Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kesi ya jinai haiozi wala hairithiwi ujumbe ndio huo Dr wa sheria amekwisha sema ushahidi ulihifadhiwa. Mkilazimisha ikulu lazimwa aswekwe lockup, alianza Masha hiyo ni salamu. Magufuli keshawatonya mahakama maalum ioooo inakuja. Na yeye EL aseme km ktk sera yake atajifungulia mahakama imchunguze.

Uzuri hiyo mahakama haitamwacha Kikwete and Co kuanzia jinamizi la IPTL mwaka 1994 mpaka escrow ya majuzi, ufisadi ktk miradi ya barabara, mabehewa fake ya train nk. Pia tunamtaka Mwakyembe amalizie ule ushahidi aliosema ameuficha ambao kama angeutoa serikali yote ingeanguka. Naamini serikali yote ni kuanzia rais mwenyewe
 
Watu Wanazidi Kumiminika Katika Viwanja Vya Jangwani Toka Jana Mafuliko Si Mafuliko, Tsunami Si TSunami Ama Hakika Historia Inaenda Kuandikwa Katika Viwanja Hivi, Hii Haijawai Kutokea Watu Wamefunga Ofic Zao Watu Wametoloka Makazini, Umebaki Wewe Tu, Nawewe Toloka Uje Usipende Kuadisiwa
 
Nyenyere

Tatizo lako ni kutojua agenda inayosimamiwa na Lowassa na UKAWA yake; agenda hapa ni rasimu ya Warioba ambayo ina kila kitu; ina dawa ya ufisadi, maadili ya uongozi, kibano cha mikataba feki, upotevu wa rasilimali, nk. tunajenga madaraja kwenda mbele hatuko bize kufukua makaburi. Kiukweli nchi inahitaji kuwa na mwanzo mpya. Watu wanajenga madaraja kwenda mbele sio kurudi nyuma: badala ya kuangalia tunafikaje kule mbele tunabakia kufukua makaburi ya miaka kumi iliyopita eti ooh Lowassa hivi oooh Lowassa vile inahusu? tunataka kujua kesho itakuwa njema?

nini misingi ya kututoa hapa? je hayo yaliyotendeka nyuma yatatokea tena? kwanini ilishindikana kuyashughulikia ipasavyo na kwa wakati? hakuna haja ya kukanyaga tu tope hapohapo na kujipaka kinye.s.i bila kupiga hatua ya kusonga mbele zaidi. Mtu mmoja hawezi kuondoa ufisadi tena kwa akili na mawazo yake. Kitakachotokea hapo ni kushughulikia maadui zake na wa rafiki zake na kuwaacha jamaa na marafiki wanaonuka ufisadi wakidunda mitaani. Lazima kiwepo kigezo kwanza na sheria ya kumnasa fisadi na kibano cha maadili yatakayomladhimisha rais afunge hata wanae bila hilo ni kujilisha upepo. Kigezo hiki kipo UKAWA ambacho ni rasimu ya Warioba ambayo hao wanaojinasibu kuondoa ufisadi walishaikataa.

Utaondoaje ufisadi huku unaikataa nyenzo ya kufanyia utekelezaji? Ili mradi Lowassa ameikubali nyenzo kwa kuja UKAWA ndie pekee atamaliza ufisadi atake asitake manake katiba itamtupa nje asipofanya hivyo. Mtu anajinasibu kuleta maendeleo, kusomesha bure, n.k. pesa ataitoa wapi wakati gesi na mali asili zote washaziuza na kuchukua chao? yuko tayari kufuta hiyo mikataba ya ovyo na kuandika mipya yenye tija kwa taifa tupate mahela? au ni yaleyale ya kukamua mama ntilie na machinga ili kodi ipaitikane? hebu tusidanganyane bwana na kupoteza wakati kupiga porojo zisizo na tija
 
Last edited by a moderator:
tupo jangwani mvua si lolote kwetu...
Kwanza ikinyesha ndio vizuri kwasababu inapunguza joto watu hawataanguka kwa kukosa hewa na maji mwilini. Inyeshe tu ndio baraka.
 
Jamanimbona hatuoni mapicha, msiache nikaanza kujuta jana nimenunua power bank ili niweze kufuatilia hii kitu kila hatua.
 
Habari wakuu,

Leo ni uzinduzi wa kampeni kwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambazo zinafanyika leo Jumamosi tarehe 29 Agosti 2015 katika viwanja vya Jangwani.

Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojiri kwenye kampeni za leo.

============

​

tupo pamoja
 
mods wana upendeleo sana huwa wanapenda kuingilia thread za chadema ni upuuuzi kabisa kuna uzi ulianzishwa jana na wanaofahamika humu kama makada wa chadema mida yaa saa 6 akaunganisha na maandalizi .....leo huu uzi hajaunganisha lakni hata mfanyeje update zitapatikana tuuu tv zote zinaonyesha...........
 
Kokoto zimeanza kusombewa jangwani..!!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1440837003.413107.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1440837003.413107.jpg
    25.3 KB · Views: 829
Back
Top Bottom