Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Yaan Lowasa anataka tumchague ili amtoe babu seya!!!! Yaan hio ndo sera ya kumpeleka ikulu. Kweli huu ni uchiziiiii.... Huyu jamaa anawaaibisha UKAWA.......
hio sio sera hayo alijibu maoni ya wananchi vipaumbele alitaja vitatu kuokoa muda ilani nza nenda web ya chadema nzi wa kijani na njano wewe.ilani hio itanadiwa vyema kwenye kampeni aliamua kuruka kiunzi cha muda na tutaicopy na kuipest huku teh teh teh
 
Yaani siku ya kutembea uchi ndio unakutana na baba mkwe!yaani leo nilitegemea watazima moto kwa hoja na sera!ni asilimia chache sana ya watu wanaoweza kutumia internet wakapata taarifa!leo unaniambia nifate sera kwenye Website nikasome?

Mama ntilie walio wengi hajui hata hiyo website ni nini!boda pia hajui website ni nini na anaipataje!leo Wananchi wameitika tena kishindo kikuu halafu mnapoteza muda kiasi hicho

Kweli bado hamjajipanga kuingia ikulu kabisaaa kwa mwendo huu,siasa chafu kuliko za CCM

nimefurahi sijamsapoti wala kubadili mawazo kumfata ukawa, watajuta leo kumsimamisha kweli ndio maana alikattwa. anataka kurudisha pesa za kampeni wananchi tukome huyu hapana kabisa.
 
Binafsi nimebaki na maswali mengi sana ya kujiuliza.Ni watu wangapi waliomwelewa Lowasa?.Lowasa ameonyesha udhaifu wake wa afya na wa kuongea, neno moja anajazia peopleees sijasikia sera hata moja wala sijasikia lolote la maana kutoka kwake. Natambua kwamba mkutano wa leo jangwani ilikuwa maalumu kwa ajili yake kujinadi na kunadi sera zake matokeo yake analeta habari za mtandao je ni watanzania wangapi wanaoweza kuingia kwenye website ya CDM na kuisoma hiyo hotuba!
Kama Ukawa hawatabadili system ya mgombea wao,mgombea wa Chichiem ataendelea kuaminiwa na wananchi walio wengi!

#HapaKaziTu. Ukawa Kwisha Habari yao.
 
Huyu lofa kashindwa tena kuongea. Halafu bado mnataka awe Rais?

Huo ni zaidi ya upumbavu huo ni uzumbukuku.

Ahahaha mie nilivyoona nyomi la wananchi ikabaki kidoogo na mie niliunge mkono chama la home!nashangaa wameharibu kuliko hata Magufuri na CCM yake!wameshindwa kabisa kutumia uwingi ule wa watu kuimaliza CCM kwa sera na hoja!70% leo wamefeli,wanainchi waliitikia wito ila Ulofa na Upumbavu ukachukua nafasi
 
Hotuba ya lowasa ni aibu tupu kama ya mtoto wa darasa la nne ni kama hakujiandaa.
 
Wakuu salaam. Nikiwa mtanzania wa kawaida kabisa ambaye napima mambo ya kisiasa kwa vigezo vya msingi kuliko ushabiki, hatimaye nimejiwekea mambo machache tu na ya kawaida kabisa ambayo UKAWA na Lowassa wanatakiwa kuyafafanua leo ili nijenge imani kwao. Mambo haya ni :

1. Kwa kuwa Lowasa kati ya mwaka 1997 na 2000 alikuwa akiiongoza wizara ya kuondoa umasikini, alifanya nini kinachompambanua kwamba anachukia umasikini? Hapa mfumo si hoja yenye tija sana kwa sababu mifumo mibovu ina kawaida ya kuwajenga viongozi bora kwani hujipambanua wazi wazi.

2. Kati ya mwaka 1993 na 1995 Lowassa alikuwa akiiongoza wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alifanya jambo gani la kumtofautisha na watendaji wengine? Wananchi wamkumbuke kwa lipi katika wizara hiyo ambayo ilikuwa maalum kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na kuondoka katika dimbwi la umasikinttti.

3. Mwaka 2000 - 2005 huyu mheshimiwa aliongoza wizara ya maji na mifugo. Ninachotaka kujua ni kwa nini katika kipindi chake cha uongozi migogoro ya wakulima na wafugaji ilizaliwa. Ni dhahiri kuwa ni wakati huu wafugaji walipata nguvu ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha tatizo ambalo limekuwa sugu hata leo.

UKAWA kwa upande wao naomba watueleze ni kwa nini tuendelee kuwaamini iwapo wamerudi kukanusha yale waliyotuaminisha hata tukawapenda.

1. Vita dhidi ya ufisadi. CHADEMA walijipambanua kama wapiganaji wa kweli dhidi ya ufisadi. Hii ndio sera ambayo bila ubishi iliwapatia umaarufu mkubwa.

CHADEMA wasimame na kukiri hadharani leo kwamba yale waliyotuaminisha kwa muda mrefu juu ya ufisadi ni uongo. Haitoshi tu kusema Lowassa hakuwahi kutueleza ukweli kuhusu Richmond. Hii ni ushahidi kuwa Chadema si chama makini hata kidogo. Kinaendesha siasa za kitapeli kwa malengo binafsi.

Tena msamaha huu uende mbali zaidi kukiri kuwa yale mliyokuwa mkijidai kuwa ni ushahidi mzito mlionao ulikuwa uongo ili kupata huruma ya wananchi.

