Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Wewe uwe na aibu,vipaumbele amevita,ameomba radhi kwa muda kuwa mchache,amezingatia muda waliopewa kisheria mimi ni ccm lakini hapo hapana,uvivu wako wa kusoma usiuweke hadharani hivi ulitaka asiheshimu sheria kwakupisha muda uliowekwa, acha ushabiki wa hovyo haulisaidii taifa,umezoea maneno mengi vitendo hakuna, mabadiliko yanaanzia kwenye matumizi mazuri ya muda.
 

Umeonaa mbaya sana
 

1. Elimu
2. Elimu
3. Elimu
Elimu bure hadi Chuo kikuu.

4. Afya. Dispensary kila kijiji.

5. Kilimo. Kilimo cha kisasa pamoja na kuhakikisha kwamba wakulima wakikopwa mazao yao wanalipwa na riba.

6. Ujenzi mpya wa reli ya kati.

7. Kuboresha huduma ya mawasiliano.

Hayo ni machache ya aliyoongea. Upo hapo?
 

Mbona umesahau kuorodhesha wizi na ufisadi wa ESCROW,EPA,MEREMETA,DEEP GREEN,KAGODA,MABEHEWA FEKI,FIDIA YA KULIPA MAKANDARASI YA SH 900 BILLION?
 
BODABODA NA MAMANTILIE DAR ES SALAAM

Hatimaye mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo bodaboda na mamantilie wamesikitika sana kwa kilichotokea katika ufunguzi wa kampeni za mzee Lowasa.

Awali wanainchi walitegemea kama siku yao muhimu ya kusikiliza ilani ya Chadema, ambayo ndiyo ingekuwa chachu ya maendeleo yao hapo badae lakini wamesikitika mara baada ya mzee kushindwa kuongea na kuwambia wanainchi ILANI ITAWEKWA KTK WEBSITE YA CHAMA, jambo ambalo limezidi kuwapa upofu na kuwa na mashaka na uwezo wa mzee Lowasa pamoja na watu wanaomzunguka.

Hata hivo bodaboda na mamantilie wamesema wao hawana uwezo wa kusoma kutokana na kukosa elimu, swala ambalo walitegemea mgombea analifahamu vema hali ambayo imekuwa tofauti.

Kwa mujibu wa maelezo ya maelezo ya wanainchi hao, sasa wameamua kumuunga mkono Dr John Pombe Magufuli.
 
hawakua wezi na pia hawakuwa wamepelekwa mahakamani.
EPA ilikua ni case ya watu kuchukua pesa za epa kama mkopo na kutozilipa.
huo siyu wizi ni bad loan

wangekua sio wezi wengine wasingeingia gerezani... usitufanye wote hatujui kitu, EPA mliiba na bado mkasameheana tena bungeni!!! vidagaa mkawafunga
 

Pole mkuu, tatizo hana uwezo wa kujenga hoja zenye mashiko..... Hio ndo fact
 
Hizo ni extra babuu, ni sawa na magufuli alivyowaambia uvccm hatawaangusha.
Kufungwa kwa watu hao kunaleta hisia ya uonevu kwa wananchi wengi, akipita yaliyopita si ndwele wanapata msamaa wa raisi, tunafurahia ushindi

Haya wananchi wenyewe walikuwa wanapiga kelele Fulani Fulani. Ikabidi akidhi kiu yao! La Balali kwa mfano kuna watu walibeba bango kubwa limeandikwa ukienda ikulu tunataka umlete balali
 
Watanzania wamezoea kudanganya

Mtu aje aseme nitajenga fly overs Tazara, nitahakikisha barabara sita chalinze mpk Dar, ndio ujinga ujinga wetu.

Usiseme mengi kuliko inavohtajika, maana kwa miaka mi 5 huwezi fanya yote. Kasema vitu vyenye athari kwa watanzania wote, sio wana Dar es salaam tu.

1. Elimu
2.Elimu
3.Elimu
4. Reli ya kati
5.Shirika la Ndege
6.Maji vijijini

Wasiojua kuongea ndio Watendaji

Lowasa will be our next president by the Grace of God

1
 
Sisi tupo hapa illinois chuoni tunawaombea tu

vipi hizi picha siyo za kutengenezwa na computer kama alivyodai mkuu?
 
kama kijana Wa Tanzania napenda kuona mabadiliko yanatokea katika nchi hii. nchi inahitaji kiongozi na mfumo safi Wa kuiongoza katika kupambana na matatizo mbalimbali. niliwategemea sana CDM na vyama vinavyo unda UKAWA nikiwa na imani kubwa kuwa vitaleta mabadiliko na kuikomboa nchi kutoka katika matatizo tuliyo nayo sasa! ila kuanzia Leo nimepoteza matumaini kabisa ya kuyapata hayo mabadiliko. UKAWA wameshindwa kuweka mgombea ambaye angeweza kutatua shida za watanzania. lowasa sio mtu wa kuleta mabadiliko hata siku moja, mabadiliko Tanzania baadae saaaaaaana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…