Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Are you talking to me? Sasa ulitaka mapokezi ya huyu jamaa,
View attachment 281770
Watu wa Chadema wawe barabarani? Hao ni wenzake ndani ya CCM, ndio maana alisema naomba wale wa peoples wanipe kura.

ha ha ha

attachment.php
 
Huyu lofa kashindwa tena kuongea. Halafu bado mnataka awe Rais?

Huo ni zaidi ya upumbavu huo ni uzumbukuku.
 
Yaani siku ya kutembea uchi ndio unakutana na baba mkwe!yaani leo nilitegemea watazima moto kwa hoja na sera!ni asilimia chache sana ya watu wanaoweza kutumia internet wakapata taarifa!leo unaniambia nifate sera kwenye Website nikasome?

Mama ntilie walio wengi hajui hata hiyo website ni nini!boda pia hajui website ni nini na anaipataje!leo Wananchi wameitika tena kishindo kikuu halafu mnapoteza muda kiasi hicho

Kweli bado hamjajipanga kuingia ikulu kabisaaa kwa mwendo huu,siasa chafu kuliko za CCM

Kwani magufuri aliongea sera gani? Kikwete aliyeongea mengi alitekeleza yapi? Zaidi ya serikali kukumbwa na kashifa kibao. Mzee kataja vipaumbele ambavyo vimetambuliwa na ilan, au ulitaka na utkelezaji uwe leo? Watanzania mtu akawadanganya kwa kuongea mambo rundo ndo mnahisi ndo bora.
 
Bado Lowasa hajakonga nyoyo kwa kuinadi ilani vizuri
Bora kuwa muwazi kuliko kuidhurumu nafsi yako, watu tumechoka ccm ila Lowassa bado hajakidhi matarajio ya wengi.

Ila kwa sababu ccm imechokwa hakuna namna.!
 
Tatizo ni muda.Mmepewa majibu ya Richmond mmekosa njia mnaanza kukimbilia kwenye issue ya kuongea.Tunacheza na muda sisi si kama mambumbu wa Lumumba waliopoteza muda kwa Show za kina diamonda na kuzidisha muda..
 
Jamani Jamani sasa Mabadiliko Ndio haya Jamani Mungu wangu wangu Ccm watatawala Muda mrefu sanaa

Yaani CCM itatutawala mpaka Yesu arudi kama wapinzani wenyewe ni hawanaoongozwa na watu wakubadilisha gia angani.... Tumewekewa placebo tu, hakuna wapinzani na mwaka huu tumejua rangi zao!
 
Nimeipenda sana hii. Na nina imani kabisa inawezekana 100%. Hotuba nzuri sana, fupi yenye maana kubwa.
 
WanaJF,

Nipo njiani kuelekea nyumbani kwangu nikiwa natoka hapa viwanjwa vya jangwani.

Kusema ukweli, siku ya leo nilitaka kumsikiliza ndugu Lowassa kwa umakini mkubwa sana, ili kama nikishawishika nimpe kura yangu.

Lakini kwa masikitiko makubwa sana ndugu zangu wanaJF, nimeishia kuambulia website ya CHADEMA!!!

Shauku yangu kubwa ya kupata mabadiliko kupitia UKAWA imeyeyuka ghafla, kwa mantiki hiyo, sina budi kuwapa CCM kura ya urais kwa kuwa bila shaka yoyote nilitathmini yale aliyosema Magufuli na nikaona yanatekelezeka.

Kwa wale ambao hamkupata fursa ya kwenda jangwani, nawahakikishia kuwa hamjapoteza lolote. Sisi tuliokuwa hapa jangwani tumeondoka vichwa chini, Lowassa ametuangusha tena kwa mara nyingine.

Aidha, huyu Lowassa anasema Watanzania wana shida na umaskini mkubwa. Je, huo uwezo wa Watanzania kuwa na vifaa ikiwemo smartphones na Laptop, au kwa maneno mengine, huo uwe
 
unazungumzia mstabali wa Watanzania miaka 50 mbele kwa dakika 10 za kuzungumizia bab seya
 
dah naomba kazi ya kumuandikia hotuba lowassa for free nadhani chadema wameshindwa ktk sector ya hotuba kwa kiongozi wetu nimekuwa very very very disappoint on that dah

mpaka leo hujapata kazi ya kufanya, ccm si walisema wametengeneza ajira milioni moja!!! wamekusahau kada
 
Jamani kama ni mawazo yangu tu nisamehewe jamani,nahisi Lowassa,kazungumza kifupi sana,uzinduzi kabisa wa kampeni kweli na umati wote huu.

Mkutano wa uzinduzi kabisa?

Hachekicheki hovyooo?
 
Lowassa amehutubia dakika 11 yaani kuanzia SAA 11.41 hadi saa 11.52. Hakika hawezi mikikimikiki ya kwenda IKULU.
Kwa hili watanzania tujifunze.

Ni bora huyu ametumia dakika 11 kuongea facts na hoja zenye mashiko kuliko wale waliotumia wakata vyuno jukwaani bila kusahau kuporomosha matusi!!!

Nnachoanini ni kwamba muongea mengi huwa anafanya machache na MUONGEA MACHACHE YENYE mashiko huwa anafanya mengi kwa vitendo!!!

UKAWA is the correct answer for our beloved Tanzania!!! We endelea kupiga kelele sisi twasonga na Lowassa wetu!!
 
Babu seya amelawiti watoto halafu huyu lofa anasema atamtoa, amtoe yeye ni mahakama? Na akisha mtoa itawasaidia nini watanzania? Kweli ukawa wamechemsha.Sasa ndio nimeelewa kwanini ccm walimpiga chini.
 
utazidi kumsikia ila kipimo cha utendaji kazi sio kuongea..angalia vipaumbele vyake ..na jinsi atakavyo vitekeleza....
 
Back
Top Bottom