2. CHADEMA ikiri na kuomba radhi kwa watanzania kwa kitendo chake cha kukiuka misingi kiliyojiapiza kuisimamia na kukanyaga demokrasia. Msamaha uombwe dhidi ya dharau na kejeli walizofanyiwa waliokipigania chama hata kukifikisha hapo kilipo. Mchakato wa kupata wagombea katika ngazi za urais na ubunge umegubikwa na sintofahamu kiasi cha kusababisha mgawanyiko wa kisiasa. Intelijensia ya CHADEMA imekuwa juu ya matakwa ya wananchi.

3. CHADEMA iombe radhi kwa utapeli wa kisiasa ilioufanya dhidi ya mauaji ya Olasiti. Ule mkanda unaoonyesha wauaji wakitekeleza mauaji hayo umeota mbawa. Hizi ni siasa za kitapeli. Kutafuta huruma za wananchi kwa hila.

4. CHADEMA wafafanue mipaka ya mashirikiano yao na CUF hasa linapokuja suala tata na nyeti kwa maslahi ya nchi la sera ya ULIBERALI. Watanzania tumeaminishwa na CHADEMA kwamba CUF wanasimamia ushoga na wanauunga mkono. Naomba CHADEMA waelezee msimamo wao, ama waombe radhi kwa kuwazushia uongo CUF.

Haya ni baadhi ya masuala ya msingi sana ambayo natarajia mkutano wa leo wa UKAWA utayatolea ufafanuzi.

Tujadili kwa hoja, matusi mwiko. Lizaboni, RIZ1, et al

Watanzania zaidi ya 20milioni wameahidi kumchagua kwa kura za ndio mheshimiwa lowasa na hivyo kumuwezesha kuwa rais wa hawamu ya tano wa JMT.
 
Trully!? Lowassa KACHEMSHA safari yake ya MATUMIZI imeishia hapo! 10 min mtu utaongea nn!? Kazi nyepesi ya kumtongoza binti yeyote haitumii huo muda sembuse kupiga promo za nguvu kuwashawishi watu kwenda kukusanyana na kusikiliza dk kumi!? Kweli!? Mpira Pesa ni sawa na kuokota malaya kimboka kwa dk hizo kumi na mzigo anakupa so Lowassa kwa style hiyo utawapata wa kimboka!
 
Kiukweli Lowassa anapendwa sana na makundi mbalimbali lakini kunaumuhimu wa CHADEMA kumuandaa katika upande wa kutoa hotuba.
 
1.Nitamtoa babu Seya.
2.Nitamleta Balal.
3.Nitawatoa ndani mashekh wa Zanzibar.
Na still bado tuakamshangilia kwa vifijo na vigerere.
Hivi babu Seya na Balal pamoja na hao mashekh wa Zanzibar watahusika vipi kuimarisha uchumi wetu na kutuondolea umasikini?
Je watashusha bei ya umeme,chakula,mafuta,sukari nk?
Ahsante mzee Mkapa,sasa nimekuelewa.
Sisi ni wapumbavu na malofa!!!
Ngoja niwahi usafiri wa kurudi kwangu Ukonga maana nimevurugwa sana na huyu mzee na ninajuta kuja jangwani leo!!!

Hizo ni extra babuu, ni sawa na magufuli alivyowaambia uvccm hatawaangusha.
Kufungwa kwa watu hao kunaleta hisia ya uonevu kwa wananchi wengi, akipita yaliyopita si ndwele wanapata msamaa wa raisi, tunafurahia ushindi
 
Pia nipeni mfano wa taifa japo moja ambalo limefanikiw kutoa elimu bure toka elimu ya awali mpaka chuo kikuu.....mnatudharau sana hata sie wasomi kwakutufanya wapumbuvu tusio kuwa na uelewa.....ovyo kabisa
...
 
WanaJF,

Nipo njiani kuelekea nyumbani kwangu nikiwa natoka hapa viwanjwa vya jangwani.

Kusema ukweli, siku ya leo nilitaka kumsikiliza ndugu Lowassa kwa umakini mkubwa sana, ili kama nikishawishika nimpe kura yangu.

Lakini kwa masikitiko makubwa sana ndugu zangu wanaJF, nimeishia kuambulia website ya CHADEMA!!!

Shauku yangu kubwa ya kupata mabadiliko kupitia UKAWA imeyeyuka ghafla, kwa mantiki hiyo, sina budi kuwapa CCM kura ya urais kwa kuwa bila shaka yoyote nilitathmini yale aliyosema Magufuli na nikaona yanatekelezeka.

Kwa wale ambao hamkupata fursa ya kwenda jangwani, nawahakikishia kuwa hamjapoteza lolote. Sisi tuliokuwa hapa jangwani tumeondoka vichwa chini, Lowassa ametuangusha tena kwa mara nyingine.

Aidha, huyu Lowassa anasema Watanzania wana shida na umaskini mkubwa. Je, huo uwezo wa Watanzania kuwa na vifaa ikiwemo smartphones na Laptop, au kwa maneno mengine, huo uwe

kumbe unauwezo wa kuingia jf y not web ya chadema ama nawe unataka tu uonekane unajaza server humu
 
kikwete alivyowasamehe wezi wa EPA aliingilia kazi ya nani... au alikua jaji kipindi hicho

hawakua wezi na pia hawakuwa wamepelekwa mahakamani.
EPA ilikua ni case ya watu kuchukua pesa za epa kama mkopo na kutozilipa.
huo siyu wizi ni bad loan
 
Babu seya amelawiti watoto halafu huyu lofa anasema atamtoa, amtoe yeye ni mahakama? Na akisha mtoa itawasaidia nini watanzania? Kweli ukawa wamechemsha.Sasa ndio nimeelewa kwanini ccm walimpiga chini.

Hata mimi nashangaa, lakini wito wa kumtoa babu Seya ulianzia Mbeya. Inawezekana kuna lililojificha, ngoja tusubiri.
 
Back
Top Bottom