaanzisha thread amesepa....
 
Usiku kucha watu wanasafiri kuja Dar kutengeneza mafuriko. Hahahaha kweli watani zetu hawa wamekosa hoja wala Sera Bali wameamua mwaka huu kutuburudisha tu tukisubiri kuapishwa kwa Raisi Dr.John Pombe Magufuri
Hao wanaosafiri ni watanzania? Ni wapigakura?
Sasa kuna tatizo gani?
 
huu ni umbwiga mkubwa sana aiseee picha hakuna zaidi ya maneno tuuu.
 
Uwanja wa Jangwani hautatosha kwa shughuli ya leo......... Mungu anakwenda kudhihirisha uwongo na unafiki wa CCM.
 
Nyenyere

Tatizo lako ni kutojua agenda inayosimamiwa na Lowassa na UKAWA yake; agenda hapa ni rasimu ya Warioba ambayo ina kila kitu; ina dawa ya ufisadi, maadili ya uongozi, kibano cha mikataba feki, upotevu wa rasilimali, nk. tunajenga madaraja kwenda mbele hatuko bize kufukua makaburi. Kiukweli nchi inahitaji kuwa na mwanzo mpya. Watu wanajenga madaraja kwenda mbele sio kurudi nyuma: badala ya kuangalia tunafikaje kule mbele tunabakia kufukua makaburi ya miaka kumi iliyopita eti ooh Lowassa hivi oooh Lowassa vile inahusu? tunataka kujua kesho itakuwa njema?

nini misingi ya kututoa hapa? je hayo yaliyotendeka nyuma yatatokea tena? kwanini ilishindikana kuyashughulikia ipasavyo na kwa wakati? hakuna haja ya kukanyaga tu tope hapohapo na kujipaka kinye.s.i bila kupiga hatua ya kusonga mbele zaidi. Mtu mmoja hawezi kuondoa ufisadi tena kwa akili na mawazo yake. Kitakachotokea hapo ni kushughulikia maadui zake na wa rafiki zake na kuwaacha jamaa na marafiki wanaonuka ufisadi wakidunda mitaani. Lazima kiwepo kigezo kwanza na sheria ya kumnasa fisadi na kibano cha maadili yatakayomladhimisha rais afunge hata wanae bila hilo ni kujilisha upepo. Kigezo hiki kipo UKAWA ambacho ni rasimu ya Warioba ambayo hao wanaojinasibu kuondoa ufisadi walishaikataa.

Utaondoaje ufisadi huku unaikataa nyenzo ya kufanyia utekelezaji? Ili mradi Lowassa ameikubali nyenzo kwa kuja UKAWA ndie pekee atamaliza ufisadi atake asitake manake katiba itamtupa nje asipofanya hivyo. Mtu anajinasibu kuleta maendeleo, kusomesha bure, n.k. pesa ataitoa wapi wakati gesi na mali asili zote washaziuza na kuchukua chao? yuko tayari kufuta hiyo mikataba ya ovyo na kuandika mipya yenye tija kwa taifa tupate mahela? au ni yaleyale ya kukamua mama ntilie na machinga ili kodi ipaitikane? hebu tusidanganyane bwana na kupoteza wakati kupiga porojo zisizo na tija

Katiba ya wananchi?

Prof. Lipumba yupo wapi?
 
Last edited by a moderator:
huu ni umbwiga mkubwa sana aiseee picha hakuna zaidi ya maneno tuuu.

Aliyeanzisha thread anaihujumu UKAWA.... Mpaka sasa watu ni wengi halafu haweki picha hata moja
 
Back
Top Bottom